Sipingi umuhimu wa mtu kuhubiriwa au kufundishwa kwanza then ndio mtu aombewe au ajiombee mwenyewe. Soma mistari ifuatayo kwa makini utaona wazi uponyaji unatangulia kabla ya mafundisho.
Yohana 5:1-8
[1]Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu.
[2]Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano.
[3]Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke.
[4]Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.]
[5]Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane.
[6]Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
[7]Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.
[8]Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.
Marko 10:46-52
46 Wakafika Yeriko. Na Yesu alipokuwa akiondoka pamoja na Wanafunzi wake na umati wa watu, kipofu mmoja, jina lake Barti mayo, mwana wa Timayo, alikuwa ameketi kando kando ya njia, akiomba.
47 Aliposikia kuwa Yesu wa Nazareti alikuwa akipita, akaanza kupiga kelele, “Yesu, Mwana wa Daudi, nionee huruma!”
48 Watu wengi wakamkemea, wakamwambia akae kimya. Lakini yeye alipiga kelele zaidi, “Mwana wa Daudi, nionee huruma!”
49 Yesu akasimama akawaambia, “Mwiteni.” Wakamwita wakamwambia, “Changamka! Usimame, anakuita.”
50 Akatupa vazi lake kando, akaruka juu, akamwendea Yesu. 51 Yesu akamwuliza, “Unataka nikufanyie nini?” Yule kipofu akajibu, “Mwalimu, nataka kuona tena.” 52 Yesu akamwambia, “Nenda, imani yako imekuponya.” Wakati huo huo akaweza kuona, akamfuata Yesu njiani.
Yakobo 5:14
Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana
Umeonaa? Mtu kama anaumwa, awaite wazee wamuombee. Sio wamfundishe kwanza!