Ukienda kwa shehe akikupa vikaratasi kama hivi uwe unavibeba ama kuviweka chumbani vichane na usirudi tena kwake, ni uchawi mtupu

Ukienda kwa shehe akikupa vikaratasi kama hivi uwe unavibeba ama kuviweka chumbani vichane na usirudi tena kwake, ni uchawi mtupu

Mbona mwamposa anatoa mafuta hamsemi uchawi ila wa dini ya mnyaazi wakitoa karatasi tu mnasema uchawi.

Kwani dini ya mnyaazi si inahusika na majini na mambo kama hayo si ndo uchawi wenyewe
 
Dah sasa ndo nathibitisha zaidi kua ww unaelekea kukufuru kabisaa

Hlf ety since 1991 unasoma dini , ivi unasoma dini gni ww usoijua hta iyo hadithi


Maghurafi mna tabu sanaaa
We Hadith unazijua!?..unajua historia yake!?..unajua ummar bin ul khattab alifanya na kusema nini kuhusu Hadith!?..unamjua khalifa mwingine aliyelaani Hadith!?..nimepita kote huko uliko na kwingineko kuhusu dini,bado una safari ndefu ya elimu ya dini ikiwa kweli unaitafuta
 
We Hadith unazijua!?..unajua historia yake!?..unajua ummar bin ul khattab alifanya na kusema nini kuhusu Hadith!?..unamjua khalifa mwingine aliyelaani Hadith!?..nimepita kote huko uliko na kwingineko kuhusu dini,bado una safari ndefu ya elimu ya dini ikiwa kweli unaitafuta
Naomba nisikujibu tena kwa hatua ulofikia inaonekana una matatizo ya Afya ya Akili sio bure wewe
 
Leo wachungaji wa mchongo kina Mwamposa na mafuta yao tuwapumzishe kidogo tuangalie upande mwengine


336923133_932706677932030_4425398350988145523_n.jpg


343930075_194729550027513_5680366304643186106_n.jpg


View attachment 2603934

Nimekuwa katika magroup ya tiba naona kuna hivi vikaratasi watu wanapewa ama kuelekezwa kuvichora na wa kuitwa mashehe wakiwaambia ni tiba, ulinzi, kuongeza, mvuto, n.k. niwarahishie tu kwamba huu ni UCHAWI!!

Kama ni ya matibabu ya kiroho kama kurogwa, hakuna anaeweza kutibu zaidi ya Allah bega jwa bega na dua, vifungu, rukya .

Kama ni kwa kujilinda, maandishi au michoro haiwezi kukulinda, Ni imani yako kwa Allah ndiyo inayokulinda pamoja nawe kupiga dua, kunukuu vifungu vyake.

Maneno ya korani hayapo kwajili ya kuchanganywa na michoro ama maneno mengine kwenye kijikaratasi, huo ni ushirikina wa kumshirikisha Allah na vitu vya ajabu ajabu, Allah hawezi kusaidiai hapa bali hayo maneno ya quran yanazuga tu ili ile michoro mingine au maneno ndio vitumike, hayo maneno hata ukimpa muarabu ni ngumu sana kuyatambua, ni lugha za kishetani

Ukipewa hivi vitu pindi unapotoka tu njiani chana chana kabisa tupa kule visiiingie nyumbani kwako na kama ulibebea mfukoni hio nguo choma kabisa
Nami kidogo nitoe nijuacho....

Hilo talasimu la kwanza limeandikwa nini ?!!!

Jibu.....

Yamerudiwa manenoneno "Allah... Allah...Allah....na aya za Quran zilizotajwa Allah....hiki si kitu kibaya....

Talasimu la pili.....

Hapa kidogo kuna muhali....

1)Wako waislamu wengi(wajuzi wa elimu) wasiokubali haya...wana sababu zao na si za kupuuzwa.....

2)Wako waislam wengi(wajuzi wa elimu) wanaokubali haya....wana sababu zao na si za kupuuzwa pia...

1)Kundi la kwanza.....

Hawa walitokea miaka mingi iliyopita wakifuata elimu ya Ashaikhul Kiraam Ashaikhul muadhama Al Allama ibn Taymiyyah na wanafunzi wake waliokuja kuwa masheikh wakubwa(Allama)...Akina Ibn Quddama Al Maqdisi,Ibun Qayyim Al Jawzii,...hawa ni wafuasi wa madhehebu ya HANBALI ukimtoa Al Allama Ibun Kathir(madhehebu ya Shafi) japo pia anafuata baadhi ya itikadi za HANBALI.....

Ibun Taymiyyah alikataa uzushi wote na aliwapinga wanazuoni wa Kalam na "reasons"....hakutaka utumie "reasoning" katika ufafanuzi wa sifa za Mungu(majina ya Allah) kama "Rahman ,Karim ,Latwifu,Rahiim ,Shakur"...aliamini sifa zake ni hizo...zipo...hazihitaji tafakuri nyingine...mathalani kurudia idadi za jina fulani hukupa kitu fulani...hili alilipinga kwa fikra na ufafanuzi wake wa kuzama katika bahari ya elimu ya dini.....
Alipinga sifa za mtume S.A.W kuzifanyia sherehe mathalani Maulid,alipinga kuzuru makaburi,alipinga kukusanya watu kuwakukumbuka waliokufa kwa kufanya maombi(haya maarobaini)...alipinga dhikri za masufi mathalani kuzama sana katika "mysticism" mfano wa dhikri zirudiwazo mpaka watu kucheza ama "kudansi" akiziita ni "ulevi-intoxications"....

Kundi la pili.....

Hawa ni wale wanazuoni wenye kutanguliza sifa za Mungu(majina ya Allah)...Allah's attributes mathalani "Jabbar" kuwa ukirudiarudia jina hilo kwa idadi fulani basi huweza kukupa mathalani ujasiri ama nguvu fulani kama lilivyo jina lenyewe....humu wengi ni masufi wenye kufuata madhehebu ya HANBALI+SHAFII+MALIKI...masufi ni watu wanaoamini sana katika DHIKRI(maombi ,utajo wa Allah) kwa kurudiarudia...huweka vigenge kwa pamoja wakazitaja sana sifa za Allah(majina yake) na sifa za mtume SAW...kwa MASHAIRI(ode) ,kwa kughani ,kwa kujitingishatingisha....wako wanaoingiza mpaka katika "miziki-nasheed" na wako wanaokataa hayo....wako wanaofanya maombi(dhikri) wakazama katika "meditations" kama wale mabuddha na wale wanaofanya YOGA wakafikia stage ya ulevi kwa kuzama huko(ectasy) na wako wanaokataa uzamaji huo(ectasy)...kifupi ndani ya kila kundi huwa HAWAKUBALIANI NA KILA JAMBO...na hii iko madhehebu yote na itikadi zote za kiislam(si Shafi ,Si Hanbali ,Si Maliki ,Si Hanafi)...si Maturidi ,Si Salafi....si Shia.....kifupi kila Kundi Lina vikundi vidogovidogo ndani yake....

Isisahaulike kuwa hawa MASUFI wengi wao wanaamini pia katika KUZURU MAKABURI,kufanya dua katika makaburi ya WATAKATIFU(SAINTS),masharifu,wanazuoni wakubwa....wako wanaofika mbali na kuwaomba waliolala humo makaburini na wako wasiowaomba bali hufanya kitu kiitwacho "Wasila- kupitia hao"...hapa ndipo penye tofauti kubwa na masalafi(hawa wanapinga kabisa kuwaomba ,ama "wasila-kupitia" kwa hao niliowataja hapo juu....

Ikumbukwe hao MASUFI pia wanaamini katika kufanya maombi kuwaombea waliokwishakufa(hitima ,arobaini n.k) wakiwa na misimamo ya aya ya Quran isemayo "....Allahumma rabbana ighfirlana wal ikhwanina lladhina Sabaquna bil iiiman-Mola wetu tusamehe madhambi yetu na ndugu zetu waliopita katika iiiman"....kwa upande wa MASALAFI wao hawakatai hiyo aya bali wanasema kuwa MTUME SAW hakuwakusanya watu kusoma HIVYO VISOMO VYA KUWAREHEMU WALIOPITA na pia kupika vyakula(ubwabwa,pilau ,biriani mihogo ya nazi ndondo,uji na mafenesi)....masalafi nao wanapinga mikusanyiko ya kumkumbuka mtume SAW(Mazazi yake-birthdays-Maulid).....

[emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115]
Nimefafanua hivi kabla sijaendelea zaidi......

#YetzerHatov
#DoNotDoHarm
 
Muendelezo........

Kuhusu hilo TALASIMU la pili.....

Humo ndani iko elimu ya "unajimu" ya wasomi wakubwa wa unajimu na mahesabu....mathalani MASLAMA AL MAJRITI...huyu alitokea Andalusia(mwarabu ama mbeber wa Spain)....ndiye pia mgu duzi wa MERCURY 2 OXIDE....ndiye aliyerekebisha majedwali ya Msomi mkubwa wa Iraq Muhammad Mussa Al Khwarizim(mgunduzi wa mahesabu ya ALGEBRA....nitakuja kumzungumzia siku nyingine....

MASLAMA AL MAJRITI huyu alikuwa ni sufi na aliandika kitabu cha meditations za ndani za usufi ,unajimu ,matibabu na ulinzi kiitwacho PICATRIX( hiki kimefanyiwa tarjumi na nchi za ulaya na wako wanaosema pia kina elimu tata(yaani uchawi wa nembo na mahesabu)....

Yuko msomi mwingine ambaye SALAFI hawataki hata kumsikia[emoji1787][emoji1787][emoji1787]aitwaye AHMAD AL BUNI...huyu aliandika kitabu kiitwacho SHAMSIL MA'ARIF(knowledge of gnosis)...ufahamu wa wenye akili(kuitwa mwenye akili si jambo dogo jamani...haswa katika ulimwengu wa mafilosofia......hata peponi watakwenda tu wenye akili na si mazamwamwa na mahobobo [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Huyu bwana Al Buni naye ni mmoja wa kuamini sana MAHUSIANO ya mwanadamu na hesabu....zikiwemo pembe na "angle"....kwake amekwenda mbali zaidi kwa kuyatafsiri majina kwa sifa za nje na za ndani(kwenye hizo sifa za ndani ndio wengi wetu hatukubaliani) ila ELIMU NI BAHARI....Mwenye kuimiliki YOTE ni ALLAH PEKEE...si malaika wala si manabii bali huwakadiria wanaadamu vile ATAKAVYO kwa hiyo usijifanye wewe UNAJUA KILA KITU...hapana....haya ni makosa.....na si elimu yote aliyokufundisha SHEIKH ,ASKOFU ,MCHUNGAJI,MGANGA,MWALIMU wako ndio mwanzo na mwisho wa elimu....hapana haya ni makosa ni si kitu bora kwa mwanadamu mwenye kudai kumpenda MWENYEZI MUNGU ukweli wa kumpenda [emoji1787][emoji1787]

Hayo MAJEDWALI ,miraba ,mistatili na "angles" ni moja ya elimu za huyo bwana msomi Al Buni ambaye wako waislam wasioona hayo kwa mtume Muhammad SAW huitakidi kuwa ni "mauchawi" tu....

Tukirudi katika lile talasimu la pili hapo juu...

Humo ndani Kuna jina la Mwenyezi Mungu "Allah"...

Humo ndani kuna elimu za unajimu za siku na nembo zake mathalani huo MNYOTA(nembo ya Jua-siku ya jumapili)... Kuna minembo ya siku ya jumatatu mpaka jumamosi)....hawa wanajimu wanapochora minembo yao huamini kuwa maisha ya UNIVERSE(ulimwengu) amepewa mwanadamu...na kila kimzungukacho kinamuathiri POSITIVELY ama NEGATIVELY mathalani bila JUA hakuna maisha.....bila MWEZI(siku ya jumatatu kwao) hakuna maisha(CLIMATE CHANGES ,KUPWA NA KUJAA KWA MAJI) ,bila sayari zilizomo katika universe mathalani (Venus ,Mercury) basi mpango wa universe haujakamilika....huamini kuwa madini yaliyopo ndani ya mwanadamu pia yako ardhini na pia hizo sayari nyingine.....huamini kuwa bila ya MAISHA ya mwanadamu basi SHETANI asingeumbwa....huenda mbali kwa kuamini pia malaika pamoja wameumbwa kuwa wafanyakazi wa Allah pia VAZI la ukamilifu wao na kuwepo mwanadamu mathalani...

Malaika wanaoleta mvua duniani....mvua ni kwa viumbe wote ila mwanadamu ni zaidi(mkubwa wao)....

Malaika wanaongamiza(kama kule kwa nabii Lutu ,nabii Nuhu)...hawakuletwa isipokuwa ni kwa wanaadamu....

Malaika wanaosimamia PEPO (haikuumbwa isipokuwa ni kwa ajili ya wanaadamu na majini ambao watamkataa jini mwenzao IBILISI na kazi zake)....

Malaika wanaosimamia MOTO(haukuumbwa isipokuwa ni kwa ajili ya watoto wa Adam+Eva watakaokaidi maelekezo ya Mungu Mwenyezi na wale majini watakaomfuata IBILISI)....

Kifupi hawa wanajimu wanaamini MWANADAMU ndio kiumbe Bora na mtukufu zaidi kushinda malaika+majini pale tu asipokaidi maelekezo ya Mwenyezi Mungu(ikiwepo kuitawala dunia ,anga na vilivyomo ndani yake) kwa kutumia AKILI NA VIPAWA ALIVYOJAALIWA...niliingia kwenye majadiliano ya kupingana na mmoja wao akaniambia nimueleze maana ya hii aya ya biblia takatifu " watu wangu huangamia kwa kukosa maarifa....na zile aya za Quran(je hamna akili ,je hamtafakari n.k).

Kwa hiyo hilo litalasimu la pili lina pembe....

Ziwe 3
Ziwe 5

Hizi humaanisha MWENYEZI MUNGU ,BINADAMU ,ULIMWENGU NA VILIVYOMO NDANI YAKE...

Mathalani ile NYOTA YA mfalme nabii DAUDI....
Nyota ya mfalme nabii SULEIMAN...

Hata wayahudi wanatumia kama ishara ya MWENYEZI MUNGU+WAO+NCHI YAO YA AHADI (pembe tatu mbili-iliyojuu na iliyo chini)...mistari ile ya ramani yao ni kuanzia mto SHAMU mpaka mto EUPHRATES Iraq kuwa ndio ardhi waliyokabidhiwa na YHWH(Muumba Mbingu na nchi)......

Asanteni wapendwa mbarikiwe sana ,aaaamin aaaamin[emoji120]

Wallahu A'alam [emoji120]

#YetzerHatov
#DoNotDoHarm
 
Sio yeye tu alisema sisi wote ni miungu kasome Yohana 10:34 -36

Yohana 10:34
Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?

Yohana 10:34
Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?

Yohana 10:35
Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka);

Yohana 10:34
Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?

Yohana 10:35
Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka);

Yohana 10:36
je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?
 
Yan wewe kweli mpumbavu na hyo sunni yako washamba wa tupu....
Allah anasema magonjwa yote yanatoka kwake na tiba zinatoka kwenye kitabu chake...
Sasa kw taarfa yako,hiyo tarasimu ya kwanza hapo juu..manuizo yake ni kusomea BARAHATIHI 11...Halafu unaleta aya nusu unadhn cc wajnga?
Mmhhhhhhhh!!!!!![emoji25]
 
Hiyo ni talasimu ni aina fulani ya kinga naweza kusema ni kama jini hiyo watu wengi wanatembea nayo unakuta wameweka kwenye waleti ni ishu ndogo sana ila sheria yake ni moja usije kushika talasimu lililonuiwa kwa ajili ya mtu kama halikuhusu achana nalo especially kwa wanawake wanaopenda ku sachi wanaume
Mmmhhhhhhhg!!![emoji849]
 
Hiyo ni talasimu ni aina fulani ya kinga naweza kusema ni kama jini hiyo watu wengi wanatembea nayo unakuta wameweka kwenye waleti ni ishu ndogo sana ila sheria yake ni moja usije kushika talasimu lililonuiwa kwa ajili ya mtu kama halikuhusu achana nalo especially kwa wanawake wanaopenda ku sachi wanaume
Duh!
 
We Hadith unazijua!?..unajua historia yake!?..unajua ummar bin ul khattab alifanya na kusema nini kuhusu Hadith!?..unamjua khalifa mwingine aliyelaani Hadith!?..nimepita kote huko uliko na kwingineko kuhusu dini,bado una safari ndefu ya elimu ya dini ikiwa kweli unaitafuta
Mi naomba unijuze hapo kwenye alichokisema Omar bin Khatwaab kuhusu hadith na pia huyo khalifa aliyezilaani hadith.

Naomba kujua tafadhali
 
Uchawi si ushirikina,ni uelewa mbaya tu juu ya shirki,malaika walifundisha uchawi hawakufundisha shirki,wanaoitwa washirikina kwenye Quran walikua wakiabudu sanamu,acha kujitia una elimu Sana na umeongoka na usalafi wako mnaogeuza wanazuoni kuwa miungu kwa kufuata fatwa zao badala ya Quran
unaweza kufafanua tofauti ya uchawi na ushirikina? tupate maarifa zaidi
 
Leo wachungaji wa mchongo kina Mwamposa na mafuta yao tuwapumzishe kidogo tuangalie upande mwengine.

336923133_932706677932030_4425398350988145523_n.jpg
343930075_194729550027513_5680366304643186106_n.jpg
View attachment 2603934

Nimekuwa katika magroup ya tiba naona kuna hivi vikaratasi watu wanapewa ama kuelekezwa kuvichora na wa kuitwa mashehe wakiwaambia ni tiba, ulinzi, kuongeza, mvuto, n.k. niwarahishie tu kwamba huu ni UCHAWI!!

Kama ni ya matibabu ya kiroho kama kurogwa, hakuna anaeweza kutibu zaidi ya Allah bega jwa bega na dua, vifungu, rukya.

Kama ni kwa kujilinda, maandishi au michoro haiwezi kukulinda, Ni imani yako kwa Allah ndiyo inayokulinda pamoja nawe kupiga dua, kunukuu vifungu vyake.

Maneno ya korani hayapo kwajili ya kuchanganywa na michoro ama maneno mengine kwenye kijikaratasi, huo ni ushirikina wa kumshirikisha Allah na vitu vya ajabu ajabu, Allah hawezi kusaidiai hapa bali hayo maneno ya quran yanazuga tu ili ile michoro mingine au maneno ndio vitumike, hayo maneno hata ukimpa muarabu ni ngumu sana kuyatambua, ni lugha za kishetani.

Ukipewa hivi vitu pindi unapotoka tu njiani chana chana kabisa tupa kule visiiingie nyumbani kwako na kama ulibebea mfukoni hio nguo choma kabisa.
Habari mkuu naimani ni Mzima wa Afya.....
Nilitamani sana nikujibu kwa misingi ya akili lakini kwa kuwa tu umeweka mada hii kwa habari na hoja mchanganyiko itoshe tu na mimi pia nikujibu kwa misingi ya habari na hoja mchanganyiko...

Kwa kuanza nakuomba uniwie radhi kwa kukuita wewe ni Mpumbavu namba 20, Nilisema kila mpumbavu nitakae kutananae anaongea vitu asivyovijua basi nitampa cheo chake cha upumbavu yeye ni Mpumbavu namba ngapi hivyo chukua hiyo yako ni Namba 20...

Kwa kufikia hapo tu najua vidole sasa hivi vitakuwa vinakutukutia uanze kuporomosha matusi lakini usihofu mpumbavu sio tusi ni pale tu mtu anapoteleza kwenye ujuzi....

Hizo ulizoweka hapo picha na kuorodhesha kisha na kusema kwa majigambo kuwa ni Uchawi. Wanaozijua ni wenye kuita talasimu yaani talisman ambayo hutegemea na muhusika anaitizama vipi na katengeneza kwa misingi ipi...

Ikiwa wewe sio mwenye asili ya persian kujua hizi ni nini kwako inaweza kuwa shida hata kwa waarabu na waislamu wenyewe.
Kwa maana talasimu inaweza kuwa kwa mtu yoyote na hali yoyote ile unaweza kuigeuza ikawa ya kizungu,kiarabu,kihindi,kichina,kijapani,kifaransa,kuswahili hata kisukuma au kijaluo.

mradi ulichoandika hapo kiwe kina maana ambayo wewe unayoitaka iwe hiyo mathalani moja ya talasimu yoyote hapo iliyoandikwa jina Allah ukiamua kuandika Shetani inaenda tu kwa shetani kama wewe ni Mwenye kuabudu shetani

Kama ilivyo kwa madai yako kwamba hakuna anaeweza kutibu pasipo mwenyezi Mungu basi pia hakuna anaeweza kudhuru pasipo idhini ya mwenyezi Mungu...

Kuna member hapo kakwambia wewe hujui mengi bado ni kweli hujui mengi.

Mwenyezi Mungu akuepushe kuwa mmoja kati ya wanafiki kwa maana kama wewe ni msafi majukwaa ya uganga uchawi mashehe wa michongo, wachungaji waongo ulienda kutafuta nini kama sio unafiki?

Vile vile kama wao wanakosea ulitakiwa uwaambie kule kule kuliko kuja kusambaza unafiki wako huku. Kama wewe ni Mkristo basi umekosea hata kama ni mwislam basi umekosea pia kwa maana anaekosea hurekebishwa pale pale....

Unafiki mwingine ni wewe kusema kwamba Mungu anatosha kuwa tiba maana yake wachawi wako baada ya kujaribu kukutibu wakashindwa ukamrudia Mwenyezi Mungu which ni jambo zuri...

Ila shida umemrudia kinafiki kwa maana unatafuta hapa jukwaani support ya watu wakusupport kuwa kuacha uchawi ni Jambo zuri... Of cause ni jambo zuri hakuna anaekataa lakini kama wewe umeongoka basi kawaongoe na wenzio sio kuja kuwateta huku....

Pia unasema ushahidi wa maneno ya Quran kuzuga hapo bado hatujaona hapo ni wapi kwenye hizo tarasimu ulizopost kuna aya za Quran za kuzugia?

Hizo namba za kiarabu na hizo boksi boksi ndio unaita Quran? au kuona tu hilo jina la mwenyezi Mungu? Jina la mwenyezi Mungu anatumia mtu yoyote hata wanafiki kama wewe, Kujificha maovu yao.

hayo maneno hata ukimpa muarabu ni ngumu sana kuyatambua, ni lugha za kishetani.

Usiseme kitu usichokijua hii lugha ni ya kiarabu lakini sio kiarabu unachojua wewe, lugha ya talasimu kwa pamoja na lugha zingine zote mazao yake ni Babilon ambapo kila mtu pale alitoka na lugha yake jifunze historia.

  • Kwa hiyo watoto shule wanaofundishwa maumbo ya hesabu wanafundishwa maumbo ya ushetani?
  • Kwa hiyo jina hilo katikati hapo la Allah ni jina la kishetani?
  • Kwa hiyo hizo pembe tano hapo ni mchoro wa kishetani?
  • Kwa hiyo malaika Gabriel,Michael,Rafael na Izrael hapo ni wa shetani?
  • Kwa hiyo kuandika قوله الحق و الله الملك ni ushetani yaani Neno lake ni kweli, na Mungu ndiye Mfalme?
  • Kwa hiyo ٱلْفَتَّاحُ yaani Mfunguzi AMBAYE anafungua aina zote za vitu vilivyofungwa ni shetani?
Mbona kama kadri siku zinavyozidi kwenda ndio jamii forum inazidi kuvamiwa na wapumbavu?
Au umeamua kuwadanganya hawa wasiojua maana za maneno ya kiarabu kuwa Quran ni lugha ya uchawi?
Nasubiri majibu

Rakims
 
Ukimkubali yesu Kristo mambo ya ushirikina yanakuwa hayana nafasi kwenye maisha yako.
Kila anaeamini Mungu mmoja na anaeamini uwepo wa Mungu mmoja na ni katika kizazi cha Adam kwa kukubali utume wa Ibrahim ambaye rafiki wa mwenyezi Mungu.

bila kubagua mitume wengine anatakiwa kumfuata na kumkubali Yesu mwana wa Maria kwa kutegemea tu kukubali kwake ni kwamba yesu bado yupo hai na atarudi nae ni moja kati ya wakombozi wa siku za mwisho ni roho ya mwenyezi Mungu na si vinginevyo hivyo Unavyotaka watu kuwaaminisha..

Hivyo usiwe unatutajia Yesu bila kutoa maana au thamani ya maana ya uwepo wake hata wachawi wanamkubali yesu na bado wanafanya yao...

Mashetani pia wapo wanaotoka katika jina la yesu lakini sio yesu wa michongo...

Hata ambao hawajamkubali yesu wapo ambao uchawi na ushirikina hauna nafasi kwao so usijifanye kuwa superior kwenye jukwaa la asilimia kubwa ya watu wasiojulikana.

Rakims
 
Back
Top Bottom