Ukifuatilia kile kinachoitwa ujanja wa mjini ndio ushamba wenyewe

Ukifuatilia kile kinachoitwa ujanja wa mjini ndio ushamba wenyewe

Hii ipo duniani kote. Hata uvaaji. Huwezi kuta mtu mjanja amevaa mrolex. Utakuta kajificha huko kwenye Vacheron Constantin. Huwezi kuta anashabikia trend za mziki wa mjini, anajua yeye nini kinamfurahisha na anafuata hicho. Ni kweli watu wengi wa mjini ni washamba sana, bahati mbaya watu wengi wa nje ya mji huiga hao wa mjini.
 
Hii ipo duniani kote. Hata uvaaji. Huwezi kuta mtu mjanja amevaa mrolex. Utakuta kajificha huko kwenye Vacheron Constantin. Huwezi kuta anashabikia trend za mziki wa mjini, anajua yeye nini kinamfurahisha na anafuata hicho. Ni kweli watu wengi wa mjini ni washamba sana, bahati mbaya watu wengi wa nje ya mji huiga hao wa mjini.
Watu wa mjini siyo washamba.
Watu wa "Shamba" ndiyo washamba. na kuwa mshamba siyo jambo baya, ni kwamba tu unakuwa ni mtu uliyekulia kijijini au kwenye miji midogo.
Watoto wa mjini maisha yao tangu utotoni ni ya kizungu i.e "Westernized". Kwa mfano, Wema Sepetu ni mtoto wa mjini na Bint kigoma siyo mtoto wa mjini.
Au Vunja Bei na Joseph Kusaga wote wana visu ila mmoja ni mtoto wa mjini na mwingine siyo mtoto wa mjini.
 
Kuna Sheria.
Sheria zikifuatwa, inatosha. Hayo maadili ni uchaguzi wa mtu. Kuna maadili ya kidini, kabila, chama au ushirika Fulani eg. Freemasons, Yakuza, triads etc...
Kuna maadili mengi duniani na kila mtu atafuata yake.
Waacheni watu wawe huru kufanya wanayotaka, hayo siyo maisha yako, ni yake.

Hatuzungumzii Duniani. Nazungumzia Tanzania.
Yote niliyoyataja sio maadili kwa hapa Tanzania.
Labda kama wewe ni mzungu au muarabu pori. Yaani baba mzungu, mama mswahili unahaki ya kusema hayo
 
Hatuzungumzii Duniani. Nazungumzia Tanzania.
Yote niliyoyataja sio maadili kwa hapa Tanzania.
Labda kama wewe ni mzungu au muarabu pori. Yaani baba mzungu, mama mswahili unahaki ya kusema hayo
Mimi ni mluguru na nina maadili tofauti na mmasai au mmakonde.
Pia ni mlutheri na nina maadili tofauti na muislam. Mwanamke akivaa mini-skirt, au akivaa baibui na kufunika uso wake kwangu mimi ni sawa tu.
Au labda nipo Nungwi na wanawake kule wanatmbea na thongs, kwangu mimi sawa tu wala sishtuki.
hakuna maadili ya kitanzania, kuna sheria za Tanzania. tuache kuishi primitively na ku-judge watu eti waishi kama mnavyotaka.
Taifa huru huendelea, na mojawapo ya sifa za jamii huru ni tolerance. Mataifa yasiyo huru huwa hayaendelei and their life sucks.
 
Hapo kwenye utapeli na kujisifu uzinzi waga nashangaa hata mimi.. (hayo mengine ni hobbies za mtu)
Ila haya mambo mara nyingi yanafanywaga na wakuja.
Wenyeji wanatuchora tu tunavyokuja na afya zetu nzuri, tukitajirika na kurudishwa makwetu na kilo 2
 
Tatizo linaanza kwenye jamii kama mimi nipo interested na wasanii, ngono na ulevi lakini jamii iliyonizunguka inanitafsiri kama mjanja.

Jamii hiyohiyo inamuona mshamba kijana ambaye sio mlevi anayevaa suruali za vitambaa na mashati ya kuchomekea aliyeokoka ambaye ana mke na watoto wake.

Tatizo lipo kwenye jamii.
 
UKIFUATILIA KILE KINACHOITWA UJANJA WA MJINI NDIO USHAMBA WENYEWE

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli

Hakuna Watu Washamba na wajinga kama vijana wa mjini wale wanaojiita na kujiona wajanja. Ninawaita Washamba na wajinga kwa sababu ya mambo wanayoyafanya na yale wanaojivunia nayo.

Taikon ni mtu wa kwenda kwa hoja, nitatoa mifano iliyodhahiri kuonyesha ni namna gani wale wanaojiita wajanja wa mjini wengi wao ni Washamba na limbukeni.
Mifano hiyo ni pamoja na mambo yafuatayo;

1. Mtu ni mshamba yeyote huiga Wasanii na Watu wa burudani. Yaani Role model wa Watu Washamba ni Wasanii au wanamuziki.
Moja ya dalili kuwa wewe ni mshamba na unaakili ndogo sana ni kuchukulia mno ya entertainment kama ndio maisha halisi.
Watu smart na classic huwezi kuwakuta wanawachukulia serious wasanii na Watu wa burudani.
Ukijiona wewe sio msanii lakini unapenda kuishi kama wasanii ujue wewe ni mshamba na unaupeo mdogo mno.

Kwamba Msanii kavaa hivi na wewe unafanya hivyo. Vijana wa mjini hufuata mitindo ya maisha ya wasanii na Watu wa entertainment. Hiyo ni sehemu ya ushamba. Kama utafuatilia vizuri Wanamuziki wengi hasa wa huku Afrika wenyewe kama wenyewe wengi wao ni Washamba na wanaupeo mdogo sio ajabu hata mambo wanayoyafanya ni yakitoto na ku- entertain ujingaujinga.

2. Watu Washamba wanatabia ya Bendera fuata upepo kwa Sababu hawana upeo mkubwa wa Akili.
Vijana wa mjini ukiwafuatilia ni bendera fuata upepo tena upepo wa wenye upeo mdogo.
Ukija mtindo wa kata K watakata K wote. Ukija mtindo wa kutoboa masikio watatoboa maskio. Ukija mtindo wa Kupaka Bleach watapaka bleach. Ukija mtindo wa kuvaa vipenzi vifupi vya kuonyesha mapaja watavaa. Ukija mtindo wa kuchora tattoo. Wanachora.

Washamba na limbukeni ni Watu wa kufuata Mkumbo. Hawana ubunifu. Tena bora waige vitu vya maana. Hawawezi kuiga vitu vya maana kwa sababu vitu vya maana vinahusisha akili kubwa ambayo hawana, au vinahusisha kutumia matumizi makubwa ya akili jambo ambalo hawataki kutumia akili kubwa.

Ni rahisi kuharibika mjini kwa sababu ndio kuna kundi kubwa la wajinga na washamba.
Wao kujaribu jaribu kila kitu ndio ujanja.
Ikitoka Kuberi wapo.
Ikitoka Shisha wapo.

3. Kujisifia Upumbavu na Uovu.
Ukitaka kujua mtu ni mshamba au Dishi lake halisomi ni katika yale anayojivunia.
Unakakuta kakijana kwa ulemavu wake wa akili kanajisifu mambo ya ajabuajabu.
Mara kutoka na Wake za Watu alafu hadharani, halijioni kuwa linajitia aibu kwa sababu upeo mdogo.
Mara mimi Mademu wananikubali alafu ukicheki ni kijana anayetakiwa kuwa na mke na watoto. Lakini kwa vile ni mshamba haoni hilo.

Wewe kutoka na wanawake wengi huoni kama huo ni ushamba na matatizo ya akili? Huoni kama unahatarisha maisha yako kama Nyumbu. Tena nyumbu anaakili. Huoni kama unaharibu jamii. Huoni kwa sababu wewe ni mshamba.

Vijana Classic na Standard wanamiiko, wanakinyaà, wanajiheshimu, Viumbe wote unaowajua ni wajanja ni wasafi na wanamiiko mikali.

Vijana wengi wa mjini wao huona ni ujanja ati kumtapeli mtu. Yaani wewe kumuibia mtu unaita ujanja wakati hiyo ni dalili kuwa wazazi wako walifeli kukulea vizuri. Yaani unawatia aibu Wazazi wako na wewe mwenyewe alafu unajiita mjanja.
Unakuta vijana kazi zao ni kuibia vijana au Watu masokoni, Kariakoo, au ishu zingine alafu unajiona mjanja.

Unavunja màadili unajiona mjanja kama sio unamatatizo ya Akili.

Ukifuatilia hata kwenye vyombo ya habari hasa vile vya burudani na mitandao ya kijamii utagundua wale wenye matatizo ya akili wanapofanya mambo ambayo sio ya kawaida yanayovunja maadili ndio huita ujanja.

Unakuta kabinti kanatembea uchi, utupu wake unaonekana kabisa lakini kwa vile kanaumwa magonjwa mabaya ya kisaikolojia, kanajiona ni kajanja.

Huwezi kuwa na tabia chafu ukawa mjanja mbuzi wewe.

Unakuta kijana kazi kujisifia ujinga tuu. Mimi mtoto wa mjini, mimi mtoto wa mjini. Mimi mjanja. Lakini ukifuatilia kile anachojivunia utagundua anatatizo kubwa la kisaikolojia.

Dini huna
Akili Huna basi uwe hata na kielimu cha kuzugia na hauna.
Elimu huna basi uwe hata na kaujuzi. Nako hauna.
Pesa na mali Huna
Maadili Huna
Mahusiano thabiti na familia Huna.
Huo ujanja unaojivunia hasa ni upi? Kama sio unamatatizo wewe?

Kwa hiyo ujanja wako ni kutoboa pua yako?
Ujanja wako ni kuimba nyimbo za Diamond na Ali Kiba?
Ujanja wako ni kujua maisha ya Watu wengine, udaku?
Ujanja wako ni kuelezea na kubisha na simba na Yanga sio?
Ujanja wako ni kujua majina ya vilevi na kuvichanganya?[emoji23]
Ujanja wako ni kujua kucheza kama Chino Wana? Ili ujue unaakili za kitoto.[emoji2]
Ujanja wako ni kuweka nywele mitindo mbalimbali alafu bado ukiambiwa unaakili ndogo unasema unaonewa. Hata kijana wa kidato cha Kwanza mwenye akili hawezi kufikiria jambo hilo.

Au ujanja wako ni kujua mitaa na kona za jiji. Na wamiliki wa majengo ya jiji wakati wewe hata kwako huna?
Unakuta kakijana utasikia, lile jengo ni la fulani. Alinunua kwa fulani kwa mkopo. Alafu unajua kamhonga fulani. Hivi unaakili sawasawa kweli.

Au ujanja wako ni kwenda Beach kidimbwi au kitambaa cheupe?

Siwezi kukuambia uache huo ushamba kwa sababu tatizo hilo limeanzia akilini.
Upeo mdogo ndio tatizo lako lililosababisha wewe kuwa mshamba.

Acha Nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
hii imeenda na imeeenda! umepiga penyewe [emoji109]
 
Jitahidi sana katika maisha yako usikerwe na mtu ambaye hata hakujui.
Kama mtu hakujui, halafu anakukera na unamchukia basi ujue wewe ni mwanadamu mwenye utashi mdogo sana, unakaribia na sokwe (ingawa utamzidi kidogo sana).
ni sawa.. ni km vile wewe ulivyo kerwa na bandiko la mtu ambae nadhani hata hakujui na unamchukia basi ujuwe ww ni banaadamu mwenye utashi mdg.sana...
 
Back
Top Bottom