Ukifika Mabibo sokoni ndo utajua kwanini watu hawataki kuachia office

Ukifika Mabibo sokoni ndo utajua kwanini watu hawataki kuachia office

mzee wa mafisa wa mikakati hapajui hapa ee?
maxresdefault-14.jpg
Yeye hakusanyi ushuru, kuna watendaji, diwani, manispaa, uongozi wa soko n.k
 
Wanajamvi,

Mimi binafsi napenda sana biashara kitu ambacho kimenifanya niwe mfuatiliaji wa mambo mbalimbali yahusuyo biashara. Nilichikiona Leo pale Mabibo soko la matunda miundo mbinu ya pale inasikitisha.

Ushawahi kuona soko lenye tope na watu wakitembea peku wakivuruga hilo tope na business zinaendelea kama kawa noti zinahesabiwa kwa wingi kama bank. Alafu ukitoka pale nje kuna biashara ya kuosha miguu mh! Dar es Salaam jamani.

Sijui ushuru unatumika kufanya kazi gani pale ni hatari sana kwa afya za watu.Nilichojifunza ni kwamba hakuna kazi rahisi hapa kwa dunia.

Karibu mjionee hasa msimu huu wa mvua, ila kule upande wa viazi ni kusafi. Naamini hawa wafanyabiashara wangeamua badala ya kutoa ushuru watengeneza miundombinu wakijichanga buku5 daily nahisi in 2 yrs pangependeza sana kama Manispaa imeshindwa kuboresha miundombinu.
Ushuru ni dili za watu ukishangaa matope ya mabibo usisahau na mahandaki ya stand ya kimataifa ya mabasi ya Ubungo kama uwanja wa mnada wa ng'ombe na ushuru unatolewa,wangegoma kutoa ushuru wachangishane waweke miundombinu vizuri ila lzm kuwepo na tofauti kati ya third world na develop world.Ndo utalii wa ndani huo kivutio,Pesa juu ya tope au mashimo ya Ubungo stand.
 
Duuu hiyo biashara ya kuosha miguu
Ipo hata soko la Ilala nilionaga kuna watu wanafanya izo kazi,kunawa shilingi mia .........na kijana wa watu unamkuta ana madumu kama kumi ivi ameyaweka pembeni
 
Kwanini wasiweke pavement? Nadhani ndyo suluhisho
 
Back
Top Bottom