Ukienda kwa Nabii T.B. Joshua, jihadhari sana

watu wasome maandiko kuepuka mitego ya shetani
Biblia inafunua siri nyingi za kuepuka matatizo tunayokutana nayo maishani. Lakini watu hawaisomi. Matokeo yake wakikutana na manabii wa uongo wanadanganywa kirahisi. Biblia inasema siku za mwisho manabii wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi. Bila kusoma Biblia na kukaa katika kanisa linalofundisha kweli yote ya Neno la Mungu, ni rahisi kupatwa na hayo ya 'bimkubwa'
 
Dhambi ni nini? tuanzie hapo kwanza....
Dhambi ni uasi.
"Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi."(1 Yoh 3:4).

Uasi ni nini? Ni kuvunja amri na maagizo ya Mungu. Amri na maagizo ya Mungu yameandikwa kwenye Biblia. Kwa mfano, amri mojawapo ya Mungu inasema: "usizini". Mtu akizini anafanya uasi mbele za Mungu, anavunja amri au agizo hilo la Mungu.

Wanaovunja amri za Mungu adhabu yao ni kutupwa katika moto wa milele siku ile ya mwisho. Na wengine chamoto wanaanza kukipata hapahapa duniani.
 
Ni nani anaweza kuwa mtakatifu?
Mtu yeyote akitubu dhambi zake zote na kuziacha na kukubali Yesu awe Bwana na Mwokozi wake, anaokoka. Kwa maneno mengine anatakaswa kwa damu ya Yesu na kufanyika mtakatifu. Watakatifu wapo wengi duniani na Mungu anapendezwa na watu hawa.

Zaburi 16:3​

Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.
 
Uasi unahusisha fikra na mitazamo, tatizo watu wengi wanachanganya matendo maovu na dhambi. Dhambi haipo kwenye matendo, ipo kwenye fikra, ni kitu cha ndani kinachohusu dhamiri....
 

43 Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.


44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.


45 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
Mathayo 12:43-45
 
Mtu yeyote anayejiita Nabii au Mtume halafu mtu huyo anafundisha kuwa YESU KRISTO alikufa Ijumaa na kufufuka Jumapili alfajiri, mtu huyo siyo Nabii wala Mtume wa KWELI.
Tena ikiwa Nabii huyo au Mtume huyo anakubali kuwa YESU KRISTO alizaliwa 25 December na anasheherekea sikukuu hiyo kanisani kwake, basi fahamu kwamba Nabii huyo au Mtume huyo ni wa uongo.
Ili mtu awe Nabii ni lazima kwanza awe amejazwa ROHO MTAKATIFU. Huyo ROHO MTAKATIFU yeye anaijua KWELI na kamwe hafungamani na uongo wa aina yoyote ile. Mtu mwenye ROHO MTAKATIFU huongozwa na huyo ROHO katika KWELI yote sababu huyo ROHO ni ROHO WA MUNGU na siku zote MUNGU hafungamani na uongo.
Ukweli ni kwamba YESU KRISTO hakuzaliwa 25 December na wala hakufa siku ya Ijumaa. Ukweli huu unajulikana na wale tu wenye ROHO MTAKATIFU!!

Tena baada ya wale Mitume 12 na Paulo kuwa Mtume wa 13 ,duniani hakuna Mtume mwingine yeyote yule aliyetumwa na BWANA. Akitokea mtu na kujiita yeye ni Mtume, mtu huyo ni muongo na unapaswa kukaa naye mbali kama vile gonjwa la "corona".
 
Tena ikiwa Nabii huyo au Mtume huyo anakubali kuwa YESU KRISTO alizaliwa 25 December na anasheherekea sikukuu hiyo kanisani kwake, basi fahamu kwamba Nabii huyo au Mtume huyo ni wa uongo
Sidhani kwamba Wakristo wanaposherehekea kuzaliwa kwa Yesu tarehe 25 Dec, wanamaanisha kuwa Yesu alizaliwa tarehe hiyo. No. Hiyo ni siku iliyochaguliwa tu kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu. Kwamba Yesu alizaliwa July au Aprili hiyo sio issue. Jambo muhimu ni kwamba alizaliwa kwa ajili ya wanadamu. Hicho ndicho kinachowafanya washerehekee.
 
Haya umeusomaaa kumbe umeelewa umeambiwa alikuwa anakwendaa"" then anafanya nini??? Jibu ni "ANAFUNDISHA" kuhusu habar za ufalme wa Mungu kumbe ushaona mwenyew kuwa the first priority ya mission yake ilikuwa kuwafundishaa kuwapa maarifa ya neno, kwanzaa na ndipo mambo ya uponyaji yalifuata hiyo ni kuonesha kuwa chamsingi na chamuhimu ni wew kuijuwa kwel na kupata hakika ya kuuona ufalme wa Mbingu kabla hata ya uponyaji...bado ukwel unabak pale pale kuwa kristo hakuja kukutibu ww bali alkuja kukupa mwanga wa kupata ujue utajitibujeee na sio kuwa tegemezi kwa mtu bal kwa Mungu pekee....Nashukuru umeleta neno limekufunza mwenyew[emoji41][emoji41]
 
Mkuu kuna watu hawajawahi kutenda dhambi Ila ni wagonjwa taabani,by the way nimeupenda mwandiko wako,hongera!.
Shida sio wameponywaa,,shida ni wametumia njia ipi kuponaa upo apo?? Kumbuka hata mizimu ina huruma sana kwa wanadamu nayo inanguvu za kuponya ma kufanya miujiza,,uruma yako uliyofanyiwa isiwe kigezo cha kumtunuku aliekuponya kuwa ni mtakatifu,,,HAIPO HIYO
 
Zile ni drama tu wale wachawi wakubwa,,,wamuombe Mungu awaponeshe korona waache uwiz
 
Sawa kaka, si unaona mzungu anatii masharti .Ukiweza kutii masharti yasiyo ya giza wewe ni mtu wa Mungu na utabarikiwa na kuwa na maisha marefu.Mfano huku kwetu tunaambiwa don't drink and drive wenzetu wanatii sisi huku mtu hajali hata kidogo.tena akijua askari hamfuatiii ndio kabisaaa.Wenzetu wanatii hivyo vifo vitokanavyo na kuendesha gari amelewa ni kidogo .Mfano uliotoa.ni wa ngono zembe nk .
 
Biblia huwa unaisoma mara moja kwa mwaka? Kuhubiri/kufundisha na uponyaji vyote ni muhimu. Mtu kiziwi(asiyesikia kabisa) utamfundisha kwanza ndio umuombee apone? Yesu aliposema fufueni wafu, hao wafu watafundishwa kwanza ndio wafufuliwe?
 
Sipingi umuhimu wa mtu kuhubiriwa au kufundishwa kwanza then ndio mtu aombewe au ajiombee mwenyewe. Soma mistari ifuatayo kwa makini utaona wazi uponyaji unatangulia kabla ya mafundisho.
Yohana 5:1-8
[1]Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu.
[2]Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano.
[3]Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke.
[4]Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.]
[5]Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane.
[6]Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
[7]Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.
[8]Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.

Marko 10:46-52
46 Wakafika Yeriko. Na Yesu alipokuwa akiondoka pamoja na Wanafunzi wake na umati wa watu, kipofu mmoja, jina lake Barti mayo, mwana wa Timayo, alikuwa ameketi kando kando ya njia, akiomba.
47 Aliposikia kuwa Yesu wa Nazareti alikuwa akipita, akaanza kupiga kelele, “Yesu, Mwana wa Daudi, nionee huruma!”
48 Watu wengi wakamkemea, wakamwambia akae kimya. Lakini yeye alipiga kelele zaidi, “Mwana wa Daudi, nionee huruma!”
49 Yesu akasimama akawaambia, “Mwiteni.” Wakamwita wakamwambia, “Changamka! Usimame, anakuita.”
50 Akatupa vazi lake kando, akaruka juu, akamwendea Yesu. 51 Yesu akamwuliza, “Unataka nikufanyie nini?” Yule kipofu akajibu, “Mwalimu, nataka kuona tena.” 52 Yesu akamwambia, “Nenda, imani yako imekuponya.” Wakati huo huo akaweza kuona, akamfuata Yesu njiani.

Yakobo 5:14
Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana

Umeonaa? Mtu kama anaumwa, awaite wazee wamuombee. Sio wamfundishe kwanza!
 
Waafrika wacheni ujinga jamani, T.B. Joshua si nabii wala nini he never cures anyone, yeye analipa watu ku act tu na kuaminisha watu wasiojitambua kuwa ana power za kutibu watu kumbe ni kamba tu.
 
Yale ni maigizo watu wanaandaliwa, niamboa Mtanzania Kilema alie wahi kwenda kwa TB joshua akaombewa akapona.

Au ndugu yako, jirani alie wahi ombewa na akapona
 
Wale wanao waombea huwa hawasisitizi hapo kwenye kuacha Zambi,
 
Cha ajabu wao wakiumwa wanaebda kutibiwa First class Hospital, Hawa wahubiri ni wasanii sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…