Ukifika Msamvu pale Morogoro, usipande magari yafuatayo...

Ukifika Msamvu pale Morogoro, usipande magari yafuatayo...

Sio kampuni zote, mwezi wa pili nilisafiri kwenda mkoa X, gari tulilopanda halikuwa lile tulilotakiwa kupanda japo yote ni ya kampuni moja, hivyo tukiwa safarini kila abiria akarudishiwa kiasi fulani cha pesa cha ile nauli aliyolipa mwanzo wa safari. Ilikuwa mara ya kwanza kuona wenye basi wanarudisha pesa kwa abiria bila msuguano.
Hao waelewa nilikata tiketi happy nation kutoka mkoa y kwenda mkoa z aisee pale kwa tiketi imeandika namba ya gari jipya sasa mida ya kupakia si linakija limechoka na namb D wakati tiketi ni namba E aisee siku mind coz n usku saa 10 lkn sio vzr
 
Hapana zitajwe tu Majina, ili wasimamizi wao wasikie,
Ipo kampuni inaitwa MAJINJA,hii bas niliikuta mbea .
Wakati huo mm natoka sumbawanga nimefika mbea saa 12 jion..nikatafuta bus itakayoweza kufanya safar za usiku Mbeya dar…..aisee Ndio Nikaingia ktk hiyo BUS 🚌 MAJINJA Nilichokutana nacho hata bure sitaki pesa yangu mwenyew af inantesa sasa.
Nikakata tiket , nikauliza na muda sa2 usiku bus ndio inaanza safar.
Huwezi amini pale mbea tulitoka sa4 na nusu kwa makelele sana.
Bus ikaanza safari mpka uyole ,tuganda sana pale uyole.ikabidi tuhoji shida ni nni,wakatujib anasubiriwa dereva mwenye safar yake abiria tuvuteni subira anakuja hatokei mbali.
Pale uyole tumetoka saa 6 usiku,dereva kaja anataka kuanza safar sasa taa za mbele haziwaki zemegoma gafla,ikabidi aitwe fundi tkasubiri fundi aje wa hiyo kampuni.
fundi kachokonoa chokonoa pale weee zimewaka,safari ianze tukatembea kidogo hiv mbele kuna trafik wanakaa ukiwapita hao trafiki kuna kamlima aisee gari ikashindwa kupanda inarudi nyuma 😭
Abiria walipiga ukunga,tukashuka salama tukatembea kwa miguu mpaka walipo wale trafiki kwa Msaada zaidi na uzuri abiria wote tuliazimia tubasilishiwe gar hili bus hatulitaki hatuna imani nalo ,aidhaa turudishiwe nauli.

Wao wenye gar wanadai gar lao nizima kwani nijana tu limetoka dar .abiria tunasema gari hili nibov,sasa huyo meneja anachokiongea sasa anakijua yey kalewa domo zito anatukana tu
Abiria tukawa letu nimoja tu gar hili hatuna imani nalo.
Pale wale trafiki walitusaidia jambo moja akapigiwa watu wa latra,wakaambiwa juu ya hiyo shida,mwafaka ikabidi turudishwe mbeya tutaftiwe gari nyingine eidha turudishiwe nauli.
Tukafika mbeya wale jamaa wakatukimbia,Wakaja alfajiri “et abiria Mmeamkaje “
nakumbuka alikuja askari mmoja wa latra huyu jamaa kwakweli ni askari ambae anajua nn anachofanya.

Tukaitwa wote abiria wanao enda dar tupo 35,wanaoshuka iringa 16,mikumi wapo 8,moro goro 23 hawa walikua watu wakanisani
Kila abiria alipandishwa bas yake,yule meneja aliambiwa utajua wewe pakulipa bas ya wenzio.
Kimbembe sie tunaofika dar tukpata costar mpaka iringa,iringa kwa mujib wamakubaliano kuna gar inatusubir ya dar kufika pale iringa gari hiyo inayotusubir alieachiwa gar anadai abiria watoe elf5 kila mmoja,watu wakagoma kushuka.wale jamaa wakaanza kulumbana,kupatikana kwa muafaka akaja mwenyeketi mkoa wawasafirishaji abiria na latra Tena daaah hiyo siku sisahau nafika mmi dar nimedhoofika kishenzi
Ungetafuta demu uende ukalale nae lodge
 
Wale mameneja wa stendi huwa Wana majukumu gani? Je changamoto za abiria pale stendi yeye anawajibikaje?
 
Mambo vipi ?
Leo bhana nimekuja na mada inayotuhusu sisi wote maana wote umu naamini uwa tunasafiri na nchi hii sijui ata kama kuna chama cha wasafiri maana wasafiri tunaonewa sana na kampuni za mabasi.

Utakuta unaenda stand halafu unakatishwa ticket na unaambiwa gari itaondoka muda fulani. Kwa mfano saa 4 asubuhi utashangaa unakuja kuondoka saa 9 na gari haifiki mwisho wa safari kama walivyoandika kwenye ticket unashangaa njiani unafaulishwa tena yaani unateseka balaa mpaka unapofika mwisho wa safari yako

Hii ishu imenitokea pale Msamvu nilikuwa nasafari ya MORO-TANGA nikaenda Msamvu mida ya saa 3:00 asubuhi nikapokewa na wapiga debe wakanipeleka kwa agent wa kampuni ya magari yanayoitwa TAUSI.

Akaniahidi gari itatoka IFAKARA na kufika msamvu saa 4 asubuhi na safari ya Tanga itaanza matokeo yake gari ikafika saa 9 mchana na tukaanza safari kufika mkata wakatufaulisha kwenye coaster tena kwa kusimama.

Yaani tumekuja kufika tanga saa 4 usiku na inaonekana ndo mtindo wao kuwadanganya abiria muda na destination ya safari ,yaani wanadanganya wanafika tanga mjini ila wakifika mkata wanafaulisha

Kwa Hiyo nakushauri ukifika msamvu-morogoro kama unasafari ya TANGA usijichanganye kupanda gari inayoitwa TAUSI TRANS ambazo zinafanya safari zake IFAKARA-MOROGORO utapigwa na kitu kizito na pesa umetoa ,kama kuna gari nyingine kama izo orodhesheni maana abiria hii nchi hatuna haki kabisa na tunaonewa.
Pole sana mkuu. Hadi nimekuonea huruma.

NRNE ndio dawa ya haya yote.
 
Mkuu kutaja majina ya makampuni si sahihi sana cuz unaharibu biashara ya watu.
Wewe ndo una makosa kumwamini mpiga debe, we ungetulia na kibegi chako usubiri gari inayopita mda huo udandie pyuuuu mpaka Tanga, sasa ukawaruhusu wapiga debe wakukalishe mpaka saa 9, apo mwenye shida ni wewe.
Ndivyo inavyotakiwa ndio maana kwenye page zao kuna sehemu z kutoa maoni.

Tz tuache janja janja tuwe tayari kujirekebisha
 
Wale mameneja wa stendi huwa Wana majukumu gani? Je changamoto za abiria pale stendi yeye anawajibikaje?
tz miyeyusho sana kama pale msamvu ukifanyika uchunguzi watu wanaonewa sana mule na kuna unyanyasaji nishashuhudia mpiga debe anamtongoza mtoto wa kiume ila wao hawakujua kama nawachunguza,abiria kibao wanaachwa na magari kwa makosa ya maagent na hawasaidiwi na msala anatupiwa abiria na naskia sijui kuna LATRA na ulinzi stand sijui ata wanafanya kazi gani
 
Mkuu kutaja majina ya makampuni si sahihi sana cuz unaharibu biashara ya watu.
Wewe ndo una makosa kumwamini mpiga debe, we ungetulia na kibegi chako usubiri gari inayopita mda huo udandie pyuuuu mpaka Tanga, sasa ukawaruhusu wapiga debe wakukalishe mpaka saa 9, apo mwenye shida ni wewe.
Pamoja na kuondoka saa 9 ila halijafika pia mwisho wa safari pia, mleta mada ana hoja.
 
Hili gari mm ndio kwanza nalisikia leo Tausi trans 🤣🤣🤣

Gari za tanga zipo zimatokea dom sema ww ulifichwa
Tausi Ni Tata Toka Ifakara ~Dar


Saa Tatu Asubuhi Kuna Simba, Tashriff, Hanein Kuanzia Morogoro Kwenda Tanga

Dodoma Kwenda Tanga
Simba , Ratco, Nacharo, Tashriff,

Umeshindwa Kabisa
Panda
Dodoma ~Lushoto
Kiluwa Burdan Utatelemka Segera
 
Msamvu pana mambo ya ajabu mno,wapiga debe wasumbufu,wanakudaka juu juu,unatajiwa kuda mzuri.Ukilipia tu wanakula kona wanakuacha kama yatima,ukifuatilia unaishia kutukanwa.Pia wana ushirikiano mno ni kama hakuna utawala pale.
 
Hata aboood hao washenzi tu,
Nilitoka Tukuyu nikafika Mbeya late km sa mbili nikakuta gari zimeenda,
Km kawaida agent na mpiga de e kuna gari natoka Tundu a sa tatu naondoka.
Siti ipo.
Aloo sa tatu na kitu hiloo wangu wangu.
Nikadumbukizwa ndani route kaanza.
Duh, nilikaa kwenye kiroba na kusimama kwenye korido ya bus
Mpk Dar.
Mapumziko ilikua Moro garage kwao.
 
Msamvu pana mambo ya ajabu mno,wapiga debe wasumbufu,wanakudaka juu juu,unatajiwa kuda mzuri.Ukilipia tu wanakula kona wanakuacha kama yatima,ukifuatilia unaishia kutukanwa.Pia wana ushirikiano mno ni kama hakuna utawala pale.
Usikate tiketi,mwambie likifika nikakaa utanikatia
 
Wapiga debe ndio wanaoharibu biashara za watu ;

Ila ndio hivyo kibongo bongo tunabebana mradi wote tupate riziki.
 
Ukiachana na Dar es salaam huko mikoani the only time ya kusafiri gari za uhakika ni kuenda stendi alfajiri ndio gari zipo za uhakika. Ikifika saa tatu kuendelea ni gari za kuunga unga tu. Ingekua mimi ningepanda gari mpaka chalinze halafu hapo ningetafuta gari nyengine ya kuunga.
Arusha, Moshi dar huwezi Kuta huo ujinga.
 
Kuna Bus inaitwa SEA BUS ukiwa mpanda unaambiwa inatoka mpanda to mwanza kumbe bana inaishia Tabora!.

Ile gari inatembea na mafundi wa5 kwahiyo jiongeze kabisa kwamba kazi ya hao mafundi ni nini safarini.

Kifupi tu kutoka mpanda katavi hadi tabora gari ilitengenezwa mara4!
 
Back
Top Bottom