Ukighadhibishwa unafanyaje kupunguza hasira yako?

Ukighadhibishwa unafanyaje kupunguza hasira yako?

Kwa mfano nikikerwa suluhu yangu ni kujifungia ndani na kujumlisha changamoto na magumu yote niliyopitia katika maisha yangu niliee weee mpaka moyo usuzike baada ya hapo nitakavyoanza kucheka na kufurahi na mwenzangu ni kama si yeye aliyenikwaza,ila kama sijafanya ivo ujue siku hiyo nimeamua kutema cheche mdomoni mpaka mhusika haja ndogo imbane ghafla.
Kwa upande wake yeye nikimkera anaondoka kwenda zurura huko arudi baadaee,na asipoondoka utasikia kilio cha mbwa huko nje...yaan anamtafutia kosa mbwa wangu apate kumbutua tu.Je wenzangu mkikerwa na wapenzi wenu huwa mnamaliza vp?
JamiiForums1839417146.jpg
 
Nachukua mswaki wake, naenda kusugulia sink la choo mpaka hasira ziishe afu natulia kmyaaaa as nothing happened.
 
Nachukua mswaki wake, naenda kusugulia sink la choo mpaka hasira ziishe afu natulia kmyaaaa as nothing happened.
Aisee,bora unipige tu nitajiuguza
 
Inategemea na mtu aliniuzi ni nan kwangu.
nakaa mbali nae had akili iwe sawa baadae maisha yanaendelea kama kawaida nitamwambia siku nyingne kuwa aliniuzi.
Au ninatafta mtu ninae mpenda namuomba kuonana nae tunapiga story had nakuwa sawa
 
Back
Top Bottom