Akhi
JF-Expert Member
- Jul 12, 2021
- 3,380
- 5,906
Nilikwambieni mimi huyu jamaa ni mshirikina tu hafaiHabari mkuu naimani ni Mzima wa Afya.....
Nilitamani sana nikujibu kwa misingi ya akili lakini kwa kuwa tu umeweka mada hii kwa habari na hoja mchanganyiko itoshe tu na mimi pia nikujibu kwa misingi ya habari na hoja mchanganyiko...
Kwa kuanza nakuomba uniwie radhi kwa kukuita wewe ni Mpumbavu namba 20, Nilisema kila mpumbavu nitakae kutananae anaongea vitu asivyovijua basi nitampa cheo chake cha upumbavu yeye ni Mpumbavu namba ngapi hivyo chukua hiyo yako ni Namba 20...
Kwa kufikia hapo tu najua vidole sasa hivi vitakuwa vinakutukutia uanze kuporomosha matusi lakini usihofu mpumbavu sio tusi ni pale tu mtu anapoteleza kwenye ujuzi....
Hizo ulizoweka hapo picha na kuorodhesha kisha na kusema kwa majigambo kuwa ni Uchawi. Wanaozijua ni wenye kuita talasimu yaani talisman ambayo hutegemea na muhusika anaitizama vipi na katengeneza kwa misingi ipi...
Ikiwa wewe sio mwenye asili ya persian kujua hizi ni nini kwako inaweza kuwa shida hata kwa waarabu na waislamu wenyewe.
Kwa maana talasimu inaweza kuwa kwa mtu yoyote na hali yoyote ile unaweza kuigeuza ikawa ya kizungu,kiarabu,kihindi,kichina,kijapani,kifaransa,kuswahili hata kisukuma au kijaluo.
mradi ulichoandika hapo kiwe kina maana ambayo wewe unayoitaka iwe hiyo mathalani moja ya talasimu yoyote hapo iliyoandikwa jina Allah ukiamua kuandika Shetani inaenda tu kwa shetani kama wewe ni Mwenye kuabudu shetani
Kama ilivyo kwa madai yako kwamba hakuna anaeweza kutibu pasipo mwenyezi Mungu basi pia hakuna anaeweza kudhuru pasipo idhini ya mwenyezi Mungu...
Kuna member hapo kakwambia wewe hujui mengi bado ni kweli hujui mengi.
Mwenyezi Mungu akuepushe kuwa mmoja kati ya wanafiki kwa maana kama wewe ni msafi majukwaa ya uganga uchawi mashehe wa michongo, wachungaji waongo ulienda kutafuta nini kama sio unafiki?
Vile vile kama wao wanakosea ulitakiwa uwaambie kule kule kuliko kuja kusambaza unafiki wako huku. Kama wewe ni Mkristo basi umekosea hata kama ni mwislam basi umekosea pia kwa maana anaekosea hurekebishwa pale pale....
Unafiki mwingine ni wewe kusema kwamba Mungu anatosha kuwa tiba maana yake wachawi wako baada ya kujaribu kukutibu wakashindwa ukamrudia Mwenyezi Mungu which ni jambo zuri...
Ila shida umemrudia kinafiki kwa maana unatafuta hapa jukwaani support ya watu wakusupport kuwa kuacha uchawi ni Jambo zuri... Of cause ni jambo zuri hakuna anaekataa lakini kama wewe umeongoka basi kawaongoe na wenzio sio kuja kuwateta huku....
Pia unasema ushahidi wa maneno ya Quran kuzuga hapo bado hatujaona hapo ni wapi kwenye hizo tarasimu ulizopost kuna aya za Quran za kuzugia?
Hizo namba za kiarabu na hizo boksi boksi ndio unaita Quran? au kuona tu hilo jina la mwenyezi Mungu? Jina la mwenyezi Mungu anatumia mtu yoyote hata wanafiki kama wewe, Kujificha maovu yao.
hayo maneno hata ukimpa muarabu ni ngumu sana kuyatambua, ni lugha za kishetani.
Usiseme kitu usichokijua hii lugha ni ya kiarabu lakini sio kiarabu unachojua wewe, lugha ya talasimu kwa pamoja na lugha zingine zote mazao yake ni Babilon ambapo kila mtu pale alitoka na lugha yake jifunze historia.
Mbona kama kadri siku zinavyozidi kwenda ndio jamii forum inazidi kuvamiwa na wapumbavu?
- Kwa hiyo watoto shule wanaofundishwa maumbo ya hesabu wanafundishwa maumbo ya ushetani?
- Kwa hiyo jina hilo katikati hapo la Allah ni jina la kishetani?
- Kwa hiyo hizo pembe tano hapo ni mchoro wa kishetani?
- Kwa hiyo malaika Gabriel,Michael,Rafael na Izrael hapo ni wa shetani?
- Kwa hiyo kuandika قوله الحق و الله الملك ni ushetani yaani Neno lake ni kweli, na Mungu ndiye Mfalme?
- Kwa hiyo ٱلْفَتَّاحُ yaani Mfunguzi AMBAYE anafungua aina zote za vitu vilivyofungwa ni shetani?
Au umeamua kuwadanganya hawa wasiojua maana za maneno ya kiarabu kuwa Quran ni lugha ya uchawi?
Nasubiri majibu
Rakims
Nadhani mumejionea wenyewe