Ukichoka na Mishe za Mjini Dar, Kajipumzishe Pugu “Ushoroba”

Ukichoka na Mishe za Mjini Dar, Kajipumzishe Pugu “Ushoroba”

Kuna siku nilipita relini kutoka tabata relini hadi mwanachi.
Lile eneo pale kati pametulia mno, kimyaa ni sauti za ndege, maji ya mto na upepo tu.
Husikii kelele za barabarani, nadhani huko kunanifaa sana, kelele za hapa jijini zinaumiza kichwa kichizi
 
Mambo vipi wazee?
View attachment 3000992
Kuna pahala panaitwa Pugu Kazimzumbwi alhamarufu Ushoroba.
Ni pazuri sana kwa mkazi wa Dar au Pwani anaetaka kupumzika siku moja au weekend kuzipisha kelele za bodaboda, bajaji, magari, wauza sumu ya mende, etc. Nimeenda mara kadhaa na weekend hii pia nilienda.

Utangulizi

Pugu Kazimzumbwi ni safu ya misitu iliyo chini ya TFS (Tanzania Forestly Service) inayopatikana Wilaya ya Kisarawe, mwanzoni kabisa ukitokeq Dar es Salaam. Kwa wenyeji kidogo, ni opposite na shule ya sekondari Minaki.


Unafikaje?

Kama unatumia usafiri binafsi, ukitoka Gongo la Mboto, unaendelea na safari hadi mataa ya Pugu, unaacha njia ya Chanika we unaendelea na ya Kisarawe. Mwanzoni ukivuka kibao cha Karibu Wilaya ya Pwani, mbele kidogo Kushoto utaziona ofisi zao.
View attachment 3000910

Ukifika Ofisini

View attachment 3000912
Watakupokea, watakupa introduction kidogo ya utalii uliopo na activities zilizopo na gharama zake.
View attachment 3000913

Gharama

Kuna gharama za aina mbili hapa, mosi ni gharama za kuingia. Hapa mkiwa wawili mtalipa elfu 19 pamoja na gharama ya tourguide hapo hapo na gharama za gari kuingia na gari hapo hapo.
View attachment 3000997
Malipo ni kwa control no. Kuna 5% inalipwa cash pale inaenda serikalini ila ni kama buku tu. Unapewa risiti. Na malipo ya pili ni options za activities utakazo amua kufanya ukiwa uko ndani, tutazidiscuss kidogo.


Utalii na Activities zilizopo
View attachment 3000924
Usitegemee makubwa kwasababu hii sio national park wala game reserve, huu ni msitu wa asili, kwahiyo baadhi ya vitu ambavyo utaviona maybe kwako ni vya kawaida, mfano:

Hiking/Kupanda mlima
View attachment 3000906
Hapa utapanda mlima karibia 1.5km utatumia kama dk 30-50 kutokana na stamina yenu. Ukiwa na maji 1L na mavazi sahihi itapendeza zaidi.

Ukifika juu kileleni kuna view point nzuri utafanikiwa kuona msitu mzima pamoja na kuona shehemu kubwa sana ya Dar es Salaam.
View attachment 3000899
Ukiwa juu utaona ni jinsi gani Dar hatujafanikiwa kujenga mji wetu kwa kuzingatia mipango miji.

Kayaking /Kuendesha viboat flani
View attachment 3000917
Hii ni option, utalipia elfu 10 na mnakaa wawili wawili au watatu au unaweza endeshwa.

Ukiwa mjanja vizia muda hakuna watu wengi kwenye foreni uta spend muda mwingi zaidi majini.

Camping
View attachment 3000904
Wazee wa kulala msituni inawahusu. Hii ni package kwa mtu anaetaka kuspend usiku pahala tulivu huku akiotea moto, kuchoma nyama, kunywa bia na kua karibu zaidi na nature na mpenzi wake.

Gharama itategemea na size ya tent ila
Kwa tent la watu wawili ni elfu 25 na kama una tent lako gharama inazidi kua ndogo.

Sport Fishing

Kwa wanaopenda kuvua samaki, ukilipia utaazimishwa ndoana uweze kuvua. Ila hautaondoka na samaki. Just for fun.

Unaweza kuomba moto though uweze kuwachoma au kuwala. Samaki wanaopatikana ni perege na kambare.

Location za Picha
View attachment 3000918(Hiyo Jordan Showoff tu)

View attachment 3000964
View attachment 3001000
Kuna baadhi ya watu wanaenda kwaajili ya kupiga picha za kumbukumbu mfano harusi, birthday au vikao binafsi.

Ila kuingia na camera au drone kuna gharama yake itabidi ulipie.

Kuona Mzimu wa Mavoga

Kuna pahala ambapo mzimu wa Mavoga ambapo wenyeji wa Kisarawe Wazaramo walikua wanaenda kuombea dua. Utaona ayo mapango na kujifunza.

Sikwenda kwasababu masharti moja wapo usiwe umelewa, mwanamke asiwe MP na jana yake usitoke kufanya tendo, katika ayo matatu mawili nishafeli. Nikaona isiwe shida.

Lake View
View attachment 3000914
View attachment 3000953Kuna ilo ziwa ndio laitwa Ushoroba au Minaki Dam ambalo lazamani kabla DAWASA haijafika Kisarawe lilikua linasupply maji wilayani na vijijini vya jirani.

Utaona miundombinu iliobakia mfano pumphouse na mabomba.

Kuendesha baiskeli

Ukienda na bike yako kuna trail za kuendesha kama utakua interested. Ila hawana baiki za kukodisha.

Kuna Batman caves

Ingawa lipo nje ya huu msitu ila nashauri nenda kalitembelee.

Viumbe waliopo je?

Kusema kweli hawana viumbe uko zaidi ya kobe wachache, kenge, komba, nyani, na viumbe wadogo wadogo ambao sio issue.View attachment 3000996
View attachment 3000995
Kiumbe pekee special ni Pazi mwenye bendera ya Tanzania, nadhani ndio aliowekwa kwenye round about ya Mlimani City pale.

Uoto wa Asili
View attachment 3000916
Kuna uoto wa aina nyingi ila special sana ni mti wa Mpugupugu ambao ndionumezaa jina Pugu. Inasemekana hadi leo huu mti unapatikana Tanzania pekee na katika ilo eneo la Pugu tu. Mti huu ni dawa na wataalamu mbalimbali uwa wanakuja kuchukua sample ya mti kwa tafiti za Kibotania.



Huduma za ziada

Hadi sasa, wameboresha sana huduma za vyoo na mabafu yamekua ya kisasa zaidi.
View attachment 3001003
Vile vile kuna muwekezaji amefungua restaurant anauza vinywaji na vyakula vya aina mbali mbali ingawa kidogo ni overpriced kama upo na tight budget nashauri beba takeaway au kula kabisa. Mfano Chips kavu kwa Buku 3 so kadiria mfuko wako.
View attachment 3000902View attachment 3000903
View attachment 3000965
Vitu vya kuzingatia

Kama unaenda daytrip beba maji vinywaji na vyakula ukiweza.

Zingatia usafi, usitupe tupe takataka ovyo, maana lile eneo ni safi na limewapa ajira vijana wengi sana.

Ukienda kucamp kumbuka mashuka, mito na taa (unaweza kutumia simu yako), usiogope umeme wa kuchajia upo.

Bwawa hawaruhusu kuogelea ila watajenga swimming pool wamesema.

Mi nimeona tushee hayo, mwingine aongezee.
Asante sana sanaa saaaana
 
Makadirio:

Kuingia wawili full kabisa 20k
Tent 25-30k
Mlinzi 5k au 10k
The rest ni kula, vinywaji, basi.

So approximately 60-70k
Gharama za watoto viingilio, michezo etc zipoje?
 
Kuna anejua pia ishu / details za Mkuranga forest reserves?? Kama yupo atiririke kama jamaa
 
"Kuna 5% inalipwa cash pale inaenda serikalini ila ni kama buku tu. Unapewa risiti. Na malipo ya pili ni options za activities utakazo amua kufanya ukiwa uko ndani, tutazidiscuss kidogo."

👆👆
....................
Ninaomba niongezee hapo kwenye 5%.

Nimewahi kufanya kazi Pugu Ushoroba katika kukusanya malipo ya 5%.

Asilimia 5% hupatikana hivi: mfano, mteja akilipia gharama ya Tshs 100,000/= kwa control namba na kupewa risiti, basi itambidi alipie Tshs elfu 5,000/= na kupewa risiti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.

Kwa hiyo kwa mfano huo, mteja atakuwa amelipia jumla ya Tshs 105,000/=.

Maana yake ni kwamba kiasi cha Tshs 100,000/= kinaenda Serikali Kuu (kupitia TFS), huku Tshs. 5,000/= kinaenda Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ambapo Msitu wa Pugu Kazimzumbwi unapatikana.

Karibuni sana Kisarawe, karibuni Pugu.

cc Guantanamoh
 
Unajikunja kumkaza mtoto wa mtu machakani anapita Cobra sijui Black Mamba wa kizaramo anakutia meno unabaki unagaragara.

Usisahau kuna mdau amesema alipita hapo akaona msitu umezidi kufunga so take care chief.
Msitu una takribani hekta 2,000 na pana hewa safi sana
 
Mad Max Mwanang nimesoma minaki advance, huko chini tulikuwa tunaenda sana nimezurura sana huko chini, tena kipindi hicho hio project ilikuwa bado haijaanza kwaio tulikuwa tunaenda tuu bure hamna wa kutuuliza, asaiv eti nikisikia watu sikuiz wanaenda huko kwa kulipia nashangaa sana, sema ndo hivo mabadiliko serikali imeona i-monetize hilo eneo.

Nakumbuka tulivomaliza necta tulienda huko chini kweny hio Dam tukaogelea(japo mm sikuogelea niliogopa mamba) na kuzurura(japo nilikuwa na mashaka kwasababu huo msibu una chatu wa kutosha)

Huko chini tulikuwa tunaenda kutafuta vyura wa kufanyia practical za biology
😂 😂 😂

Wakati Jocate akiwa DC wa Kisarawe ndiye alichangia hili eneo kuwa maarufu na hata kuwekwa kiingilio palianza wakati huo wa Mwendazake.
 
Imekutoa unyama sana aisee. Sharti moja usitembee haraka haraka.

View attachment 3000980
Rangi kama yangu..
IMG_20240601_083938_907.jpg

Leo na Mimi nimetupia unyama wangu wa Alexander McQueen
 
Back
Top Bottom