Ukigombana na Mkeo, akaenda kwao; USIENDE wala Usimtafute

Kwa huu uandishi hakuna aliepo kwenye ndoa kwa miaka 16....na Kama kweli Basi wanao wamedoda nyumbani na umeanza safari ya malezi upya [emoji38][emoji38]
Sawa
 
Funniest thing about wanawake wote wanaamini ni wazuri na wana uwezo wa kumtetemesha mtu yoyote ,kwa ulichoandika utaoa utaoa utaoa na hadi uzeeke utakuwa tyl n shahidi na mm "kutokuwa mjinga co kutokukubali kufanywa mjinga"
 
Inategemea na coincidence ya tukio na watoto nyumbani otherwise kitu ambacho siwezi kufanya ni kupiga magoti kumvisha pete, kupiga magoti kumuomba msamaha au kumuomba msamaha wife kwa ujumla wake nitazungumza maneno yore ila sio neno samahani
Neno samahani au nisamehe ni dawa na tiba kwenye mahusiano yote hapa duniani..Muungwana akikosea uomba samahani..kama unapeleka zawadi mbadala wa msamaha hiyo ni rushwa tu kumpumbaza mtu huyo asione kosa lako..
 
Funniest thing about wanawake wote wanaamini ni wazuri na wana uwezo wa kumtetemesha mtu yoyote ,kwa ulichoandika utaoa utaoa utaoa na hadi uzeeke utakuwa tyl n shahidi na mm "kutokuwa mjinga co kutokukubali kufanywa mjinga"

Mwanaume haoni shida kuoa hata mara elfu ikiwa ni Kwa sababu ya kulinda heshima yake
 
Ukiacha hiki kipengele cha FiDIA, naunga mkono mengine yote uliyoandika😊
 
Maisha yangu yote nilikataa Habar ya kutawaliwa na mtu anaeitwa mwanaume, napenda twende sawa hutaki pita na mia,
Kwani nini bwana weee
 
Hili bandiko lako umeongea na idadi chache sana ya wanaume, ni kama vile umewapa semina, lakini ukweli ni kuwa kizazi hiki wanaume wa hivyo ni wachache. Unaoongea nao hapa ilitakiwa kile kizazi cha ukoloni ambapo mwanaume ananyanyuka anaenda kupigania taifa bila uoga,,hawa wa siku hizi chama kimoja tu wameshindwa kukitoa madarakani hata. Kwa mapanga wamebaki kulala mitandaoni
Eeh mwanaume ambae hata mke mmoja au wawili walikuwa hawatoshi hadi mke anaomba pooo kwa hiyo inabidi mume kufanya ndoa za mitala,

Unaita hawa wavaa suruali wanaume wakati ndani mwanamke analia hatoshelezwi kizazi cha mitala kwa wanawake fyuuu,

Mwanaume wa sasa hata kikombe cha chai hamalizi wakati enzi hizo mwanaume ndo ya lita 20 ya unga siku mbili Imeisha.
 
Usiwadanganye wenzieo ohooo wengi wepesi wa kushauri wao hawafanyi hivyo
 
😍
 
Usiwadanganye wenzieo ohooo wengi wepesi wa kushauri wao hawafanyi hivyo

Mimi nawapa Tu dondoo chache za kuwafunza adabu wanawake wasiofunzwa na wazazi wao.

Masomo yangu nayatoaga Kwa watu wote lakini lengo yashikwe na watu wachache tuu.

Furaha ni yawatu wachache siku zote
 


🤣🤣🤣

Na hapa nazungumza na wanaume haswa ambao ni wachache Mno.

Kumbuka sifa kuu ya mwanaume ni AKILI, hekima, na nguvu, kisha MSIMAMO.

Sio rahisi Kwa mwanamke akikikutana na Mwanaume halisi kuleta upumbavu, hakuna mwanamke atakayekubali kumpoteza mwanaume mwenye sifa nilizozitaja.

Wanawake wa siku hizi wanaona rahisi kuachana na wala hawaoni tatizo Kwa sababu ya madhaifu ya kimsingi ya Vijana wa siku hizi.
Mwanamke ataumia kidogo alafu atasahau lakini kama angekutana na Mwanaume halisi, mwanamke kamwe hawezi kubali kuachwa alafu ati mwanamke mwingine achukue nafasi yake ajipatie furaha kwa huyo mwanaume aliyemuacha.

Siku hizi wanaume ndio wanateseka kwenye mahusiano kutokana na kupoteza Ile sifa ya Uanaume.
 
Hiyo heshima inapelekwa wap?

Heshima ya mwanaume ndio maisha yake na Ulinzi wake.

Ni Kama Mwanamke Naye anaheshima yake ambayo ni Ulinzi wake.
Mwanamke lazima alinde Utu wake Kwa kutofanya umalaya na kufunuliwa funuliwa na kila mwanaume.

Heshima ya mwanamke ukiipoteza jua umekwisha,
Kila mtu atakudharau hata wewe mwenyewe utajidharau.
Watoto utawatia uchungu na kukuona hufai kuwa mama Yao.

Ndio maana mwanamke haswa, mwanamke anayejua thamani yake kamwe hawezi kujirahisisha Kwa kutoa penzi kiholela, ni aibu Kwake na Kwa wanaomzunguka
 
Hapo umeeleweka, kiufupi ni kuwa wanaume halisi wanazidi kuisha
 
Maisha yangu yote nilikataa Habar ya kutawaliwa na mtu anaeitwa mwanaume, napenda twende sawa hutaki pita na mia,
Kwani nini bwana weee


Ukitaka ujue athari yake, njoo pm nitakueleza kinagaubaga.

Kutawaliwa na Mwanaume ndio nature ilivyo. Utake usitake.
Sema lazima ujiulize anayekutawala ni mwanaume wa dizaini gani maana wanaume hawalingani mama mlivyo Wanawake.

Mtu anaweza kuwa Mwanaume lakini ukawa umemzidi akili na hekima, huyo hawezi kukutawala. Lakini haimaanishi usitafute mwanaume wa kukutawala mwenye vigezo unavyovitaka.

Dini zote kubwa, na hata tamaduni karibia zote Duniani zinakutaka uwe chini ya utawala wa mwanaume. Hilo sio ombi ni Lazima.

Biblia inasema hivyo, Quran nayo ni vivyo hivyo, na hata Mila zetu zinasema hivyo.
Labda wewe unambie ni kabila gani

Kutokutaka kutawaliwa ni ishara ya kiburi na jeuri Kwa nature uliyotwaliwa kwayo.
Na kikawaida nature inatabia ya kukuadhibu ukienda kinyume nayo.

Kusema huwezi kutawaliwa na Mwanaume ni Dalili kuwa umeshindwa kutambua na kuona Wanaume wenye sifa za kukutawala ambao ninauhakika wapo.

Mwisho: Usipende kushindana na nature, itakugharimu pakubwa, mbaya zaidi itagusa na watoto wako pia.
Nina ushahidi katika hili

Njoo pm nitakueleza Jambo muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…