Kwani hakuna wanao pona Hospitali na baadae wanaugua tena? Kwa hio kwa akili yako kila ukiumwa basi unetenda dhambi?Na wengi wamekuwa wakipuuzia hili,halafu magonjwa yanapowarudia wanaanza kusema mchungaji flani ni fake kwakuwa bado hajapona,wakati ameshasahau alishapona na akatoa na shukrani.Kizuri ni kuwa TB Joshua ukienda kwake kabla ya maombezi huwa anawatahadharisha mapema hili kabla ya maombezi...
Ni kweli!! niliposoma kichwa cha habari na yaliyoandikwa ni tofauti!!Mkuu mediaman nakusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nimependa hoja ulizozitoa ILA natatizika kidogo na jinsi kichwa cha habari kilivyokaa; kinaweza kupeleka ujumbe ambao sio.
Ahsante
Sio kila ukiumwa. Ni hivi: kama umekuwa ukitenda dhambi, ukaugua, baadaye ukapona kwa muujiza(baada ya kuombewa), ili usipatwe tena na ugonjwa huo kwa viwango vya juu au kupatwa na jambo baya zaidi, zingatia vigezo/masharti aliyotoa Yesu: USITENDE DHAMBI TENAKwa hio kwa akili yako kila ukiumwa basi unetenda dhambi?
Kichwa cha habari kina mislead.meseji yako nzuri.Kwa neema ya Mungu tumeiona tena siku ya leo tukiwa na uzima na nguvu ya kuingia katika jukwaa letu pendwa (JF), ili kupashana habari, kutiana moyo na kushauriana. Wakati sisi tunafurahia mada mbalimbali zinazoletwa humu, tusisahau kuna ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu wana huzuni kubwa kwakuwa wamelazwa hospitalini muda mrefu kutokana na magonjwa sugu au "yasiyosikia dawa" kama vile kansa, ukimwi, kisukari, magonjwa ya moyo, nk. Ni jukumu letu kutafuta namna ya kuwasaidia.
Watu wanaougua muda mrefu hupewa ushauri mwingi sana wa jinsi ya kujinasua kutoka katika magonjwa sugu. Wagonjwa wa aina hiyo mara nyingine hushauriwa waende kwa wahubiri, wachungaji, manabii au mitume wakaombewe. Huaminishwa kuwa wengi katika wale wanaoombewa hupokea uponyaji kwa njia ya muujiza tena bila kulipa gharama yoyote.
T.B. Joshua anafahamika sana ulimwenguni kutokana na maombezi anayoyafanya katika kanisa lake kubwa, lililoko Nigeria. Kwa wanaofuatilia habari za mhubiri huyo, ni wazi watakuwa ama wamesikia au kuona vipofu, viwete, viziwi na wenye magonjwa sugu wakitoa shuhuda za uponyaji baada ya kuombewa na T.B. Joshua. Sio mhubiri huyo tu anayeombea wagonjwa, wapo wahubiri wengine Kenya, South Africa, Korea ya Kusini, USA nk wanaoombea watu wenye magonjwa mbalimbali. Kuna mhubiri fulani, Tanzania, yeye sio tu anaombea wagonjwa, amewahi kuonekana pia akiombea mtu aliyekufa, kisha mtu huyo akafufuka!
Hao wote wanafuata nyayo za Yesu. Siku moja Yesu alipokuwa duniani alimponya mtu aliyekuwa mgonjwa sana kwa miaka 38. Alikuwa hawezi kuinuka kutoka kwenye godoro lake. Yesu alimponya kwa kumwambia tu, "inuka, umekuwa mzima, jitwike godoro lako uende." Akainuka, akaenda zake, mzima kabisa! Baadaye Yesu alimkuta huyo mtu hekaluni akamwambia: "Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi."(Yohana 5:14).
Je, una ndugu, jamaa au rafiki anayeteseka na magonjwa mabaya? Ametibiwa hospitali miaka mingi lakini imeshindikana? Sio vibaya ukimshauri aende akaombewe. Akikubali ushauri wako, akaamua kwenda kuombewa mahali popote - kwa T.B. Joshua au kwa mhubirii yeyote maarufu, mwambie akiombewa, akapona, ajihadhari sana asitende dhambi tena. Mtu akitenda dhambi baada ya kupona kwa muujiza, kuna uwezekano wa kurudiwa na ugonjwa uleule kwa viwango vya juu zaidi au kupatwa na jambo baya zaidi. Nawatakia watu wote maisha ya heri.
Hahaa. Sina ushirika na mwovu shetani. Nampinga kwa Jina la Yesu kila anaponijia.Mleta mada nakuapia wewe ni uzao wa yule mwovu tena kwa 100%.
If you just read the title, you will surely be misled.Kichwa cha habari kina mislead.meseji yako nzuri.
Unaenda nje ya mada: ukiombewa(na mhubiri au mtu yeyote yule), ukapona, usitende dhambi tena.Waafrika wacheni ujinga jamani, T.B. Joshua si nabii wala nini he never cures anyone, yeye analipa watu ku act tu na kuaminisha watu wasiojitambua kuwa ana power za kutibu watu kumbe ni kamba tu.
nakuunga mkono mkuu. watu wamweka imani kwa wenzaoWatu watafute maarifa wenyewe binafsi kwa sababu hata hawa watumishi ni binaadam kama wewe, kama dhambi wanatenda kama wengine, hivyo kwanini uombewe na mtenda dhambi mwenzio, tafuta maarifa ya kuacha dhambi wenyewe. Na mzigo wa dhambi ni mzigo ambao ukiubeba huwezi jua kama ni mzigo utatembea nao miaka nenda rudi, mpaka ugundue utakua umeshamaliza waganga wote kwa ajili ya kukuagua.
Unataka kusema sticks ipeperuke kutoka Lagos Nigeria kwa upepo hadi Tanzania bila gharama.Tb Joshua is an Agent of the devil [emoji48].Nakushangaa uliekuja hapa kupigia kampeni jitu jizi na tapeli km Tb Joshua. Kwanza mahubiri yake yamejaa udhalilishaji akionyesha "live" wanawake wakijifungua baada ya kupokea maombi,na anatumia matukio haya( ArrangedMiracles) km chambo ya kuwavuta watu wengi wenye dhiki mbalimbali,hasa ukizingatia ulimwengu wa sasa watu wana dhidi na shida za kila aina.
Lakini pia hata imani yake ni ya kutia shaka.Mara awafundishe watu kufanya maombi kutumia shanga,maji na stika yenye picha yake.Je ndo maandiko yameagiza ivo? Je hayo ndio mafundisho ya WOKOVU? Wizi mtupu!!
Kibaya zaidi anaviuza hivo vitu km bidhaa,japo amekuwa akidanganya kupitia TV yake kuwa anagawa bure. Muongo! Hakuna kitu anachotoa bure hata kimoja! "You will have to pay for either direct or indirectly".Wajinga wengi wasiojua kutafakari maandiko wameamini na kuishia kupigwa pesa nyingi.
Tb Joshua anatumia uchawi na ujanja ujanja katika kuwateka watu. Nakushauri acha kupoteza muda na manabii wajanja wajanja km Prophet Bushiri,TB Joshua,Mwamposa,Gwajima, Suguye na wengineo utapoteza mda na pesa zako bureee.
AmenMtu akienda kuombewa akaambiwa atoe kwanza pesa ndio aombewe, asikubali. Yesu hakuwalipisha pesa wagonjwa. Hata wanafunzi wake alipowapa mamlaka ya kupoza wagonjwa, aliwaambia amewapa mamlaka hayo bure hivyo watoe huduma hiyo bure. Sadaka tu ndio mtu anaweza kutoa, tena kwa hiari na moyo mkunjufu, sio kwa kulazimishwa.
Naona hatuelewana unajarbu kwa nguvu zote kuhalalisha miujiza na uponyajiii..ukwel utabak kuwa zama hiz hakuna nabii,mtume wala nn awo wote ni majizi tu hata watumie biblia ganiSipingi umuhimu wa mtu kuhubiriwa au kufundishwa kwanza then ndio mtu aombewe au ajiombee mwenyewe. Soma mistari ifuatayo kwa makini utaona wazi uponyaji unatangulia kabla ya mafundisho.
Yohana 5:1-8
[1]Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu.
[2]Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano.
[3]Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke.
[4]Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.]
[5]Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane.
[6]Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
[7]Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.
[8]Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.
Marko 10:46-52
46 Wakafika Yeriko. Na Yesu alipokuwa akiondoka pamoja na Wanafunzi wake na umati wa watu, kipofu mmoja, jina lake Barti mayo, mwana wa Timayo, alikuwa ameketi kando kando ya njia, akiomba.
47 Aliposikia kuwa Yesu wa Nazareti alikuwa akipita, akaanza kupiga kelele, “Yesu, Mwana wa Daudi, nionee huruma!”
48 Watu wengi wakamkemea, wakamwambia akae kimya. Lakini yeye alipiga kelele zaidi, “Mwana wa Daudi, nionee huruma!”
49 Yesu akasimama akawaambia, “Mwiteni.” Wakamwita wakamwambia, “Changamka! Usimame, anakuita.”
50 Akatupa vazi lake kando, akaruka juu, akamwendea Yesu. 51 Yesu akamwuliza, “Unataka nikufanyie nini?” Yule kipofu akajibu, “Mwalimu, nataka kuona tena.” 52 Yesu akamwambia, “Nenda, imani yako imekuponya.” Wakati huo huo akaweza kuona, akamfuata Yesu njiani.
Yakobo 5:14
Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana
Umeonaa? Mtu kama anaumwa, awaite wazee wamuombee. Sio wamfundishe kwanza!
Bible reference yann huoni kuwa babu zako waliomba mvua ikanyesha,mpka sahv watu wanakesha kwa vikinge na wanapona tena miujiza ya nguv kulko ya awo wajiitao wachungajBible reference, please
Ndio tatizo la matapel mnakalilisha uongo tu..ni hiv biblia naijuwa zaid ya wachungaji zakoBiblia huwa unaisoma mara moja kwa mwaka? Kuhubiri/kufundisha na uponyaji vyote ni muhimu. Mtu kiziwi(asiyesikia kabisa) utamfundisha kwanza ndio umuombee apone? Yesu aliposema fufueni wafu, hao wafu watafundishwa kwanza ndio wafufuliwe?
Hakuna mtu hata mmoja ambaye hajawahi kutenda dhambi katika karne hii.Mkuu kuna watu hawajawahi kutenda dhambi Ila ni wagonjwa taabani,by the way nimeupenda mwandiko wako,hongera!.
Sasa swali langu linabakia pale pale, hao wanaojiita Manabii na wao hawaujui UKWELI ikiwa wanaye ROHO MTAKATIFU?Sidhani kwamba Wakristo wanaposherehekea kuzaliwa kwa Yesu tarehe 25 Dec, wanamaanisha kuwa Yesu alizaliwa tarehe hiyo. No. Hiyo ni siku iliyochaguliwa tu kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu. Kwamba Yesu alizaliwa July au Aprili hiyo sio issue. Jambo muhimu ni kwamba alizaliwa kwa ajili ya wanadamu. Hicho ndicho kinachowafanya washerehekee.