Ukifikisha miaka 30 achana na salamu ya shikamoo, ni unafiki

Vitoto vya dasalama vikikupa shikamoo labda kuna katukio anataka kufanya,,,,,akuombe hela au msaada mwingine ila hivihivi ngumu
 
Kwanza ni salamu ya kitumwa kwaajili ya watumwa.Kuendelea kutumia salamuu hii ni ishara kwamba tumekubali kuendelea kuwa watumwa,baada ya uhuru salamu hii ilitakiwa kufutiwa mbali.Inabidi tuache kuitumia kwani hatupo utumwani kama waarabu walivyo wafanyia mababu zetu.
 
Nyie ndio mnaofanya bangi ionekane mbaya
 
Na kama ni baba yako, mama yako au babu na bibi?
Na kama ni baba yako, mama yako au babu na bibi?
Kwetu usukumani hao wote ukiwasalimia kwa kiswahili huona kama umewadharau vile, yani mara zote hupendelea kusalimiwa kwa kisukuma basi na hata kama ni mgeni bado watakufunza lugha yao tu.
 
Sawa kuanzia Leo ntaacha hii tabia
 

ELIMU ELIMU ELIMU!!!! Nchi hii ina janga la Elimu!!!!
Yaani hata kusalimia mtu ni mjadala
Salimia mtu aliye mkubwa kwako iwe miaka miwili mitatu nk (dada yako/kaka yako/ wazazi wako nk nk nk
Mtu ambaye kichwani hamnazo ndiye hupoteza muda kujadili eti salamu abc?
Kwani inakupunguzia nini????
 
Salamu za Shikamoo ni za kitumwa.

Ndiyo maana Zanzibar watu wengine wanatumia "Cheichei" . Unasalimu "Cheichei", unajibiwa "Cheichei".

Wale wanakijua Kiswahili. Wanaujua utumwa, wanajua historia ya salamu hii ya "Shikamoo" na mizizi yake kwenye utumwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…