Pdidy
Platinum Member
- Nov 22, 2007
- 62,101
- 38,487
UKIENDA KUFANYA ZINAA, KUMBUKA MAJINA HAYA, ALAFU UJISHAURI BAADA YA HAPO UCHUKUE UAMUZI UTAKAO KUJA.
1. KUFANYA ZINAA NI KUFANYA UPUMBAVU KIBIBLIA.
2 Samweli 13:5, 11-14 (Biblia Takatifu) Yonadabu akamwambia, Lala kitandani mwako ujifanye mgonjwa na babako atakapokuja kukutazama, umwambie, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, anipe mkate nile, akaandae chakula machoni pangu nikione, nikakile mkononi mwake.
Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu.
Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinitenze nguvu; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu.
Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa.
Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye.
2. UKIFANYA ZINAA, KIBIBLIA UNAONEKANA NI MTU USIE NA AKILI KABISA, UNAEFANYA JAMBO LA KUANGAMIZA KESHO NA KIPAWA CHAKO.
Mithali 6:32-33 (Biblia Takatifu) Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.
3. KUZINI NI KUJIVUNJIA HESHIMA YAKO, (Kila unapoenda kuzini Malaika na viumbe wa Mbinguni husema Mwone flani anaenda kupoteza heshima yake.
Mithali 6:33 (Biblia Takatifu) Mtu aziniye na mwanamke huvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.
4. UZINZI UNAITWA UBAYA MKUBWA AMBAO HUPELEKEA MTU KUMKOSA MUNGU. Unapoenda kuzini rohoni husemezana haya muone anaenda kumkosa Mungu wake kwa hicho kitendo!
Mwanzo 39:9 (Biblia Takatifu) Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?
5. UZINZI UNAITWA FEDHEHA ISIYO FUTIKA!
Unapoenda kuzini fahamu unaenda kujifedhehesha, tena fedheha isiyo futika kirahisi.
Mithali 6:33 (Biblia Takatifu) Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.
6. UZINZI UNAITWA JERAHA. Unapoenda kufanya sinaa Ukiwa unasema tukafanye mapenzi ila ukumbuke unaenda kujijeruhi kabisa Mtu wa Mungu.

.Utapata jeraha la Moyo!
.Jeraha la nafsi.
Ukisema nikuonyeshe mtu asiye na Amani maishani mwake nitakuonyesha Mzinzi, Huu ni ukweli hata wewe unafahamu.
7. ZINAA NI MSIBA UNAO JITEGEMEA KWAAJILI YA KARAMA, VIPAWA NA HATIMA ZA WATU.
.Mfalme suleiman alizikwa kwaajili ya zinaa pamoja ile hekima yake.
1 Wafalme 11:1-4 (Biblia Takatifu) Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,
na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.
Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.
Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.
.Mwingine ni Mnadhiri wa Mungu Samsoni Zinaa ilimzika, Haitoshi ningelimtaja Ammoni pia.
Aisee zinaa ni Mbaya sana, Tafta msaada mapema kabla hujaizoea wala hujaita udhaifu wangu!
Mtu wa Mungu usiogope kuomba Msaada ukasaidiwa kabla tatizo halijawa kubwa bado! Usikubali zile lugha za haiwezekani kuwa mtakatifu, Inawezekana ndugu yangu!
Njoo Inbox tusaidiane, Kuchukia uovu ni kuusema sio kunyamaza ikiwa unateswa hapo unakufa ukiwa unajiona kabisa Mtu wa Mungu.
Mungu akubariki sana.
Bado una nafasi ya kubadilika ewe mzinzzii mbobeziiii
Au siooooo???usisubiri haya majina yajr jukusalimia au sio??