Uko sahihi sana, lakini lazima tuelezane njia sahihi ya kumsaidia mtu naye afanikiwe kimaisha hususani suala la kiuchumi. Kama ni Hawa vijana wa bongo naowaona akili zao,,, kama chenga hivi. Naweza kukupa mifano kadhaa 1. Nikishawahi ombwa na ndugu yangu nimsaidie ili naye atoke, nikamwambia watakaje? akanijibu fungua biashara niisimamie ili Nami nipate riziki. Nikafungua bucha nzuri tu na likapata wateja vizuri tu, kuuza kilo 70-100 ikawa kawaida kabisa na tukakubaliana faida itakayopatikana tutagawana pasupasu. Aiseee baada ya miezi kama 6 hv sikuamini kilichokuwa kinatokea. 2. Wapili tukaplani mipango na ndugu mwingine tufanye ufugaji nikamwambia sawa, coz tayari nilkuwa na shamba ikawa niliweka miundombinu tu. Basi tukaanza harakati na hata hivyo nikamwambia tutafute na fremu ya karibu ili pia wakati unasimamia ufugaji tufungue na duka ili usiwe Ido sana. Baada ya kuteleza kwa muda Mimi nanunua pumba Tani kadhaa huku mwenzangu baadhi anauza. Sasa Bora hata angeenda kufanyia maendeleo, zaidi ni kutembeza mjegeje tu kwa vibinti na wake za watu. Nikishaapa ukitaka nikusaidie nione juhudi zako na uwe na umezianza harakati Mimi nikubust lakini hivihivi tu hata mia huna pita mbali na Mimi.