Ukifa leo nani atatoa lock kwenye simu yako?

Kwanini waitoe? Yaani atakae jifanya anapekenyua simu yangu nitamrudia kama ghost nitamuwinda maisha yake yote.

Kuna magemu mengi sana nimeishia level za juu sitaki mtu ayaendeleze kisha aniaribie..
Mkuu embu yaweke hapa tuyajue
 
Vitoto vingi hapa kitaa vitatoa Loki yangu hata vya jirani hapa
 
Password yangu inafikirika, wakiwaza mara kumi na tano wataipatia
 
Nitumia lock ya swipe tu ambavyo hutumii nguvu kutoa nimeweka hivyo kwajili ya dharula yeyote ambavyo inaweza kunipata muda wowote. Ukiba naifunga tu kwa email iliusisumbie watu kupitia simu yangu.
Wekeni emergency info, ambayo hata kama simu yako iko locked mtu anaweza akaona taarifa zako za kiafya na pia akaona namba zs simu za watu wako wa karibu ukipatwa na shida.

Contacts > Groups > Emergency Contacts
 
Sitaki mtu aitoe... narudia tena SITAKI SITAKI SITAKI.. wachukue urithi mwingine simu yangu waiache au kama vipi waiflash kwanza kila kitu kifutike ndio waichukue

Two weeks ago tulikwenda kumuona mgonjwa jirani wa rafiki yangu, tulipoingia tu mtoto mmoja akampokea simu nadhani amezoeana nao, katika kugongagonga akawa ameingia kwenye simu nadhani pin ilikuwa weak, tukiwa tunaongea na huyo jirani tunasikia video za miguno, aibu iliyoje tulikaa kama dakika 5 ikatulazimu kuondoka
 
Mambo ya kutumia vitu vya marehem.
Unashangaa kutumia simu wakat watu wanaendelea kutumia mpaka namba.

Juz kati nilikua na refer kwenye watsap convo zangu za nyuma kidogo.Nikarejea mpaka kwenye chat history za 2015 nikakutana na conversation yangu na engineer mmoja mshkaji wangu ambaye kwa sasa ni marehem toka 2017 na last time tulikua pamoja urambo tabora.

Nikaifungua ile chat just for memory kurejea ishu tume discus for the last time.
Ila nikashtuka sana baada ya kufungua ile chat halaf namba ikaonekana iko online watsap!ilinishtua kidogo cz ile namba ni ya voda.Maana airtel ndio nimewazoea hawachelewi kugawa namba isiyo kwenye matumiz.
Profile nikaona ni ya kike.Nikatuma message "mambo".
Baada ya muda ikajibiwa "nani ww".
Nikamwambia "mm ni mshkaji wake na jamaa aliyekua anamiliki hii namba" hivyo tu.
Akasema "MIMI NI MKE WAKE"
ohhoooooohh!! Nikatoa ndukii ila nikawaza mengi kama jamaa alikua na vimeo aisee sijui inakuaje.
Mana now days watu wanakutana na mazaga yao mitandaon 1 to 1 connection no third party wa kurejea info incase of anything so hata kama jamaa kazima may be upande wa pil hauna taarifa unaweza ukawa unatuma message tu...
Au text za magroup hiz.
 
kwamba hamna mwanaume anayejua password za mke wake maana naona tu mke wangu atatatoa ila co mme wangu
 
Kwa upande wangu atatoa mumewangu anajua password ya vitu vyangu vyote vinavyohitaj password
 
Me kila siku kabla sijalala nafuta browse history yote au hayo mambo nayaingia kwenye private browser.

Nishawahi kumbwa na fedhea sitaki kukumbuka. Ata nikiwa na usingizi nikikumbuka ile aibu usingizi uwa unakata.
Siku ukijisahau tena tu imekula kwako
 
Ukiwa na mfuatiliaji mzuri pesa zote znaptkana
 
Mimi sihofii hizo video maana kwa dunia ya sasa yenye 4G kila sehemu kutunza hizo video kwenye simu ni upuuzi...
Lakini kuna charting zipo whatsapp na kwenye sms siko tayari watu wazione aiseeh...
 
Mimi sihofii hizo video maana kwa dunia ya sasa yenye 4G kila sehemu kutunza hizo video kwenye simu ni upuuzi...
Lakini kuna charting zipo whatsapp na kwenye sms siko tayari watu wazione aiseeh...


Ni dhahiri ultimately zinakwenda kwenye mambo yanayofanana na video
 
My first daughter and my wife know my unlock pattern. Nothing is secret in my mobile phone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…