Ukienda kwa Nabii T.B. Joshua, jihadhari sana

Hivi nikianzisha kanisa humu ndani si nitapata wafuasi wengi sana.?
 
Kansa mbal sana mzee ,kilema unaemjua wee aende kwa hao fake prophets kama huyo Joshua hawez kupona ,always 'wanapona' usowajuwa
yaan kk acha tu cku utayopata matatizo makubwa unaweza ht gombana na Mungu wako maana ht hao wanaojiita mitume huwa hawapendelei case kubwa haswa zile ambazo zinaonekana physically, wao wantk issue za mapepo au magonjwa ambayo hayaonekan kwa macho ili ht akisema umepona au vip hakuna anayeweza thibitisha, yaan cku ambayo utapata changamoto kubwa ya kiafya ndio utajua kuwa hawa watu sio kabisa
 
so ni unamaanisha ni kweli binadamu tunapata magonjwa kwa sababu ya dhambi tunazotenda? kansa kisukari n.k ni sababu ya dhambi?
 
Mkuu kuna watu hawajawahi kutenda dhambi Ila ni wagonjwa taabani,by the way nimeupenda mwandiko wako,hongera!.
Sababu zinazotufanya tuugue ziko nyingi, mkuu. Dhambi ni mojawapo tu. Kama unamkumbuka Ayubu(wa Biblia) alikuwa mtakatifu sana. Katika nchi aliyoishi hapakuwepo mtu mcha Mungu kama yeye. Lakini majipu mazito yalimuandama na mabalaa mengi: mara kufiwa na watoto, mifugo kuibiwa, nk. Si unajua kwanini hayo yalimpata? Mungu alimruhusu shetani amjaribu Ayubu. Alipoyashinda majaribu yote bila kutenda dhambi, alipona. Kuna mtu mwingine(katika Biblia) watu walimuuliza Yesu kwanini huyo mtu anaumwa, je ni wazazi wake wametenda dhambi au yeye mwenyewe? Yesu akawajibu, huyo hakutenda dhambi wala wazazi wake; bali ugonjwa ule aliupata kwa utukufu wa Mungu! Na magonjwa mengine yanatupata kwa kukosa tu maarifa. Kwa mfano, mtu anakula chips mayai kila siku; matunda hali, mboga za majani hali. Mtu huyo ni rahisi kushambuliwa na Covid-19 maana atakuwa hana kinga ya kutosha mwilini kwa sababu hali vyakula vya kulinda mwili.
 
Ulivyoandika heading na ulivyomalizia ni vitu viwili tofauti mtu yeyote akisoma heading yako atafikiri kuna hatari kule au mambo mabaya
 
hivi kwani tunapatwa na magonjwa kwasababu tunatenda dhambi?
Dhambi ya kung'atwa na mbu, malaria
TB J, alisema CORONA mwisho lini?? Alipotuletea mapichapicha ya kwenda kulala milimani.

Watakuambia ni tarehe za ulimwengu wa roho!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Yani nimejitahidi kusoma najua nikitu chamaana kumbe story looh umenimalizia mb
 
Asante kwa kwa kunipa elimu nzuri ya biblia mkuu,Mungu na akupe haja za moyo wako.amen
 
Mkuu magonjwa yanasababishwa na mambo mengi tu nje ya dhambi.
MTU ni mzinifu hatari na zinaa ni dhambi ila hawapti ukimwi kwa kuwa wanazingatia matumizi bora ya condom.

Mazungu mengi hayajui hata kuomba wala kanisa,ila umri wao Wa kuishi ni miaka themanini.

We zingatia kanuni za afya tu,kula vyakula vya asili,Fanya mazoezi,ishi na watu vizuri,ukiumwa kula mizizi achana na antibiotic za kisasa.

Babu zetu waliishi miaka mingi na hawakuwa na hospital wala kanisa na wqlikuwa hawana magonjwa magonjwa zaidi ya kulogana.
 
Na tena tusitafute miujiza ya mwili, hata ukipona leo hutoishi kimwili milele, hakuna muujiza mkuu kama ule wa kuponywa roho isiangamie.
 
Mungu yupo mbinguni, ingawaje inasemekana pia yupo mahali pote. Duniani ni kushughulika na ya dunia, halafu baadae mbinguni unatashughulika na Mungu, endapo hautaelekea kwa shetani.
 

Ila sio Matapeli hawa kina Gwajima,Lusekelo na wafananao na wao.
 
Tulikua tunauguza mgonjwa wetu hospital ya masista tabora, hali yake haikua nzuri bimkubwa akapata habari pale maeneo ya nje ya hospital kuna kanisa wanatoa huduma ya maombezi
Bumkubwa akiwa katka desperation akaomba nimsindikize ,tulivyofika kanisani tukafunguliwa gate tukakuta watu kibao wamekaa nje wanasubiri kuonanà na nabii, wahudumu wa wa nabii walitupa kipaumbele sababu ya age ya bimkubwa kabla ya kuingia ofisin kwa nabii tukaambia tuvue viatu , then tukaambiwa simu zetu tuziache kwa mlinzi, hapo alarm ikaanza kulia kwa kichwa .
Tukaingia ndani tukafungiwa mlango kwa nje tukawa ndani mule na nabii anavigezo vyote vya kua tapeli kamekaa kunyang'anyi 100% ,kakaniomba mimi nitoke nje abaki bimkubwa peke yake then mimi nitaingia peke yangu
Baada dakika chin ya kumi bimkubwa katoka na chupa mbili za maji madogo ya uhai yameandikwa hayauzwi ya na stika ya picha ya nabii , kumuuliza bimkubwa akasema yale maji kapewa kwa buku nikaona sio mbaya nikama tu katoka nayo shop ,sio huduma ya faida ,kumbe bhana ya maji kalipishwa 20,000/= yule nabii alivyoambiwa tu kuna mgonjwa akasema inabidi apatiwe mafuta chupa 3 na maji manne 70,000/= bimkubwa hakua na na hio hela ,akatoa alio nayo akapewa hizo chupa mbili za maji ,mimi nilkuja kujua siku kadhaambeleni alinificha sababu anajua mimi ningeenda kuanzisha utata ofisin kwa yule tapeli au ningeenda kuwaambia wale watu wa kwenye foleni kwamba mwamba ni tapeli
Rai yangu kwa ndugu zangu wahitaji tafadhalini sana haijalishi unapitia shida gani usikimbilie kwenye huduma za miujiza ya ujanjaujanja huduma zinazotoa huduma kupitia vitu huo ni ushirikina kabisa
Yesu aliwaagiza wanafunzi wake "wa wekeeni mikono yenu wenye shida mbali mbali nao watapata uponyaji"
Sasa haya masuala kuuziana chumvi, maji lesso na stika yametokea wapi ? Kama sio kuzimu
Tena kuna wengi kwenda kuwaona ni hela eti wanaita prophetic consultation fee 😂😂 huwez kuamin kuna watu wasomi kabisa wanalipia hio yaani ukiwa na shida una lose focus hapo ndio unakutana na matapel na mawakala wa kuzimu

Kabla sijasahau.
Mgonjwa wetu alipona kwa maombi tu maana hospital walikua kidizain kama wamesanda pia ametoka hospital hawez kusimama wa kukaa saivi anazurura watu wasome maandiko kuepuka mitego ya shetani vitu vingi vinafanywa na hao manabii sio biblical
 
Matajiri wote wachawi na ni washirikina. Kamwe hawezi kupita kwenye tundu la shindano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…