Ukifuatilia kile kinachoitwa ujanja wa mjini ndio ushamba wenyewe

Nadhani upo sahihi na hoja zako nakubaliana nazo kwa 100%.
 
Wajanja wa mjini mnaitwa huku🤓
 
Kuna kamtindo nakaona kwa ma broo wanaomiliki ndinga . Kuning'iniza funguo za gari kiunoni naona kama kaushamba hivi kujionyesha nae yuko kwenye 'list' ya wanaopush ndinga. Most of thema kama wanaiga vile. NB: Mimi similiki gari . Labda na wivu.
Hako kamtindo wajanja mavi huku kwetu wameshakaboresha zaidi, akiokota ufunguo wa aina yoyote aning'iniza kiunoni, kata kucha kiunoni, ka kisu kadogo kiunoni, filimbi kiunoni n.k
 
Kuna kamtindo nakaona kwa ma broo wanaomiliki ndinga . Kuning'iniza funguo za gari kiunoni naona kama kaushamba hivi kujionyesha nae yuko kwenye 'list' ya wanaopush ndinga. Most of thema kama wanaiga vile. NB: Mimi similiki gari . Labda na wivu.
Hahahha wengine ni kawaida tu bhana. Funguo zenyewe ukiweka mfukoni zinavunja simu😂😂.
Hii hata wazee wananing’iniza funguo za nyumba.
 
 
Huu uzi utapendwa sana na vijana wa mikoani. Anyway kuna ukweli ndani yake. Na wengi wanapotoka vijijini ndio waathirika wakubwa wa kuigiza haya maisha na maigizo ya wasanii wa muziki na maigizo ya kwenye tv.
 
Kuwa mjanja(Smart) ni neno linalotumiwa vibaya sana na vijana wa mijini.
 
Hayo mengi utayakuta vijiwe vya bodaboda.
Kama usipojichetua kidogo basi huwezi kupiga nao story.
 
Upo sahihi
Lakini mtu hata kama hakuju kama najaribu jamii au maadili lazima umchukie kama upo timamu kiakili
Kuna Sheria.
Sheria zikifuatwa, inatosha. Hayo maadili ni uchaguzi wa mtu. Kuna maadili ya kidini, kabila, chama au ushirika Fulani eg. Freemasons, Yakuza, triads etc...
Kuna maadili mengi duniani na kila mtu atafuata yake.
Waacheni watu wawe huru kufanya wanayotaka, hayo siyo maisha yako, ni yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…