Haijulikani wazazi wengine wanaleaje watoto wao kimaadili wangali wadogo. Natoka ibadani kanisani natembea kwa miguu kuelekea nyumbani, napita mtaani njiani nakuta watoto wadogo wa chekechea wengi wanacheza pamoja michezo yao ya kitoto. Nawasalimia, watoto hamjambo? Kanaibuka katoto kamoja cha kike kanajibu salamu yangu, hatujamba tukijamba tutakuambia. Kama mtu mzima nilighadhibika na kutaka kukaadhibu katoto hako ila mazingira hayakuruhusu kumpa kifinyo kwa kutoa jibu lile baya kama mzazi. Ingeleta taharuki mtaani kwa mtu mzima mpita njia kuadhibu mtoto wa mtu. Nichofanya ni kumkazia macho makali na kumkunjia uso kumuonesha sikufurahishwa na jibu lake, walipoona nimekaza uso watoto wote walikimbilia makwao na mimi nikaona isiwe taabu nikaachana nao na kuendelea na safari yangu. Kwa kweli kuna watoto wadogo hawana nidhamu kabisa, wazazi wao waliwazaa lakini hawawapi maadili mema kuheshimu watu wengine