Ukifuatilia kile kinachoitwa ujanja wa mjini ndio ushamba wenyewe

Hii ipo duniani kote. Hata uvaaji. Huwezi kuta mtu mjanja amevaa mrolex. Utakuta kajificha huko kwenye Vacheron Constantin. Huwezi kuta anashabikia trend za mziki wa mjini, anajua yeye nini kinamfurahisha na anafuata hicho. Ni kweli watu wengi wa mjini ni washamba sana, bahati mbaya watu wengi wa nje ya mji huiga hao wa mjini.
 
Watu wa mjini siyo washamba.
Watu wa "Shamba" ndiyo washamba. na kuwa mshamba siyo jambo baya, ni kwamba tu unakuwa ni mtu uliyekulia kijijini au kwenye miji midogo.
Watoto wa mjini maisha yao tangu utotoni ni ya kizungu i.e "Westernized". Kwa mfano, Wema Sepetu ni mtoto wa mjini na Bint kigoma siyo mtoto wa mjini.
Au Vunja Bei na Joseph Kusaga wote wana visu ila mmoja ni mtoto wa mjini na mwingine siyo mtoto wa mjini.
 

Hatuzungumzii Duniani. Nazungumzia Tanzania.
Yote niliyoyataja sio maadili kwa hapa Tanzania.
Labda kama wewe ni mzungu au muarabu pori. Yaani baba mzungu, mama mswahili unahaki ya kusema hayo
 
Hatuzungumzii Duniani. Nazungumzia Tanzania.
Yote niliyoyataja sio maadili kwa hapa Tanzania.
Labda kama wewe ni mzungu au muarabu pori. Yaani baba mzungu, mama mswahili unahaki ya kusema hayo
Mimi ni mluguru na nina maadili tofauti na mmasai au mmakonde.
Pia ni mlutheri na nina maadili tofauti na muislam. Mwanamke akivaa mini-skirt, au akivaa baibui na kufunika uso wake kwangu mimi ni sawa tu.
Au labda nipo Nungwi na wanawake kule wanatmbea na thongs, kwangu mimi sawa tu wala sishtuki.
hakuna maadili ya kitanzania, kuna sheria za Tanzania. tuache kuishi primitively na ku-judge watu eti waishi kama mnavyotaka.
Taifa huru huendelea, na mojawapo ya sifa za jamii huru ni tolerance. Mataifa yasiyo huru huwa hayaendelei and their life sucks.
 
Hapo kwenye utapeli na kujisifu uzinzi waga nashangaa hata mimi.. (hayo mengine ni hobbies za mtu)
Ila haya mambo mara nyingi yanafanywaga na wakuja.
Wenyeji wanatuchora tu tunavyokuja na afya zetu nzuri, tukitajirika na kurudishwa makwetu na kilo 2
 
Tatizo linaanza kwenye jamii kama mimi nipo interested na wasanii, ngono na ulevi lakini jamii iliyonizunguka inanitafsiri kama mjanja.

Jamii hiyohiyo inamuona mshamba kijana ambaye sio mlevi anayevaa suruali za vitambaa na mashati ya kuchomekea aliyeokoka ambaye ana mke na watoto wake.

Tatizo lipo kwenye jamii.
 
hii imeenda na imeeenda! umepiga penyewe [emoji109]
 
Jitahidi sana katika maisha yako usikerwe na mtu ambaye hata hakujui.
Kama mtu hakujui, halafu anakukera na unamchukia basi ujue wewe ni mwanadamu mwenye utashi mdogo sana, unakaribia na sokwe (ingawa utamzidi kidogo sana).
ni sawa.. ni km vile wewe ulivyo kerwa na bandiko la mtu ambae nadhani hata hakujui na unamchukia basi ujuwe ww ni banaadamu mwenye utashi mdg.sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…