Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 694
Fanya mazungumzo yenu yawe rahisi.
Fanya mnapokuwa pamoja iwe rahisi kwako na kwake.
Fanya ajihisi maisha yake ni rahisi akiwa na wewe. Simaanishi kifedha. Bali kihisia kwa kujiachia na kutokua mkoloni bila sababu.
Mwanamke akiona ni rahisi kuwa nawe atakua na furaha akiwa nawe. Na ataona chanzo cha kupata furaha ni kwako. Kwaiyo sehemu atakayokua anataka kuwa ni kwako pamoja na wewe.
Kuwa na misimamo na mipaka ni muhimu. Lakini isikufanye ushindwe kujiachia na kufurahi na mwanamke uliyenaye. Ukiona mipaka na misimamo yako haizingatiwi heri ubadili mwanamke wa kuwa naye.
Ukifanya maisha yenu yawe rahisi, mnakua mnaelewana kirahisi.
Mnakua kama vile mlijuana hata kabla hamjazaliwa.
Na penzi utalifurahia.
Ili kumfanya aone maisha na wewe ni rahisi mfanye ajiachie kwako kwa kuwa we mwenyewe umejiachia, kujua anachokitaka kihisia na kumpatia. Pia kutumia akili ya kawaida kujua wapi umuongoze wapi umuache na mambo yake (kumpa uhuru binafsi).
Bila ye kujihisi uhuru kwako, ataona kafungwa kwako na ataanza kufanya maisha yenu yasiwe rahisi ili muachane akatafute uhuru wake.
Ukitaka kujua haumpi urahisi kuwa na wewe utaona dalili hizi,
Mara nyingi inatokana kwamba we mwenyewe hujajiachia. Kumwambia vitu visivyoeleweka. Una maswali mengi. Mkali kupitiliza. Una wivu sana. Umemweka mwanamke juu na unamtaka kama vile ndo uhai wako. Unamfukuzia kupita maelezo. Unakua unamfatilia sana mwanamke.
Ukiona unamfatilia sana mwanamke ujue umemuweka kama kipaumbele chako, na utakua umemweka juu yako. Kufuatilia pia kuna mipaka sio umfuatilie kila kitu chake hasa kama ndo mnaanza mahusiano.
Tumia tu akili ya kawaida kujua kwamba naye ana uhuru wake binafsi.
Hajafungwa na wewe kwa kila kitu.
Ukimfuatilia sana hatojisikia amani, uhuru au kujiachia kwako. Na ataona maisha na wewe ni kama vile utumwa. Maisha hayatakua rahisi.
Kama ndo mnaanza mahusiano usimwingilie sana kwenye vitu vyake.
Kama mna mahusiano yanayokufurahisha mpe uhuru wenye mipaka.
Nikutakie Siku Njema Na Ujiachie Ufurahie Siku.

- Utakua unaogopa atakufikiriaje mana unajua kidogo tu anafura.
- Atakua anakusema ovyo na kukufanya uombe ombe msamaha.
- Penzi anakunyima/ anakupa ukiomba sana kwa masharti.
- Anakasirika haraka na mna ugomvi mara kwa mara.
- Hakuambii vitu/ anakuficha ficha na kununa.
- Ataanza kukupotezea na kujitoa kwako.
- Atakuambia hana hisia na wewe skuizi.
- Ana sababu nyingi kwanini msikutane.
- Hataki muongelee mahusiano yenu.
- Unajikuta unaogopa kumkosea.
- Utaona haeleweki.