duh ni balaa siunajua tena na ugeni wa route unakuta route hauna uzoefu nayo ndio shida,ila next time siwezi kupigwa kizembe ivyoUkiachana na Dar es salaam huko mikoani the only time ya kusafiri gari za uhakika ni kuenda stendi alfajiri ndio gari zipo za uhakika. Ikifika saa tatu kuendelea ni gari za kuunga unga tu. Ingekua mimi ningepanda gari mpaka chalinze halafu hapo ningetafuta gari nyengine ya kuunga.
Alisikiliza akili za wapiga debe.Hili gari mm ndio kwanza nalisikia leo Tausi trans 🤣🤣🤣
Gari za tanga zipo zimatokea dom sema ww ulifichwa
Sio kampuni zote, mwezi wa pili nilisafiri kwenda mkoa X, gari tulilopanda halikuwa lile tulilotakiwa kupanda japo yote ni ya kampuni moja, hivyo tukiwa safarini kila abiria akarudishiwa kiasi fulani cha pesa cha ile nauli aliyolipa mwanzo wa safari. Ilikuwa mara ya kwanza kuona wenye basi wanarudisha pesa kwa abiria bila msuguano.Watu wa magari hawanaga uteja kabxa ukisharipa nauri tu.s
yah icho kitu nilikiona shida pia ilikuwa kwa aliyenidaka nilimwambia nichekie inayotoka DOM akanilengesha kwa wapuuzi,naskia pia kuna TASHRIFF ya moro to tangaHili gari mm ndio kwanza nalisikia leo Tausi trans 🤣🤣🤣
Gari za tanga zipo zimatokea dom sema ww ulifichwa
Sema wewe unaendana na jina lako kabisaMambo vipi ?
Leo bhana nimekuja na mada inayotuhusu sisi wote maana wote umu naamini uwa tunasafiri na nchi hii sijui ata kama kuna chama cha wasafiri maana wasafiri tunaonewa sana na kampuni za mabasi.
Utakuta unaenda stand halafu unakatishwa ticket na unaambiwa gari itaondoka muda fulani. Kwa mfano saa 4 asubuhi utashangaa unakuja kuondoka saa 9 na gari haifiki mwisho wa safari kama walivyoandika kwenye ticket unashangaa njiani unafaulishwa tena yaani unateseka balaa mpaka unapofika mwisho wa safari yako
Hii ishu imenitokea pale Msamvu nilikuwa nasafari ya MORO-TANGA nikaenda Msamvu mida ya saa 3:00 asubuhi nikapokewa na wapiga debe wakanipeleka kwa agent wa kampuni ya magari yanayoitwa TAUSI.
Akaniahidi gari itatoka IFAKARA na kufika msamvu saa 4 asubuhi na safari ya Tanga itaanza matokeo yake gari ikafika saa 9 mchana na tukaanza safari kufika mkata wakatufaulisha kwenye coaster tena kwa kusimama.
Yaani tumekuja kufika tanga saa 4 usiku na inaonekana ndo mtindo wao kuwadanganya abiria muda na destination ya safari ,yaani wanadanganya wanafika tanga mjini ila wakifika mkata wanafaulisha
Kwa Hiyo nakushauri ukifika msamvu-morogoro kama unasafari ya TANGA usijichanganye kupanda gari inayoitwa TAUSI TRANS ambazo zinafanya safari zake IFAKARA-MOROGORO utapigwa na kitu kizito na pesa umetoa ,kama kuna gari nyingine kama izo orodhesheni maana abiria hii nchi hatuna haki kabisa na tunaonewa.
hapo umesema hujawah kuona hyo ndo mara ya kwanz.Sio kampuni zote, mwezi wa pili nilisafiri kwenda mkoa X, gari tulilopanda halikuwa lile tulilotakiwa kupanda japo yote ni ya kampuni moja, hivyo tukiwa safarini kila abiria akarudishiwa kiasi fulani cha pesa cha ile nauli aliyolipa mwanzo wa safari. Ilikuwa mara ya kwanza kuona wenye basi wanarudisha pesa kwa abiria bila msuguano.
Huyo anayevuta resi sio hata dereva ni deiwaka au mpiga debe anayejifunza gari unakuta dereva amelala zake hukoHahaha msamvu kuna Newforce hapo karibu na mlangoni linaenda Dar. Ukifika madalali wote wanakuambia hilo gari ndio lililopo na linaondoka fasta,huku dereva akivuta vuta resi. Usija ukajichanganya ukapanda maana hilo kama daladala na haliondoki sasa hivi.
Bora upande abood au BM hata kama ukiliona tupu. Abooud hata likiwa tupu linajaa haraka kuliko hilo kanjanja ambalo utapanda kwa kua na haraka zako kumbe ndio unachelewa.
Soma vizuri, alikata tiketi kwa agent na aliambiwa gari litafika saa 4.Kwa hiyo agent ambae ameaminiwa na kampuni ndie aliedanganya na huwezi kuitoa kampuni kwenye lawama.Mkuu kutaja majina ya makampuni si sahihi sana cuz unaharibu biashara ya watu.
Wewe ndo una makosa kumwamini mpiga debe, we ungetulia na kibegi chako usubiri gari inayopita mda huo udandie pyuuuu mpaka Tanga, sasa ukawaruhusu wapiga debe wakukalishe mpaka saa 9, apo mwenye shida ni wewe.