Ukifikisha miaka 30 achana na salamu ya shikamoo, ni unafiki

Ukifikisha miaka 30 achana na salamu ya shikamoo, ni unafiki

Una umri gani? Na Baba na Mama wako unawasalimiaje? Vipi kuhusu Babu na Bibi achana na masela.
 
Nina ugonjwa na hiyo salamu
Sijui ni siipendi? Hata sielewi… ila kunikuta na mashikamoo mimi ni nadraaa, 2/10 kwa kifupi.
Na walioleta hizi GOOD Morning Madam/ Sir, wapewe maua yao 🤣🤣

Ila sasa huku Kaskazini nimenote vitoto vinasalimia hivyo balaa. Ni tofauti na Dar, Dar unaweza pishana na katoto kimya kimya. Ila vya huku ni shwaa kamekupa shkamoo na hamjuani.
ina maana tukikutana KWA MSOLA hautaniamkia SHKAMOO?

Ntakucharaza hadi basi
 
Mimi hiyo shikamo kwangu huwaga ni kama silaha binadamu si wanapendaga heshima….mj hata nikikutana na mtu kajichokoea naona kanizidi umri namtandika shikamo yake akiwa kaka shikamo braza sister,mama au baba kwani shingapi [emoji3][emoji3]basi wanaonaga rahaa wenyewee na binafsi huwa inanifungulia mlango wa mawasiliano na mahusiano na msaada kwa haraka sana
 
Unapofikisha miaka 30, wewe ni mtu mzima, a chana na Salaam ya Shikamoo.

Shikamoo inapaswa kutumia na watoto wadogo (29 below). Mtu mzima una watoto, wengine wajukuu, eti na wewe unaamkia shikamoo.

Ni aibu mtu una miaka 30 above unaamkia shikamoo. Ni kujidanganya, kujirudisha nyuma. Ni kuidanganya nafsi yako.

Miaka 30 umeona na kufanya mengi. Waache watoto wadogo waitumie shikamoo.

Utakuta mtu ana miaka 30 anamwamkia mtu mwenye miaka 40, 50, wakati wote ni wazee, ni aibu na kuidanganya nafsi kwamba wewe ni mtoto mdogo.

Miaka 30 tayari wewe ni mtu mzima
Jamani hii kitu ipo kwa watoto wa International school hayasalimia unasikia whats your name, ukimwambia tu VVM unasikia Hi VVM
 
Yani mimi mtu ili nimpe shikamoo mpaka nione ana mvi zimajaa tele kichwani kwake
Sikuhizi hawana mvi ndugu, wanapakaa mablack manywele...

Ila utaona tu sura imeporomoka...

NB: Mkubwa apewe salamu yake.
 
Ungesema Sasa tuwaamkiaje wazee wetu au waliotuzidi umri za sahizi au habari au
Shangaa na wewe, eti habari yako mama? Hawa watu ni wajinga sana. Hivi kiuhalisia na hali halisi ya sasa, shikamoo ni utumwa? Achana na maandishi na historia, talk about realities
 
Mimi niko na 30 26 ananiambia shkamoo asee ni huzuni kwakweli
 
Sipendi kusalimia maana watu wako kama hawataki kusalimiwa,ukikaaa kimya shida ukisalimia shikamooo hawataki,Sasa wanataka nini?
 
Ni kweli. Ni kiarabu.

Hiyo salamu maana yake ni “Niko chini ya miguu yako”

Nadhani ilitumiwa na waarabu kwa watumwa.
Hiyo ilikuwa maana yao,lkn sisi ktk kiswahili chetu hatumaaanishi hivyo!tumeitohoa na kuipa maana yetu
 
Unapofikisha miaka 30, wewe ni mtu mzima, a chana na Salaam ya Shikamoo.

Shikamoo inapaswa kutumia na watoto wadogo (29 below). Mtu mzima una watoto, wengine wajukuu, eti na wewe unaamkia shikamoo.

Ni aibu mtu una miaka 30 above unaamkia shikamoo. Ni kujidanganya, kujirudisha nyuma. Ni kuidanganya nafsi yako.

Miaka 30 umeona na kufanya mengi. Waache watoto wadogo waitumie shikamoo.

Utakuta mtu ana miaka 30 anamwamkia mtu mwenye miaka 40, 50, wakati wote ni wazee, ni aibu na kuidanganya nafsi kwamba wewe ni mtoto mdogo.

Miaka 30 tayari wewe ni mtu mzima
Eti eeenh?Mimi sikujua hili.Kwa hiyo hata baba na mama zetu wazazi tunawapiga na "Whoooza...whoooozaa"?Au siyo?
 
Back
Top Bottom