Ukifika Msamvu pale Morogoro, usipande magari yafuatayo...

Ukifika Msamvu pale Morogoro, usipande magari yafuatayo...

Ukiachana na Dar es salaam huko mikoani the only time ya kusafiri gari za uhakika ni kuenda stendi alfajiri ndio gari zipo za uhakika. Ikifika saa tatu kuendelea ni gari za kuunga unga tu. Ingekua mimi ningepanda gari mpaka chalinze halafu hapo ningetafuta gari nyengine ya kuunga.
Sahihi kabisa
 
Stendi kuna utapeli mwingi sana.
 
Mkuu kutaja majina ya makampuni si sahihi sana cuz unaharibu biashara ya watu.
Wewe ndo una makosa kumwamini mpiga debe, we ungetulia na kibegi chako usubiri gari inayopita mda huo udandie pyuuuu mpaka Tanga, sasa ukawaruhusu wapiga debe wakukalishe mpaka saa 9, apo mwenye shida ni wewe.
Ni sahihi kutaja makampuni yenye huduma mbovu za kitapeli, hizo biashara za kipuuzi zinatakiwa ziharibike na zife kabisa.
 
Wewe umetoka nyumbani kwako, unajua bei au nauli na unajua inapokwenda. Kwanini uruhusu mpiga debe akushikie akili ya safari yako?

Halafu hizo ticket huwa mnapewa kama mapambo au mkataba wa kuonesha umelipa nauli na muda wa kuanza safiri? Pia gari unayo safiri nayo.

Mimi kanuni yangu ni hizi....

Nikifika stend
1. Konda aniandikie ticket kamili yenye
...Namba na jina la basi au gari
....Jina langu
....Siti namba
.....Tarehe na muda wa kuondoka
.....Mahali natoka na ninaenda
....Namba zake za simu

Akijichanganya tu amesema gari inaondoka saa 2, muda ukafika hakuna gari, lazima azitapike pesa. Tena stendi zote kubwa Sumatra/Latra wapo.

Atajuta
Hakuna tofauti ya wapiga debe, makonda na Madereva stendi, wote ni kitu kimoja tu.
 
Biashara ngumu ingia uone. Unataka.basi la watu 60 lisafiri na abiria 10 km 700 seriously. Kama una haraka panda noah/ coaster
Huko kwa Wachina yapo mabasi ya abiria 40, 30 hadi 20, walete hayo. Kwanza ni ujinga sana kuwa na mabasi ya abiria 50 na 60, yanachelewesha muda sana na ni hatari kubwa kwa usalama afya wa abiria na ajali barabarani.
 
Huko kwa Wachina yapo mabasi ya abiria 40, 30 hadi 20, walete hayo. Kwanza ni ujinga sana kuwa na mabasi ya abiria 50 na 60, yanachelewesha muda sana na ni hatari kubwa kwa usalama afya wa abiria na ajali barabarani.
Magar madogo yapo kibao kwa nini ung'ang'anie bus?
 
Mambo vipi ?
Leo bhana nimekuja na mada inayotuhusu sisi wote maana wote umu naamini uwa tunasafiri na nchi hii sijui ata kama kuna chama cha wasafiri maana wasafiri tunaonewa sana na kampuni za mabasi.

Utakuta unaenda stand halafu unakatishwa ticket na unaambiwa gari itaondoka muda fulani. Kwa mfano saa 4 asubuhi utashangaa unakuja kuondoka saa 9 na gari haifiki mwisho wa safari kama walivyoandika kwenye ticket unashangaa njiani unafaulishwa tena yaani unateseka balaa mpaka unapofika mwisho wa safari yako

Hii ishu imenitokea pale Msamvu nilikuwa nasafari ya MORO-TANGA nikaenda Msamvu mida ya saa 3:00 asubuhi nikapokewa na wapiga debe wakanipeleka kwa agent wa kampuni ya magari yanayoitwa TAUSI.

Akaniahidi gari itatoka IFAKARA na kufika msamvu saa 4 asubuhi na safari ya Tanga itaanza matokeo yake gari ikafika saa 9 mchana na tukaanza safari kufika mkata wakatufaulisha kwenye coaster tena kwa kusimama.

Yaani tumekuja kufika tanga saa 4 usiku na inaonekana ndo mtindo wao kuwadanganya abiria muda na destination ya safari ,yaani wanadanganya wanafika tanga mjini ila wakifika mkata wanafaulisha

Kwa Hiyo nakushauri ukifika msamvu-morogoro kama unasafari ya TANGA usijichanganye kupanda gari inayoitwa TAUSI TRANS ambazo zinafanya safari zake IFAKARA-MOROGORO utapigwa na kitu kizito na pesa umetoa ,kama kuna gari nyingine kama izo orodhesheni maana abiria hii nchi hatuna haki kabisa na tunaonewa.
Wamewakuta nyie wanyonge! Mi ningeua mtu au warudishe pesa hapo mkata nipande gari nitakayochagua mimi
 
Siwatetei hao Tusi na wala sikulaumu mleta mada, lkn ingekuwa vizuri mtu kusikia maelezo ya upande wa pili ili kujiridhisha kuhusu maelezo yako.

Siku hizi imekuwa kawaida wafanyabiashara, au watu mbali mbali kuchafuana bila sababu kupitia mitandao ya kijamii. Hivyo mambo ya aina hii ili mtu akubaliane nayo inahitaji ushahidi wa kutosha. Ndomaana hata mahakamani mtuhumiwa nae hupewa nafasi ya kujitetea ili kuangalia kama tuhuma alizoshitakiwa nazo ni za kweli au ni kanjanja.

Hata hivyo sio mbaya watu kuchukua tahadhari mapema.
Bila shaka we ndio kuli wa iyo kampuni ya TAUSI
 
Back
Top Bottom