Ukigombana na Mkeo, akaenda kwao; USIENDE wala Usimtafute

Mkuu samahani kwa heshima kabisa nikuambie kuwa uliyoandika ni fasihi andishi. Mtu anaitwa Mke ni habari nyingine tofauti kabisa.

Mwanaume atakayefuata wazo lako kuna mambo matatu yatampata:
1. Sonona
Heshima ya Magu ni zaidi ya Nyerere am telling you
 
Sio kila mwanamke kazaliwa kutawaliwa na mwanaume, na sio kila mwanaume kazaliwa kutawala mwanamke.
Sometimes nature inabadilika.

Ndo mana unaona hadi siku hizi viongozi wa juu nchi/duniani ni wanawake pia tofauti na zamani ambapo mwanaume alikuwa mtawala kwa kila kitu.

Mwanamke alikuwa ni mtu wa kuumia na kutawaliwa tu lakin kizazi cha sasa kimekataa.
 

Nature haibadiliki Mkuu. Kila kitu kipo Kama kilivyo.

Mwanamke ambaye hajaumbwa kutawaliwa ni Wale walioumbwa kuwa kama chombo cha STAREHE Kwa wanaume wengi. Wengi huitwa Malaya au Makahaba.

Hakuna mwanamke yeyote Duniani ambaye atakuwa na heshima Kama asipokuwa chini ya MWANAUME.

Kuhusu viongozi,
Mwanamke anaweza kuwa kwenye kiti cha utawala Kama Urais au Umalkia lakini kamwe hawezi kuongoza yeye Kama yeye pasipo wanaume kuwa nyuma yake.

Lakini wanaume ni watawala hata pasipo kuwa na wanawake nyuma Yao.

Mwanamke alikuwa ni mtu wa kuumia kutokana na ujinga wao na ujinga wa jamii Kwa kushindwa kuchagua mwanaume wa kumtawala.

Kuchagua Mtawala inahitaji hekima kubwa Sana.

Hata sasa hivi wanawake wanateseka na wataendelea kuteseka Kwa sababu wengi hufikiri kila mwanaume anauwezo WA kuwaoa/kuwatawala. Jambo ambalo sio Kweli.

Mwanamke pasipo Mtawala ni Sawa na Mwanadamu pasipo na Mungu.

Ni Sawa na mwanadamu aseme hataki kutawaliwa na Mungu Jambo ambalo haliwezekaniki.
Labda mwanadamu achague mungu wa kumtawala lakini sio kusema hawezi kutawaliwa na MUNGU.

Ndivyo nature ilivyo.
 
Hamna mahali ambapo nimesema sijaolewa.
Ubabe Ubabe ndo sipendagi,
Heshima utapata lakini Ubabe wako tupa kule

Mwanaume mbabe ni Yule asiyetumia akili na hekima.

Ubabe ni mtamu ukimpata mwanaume halisi, ambaye anautumia ubabe Kama Pilipili kwenye nyama choma au Dagaa Rosti na ugali.

Ubabe ni Kama Pilipili kwenye mboga, isizidi wala isipungue
Ubabe lazima utumike Kwa Asilimia 10% Ila akili na hekima 90%.

Mwanaume bila kaubabe anapoteza sifa ya kuwa Mwanaume na anapoteza ule uromantiki Kama dume.

Wanawake hupenda Kupendwa na kudekezwa,
Hupenda kusikilizwa lakini sio kusikilizwa Kwa kila kitu.

Wanawake ni viumbe WANAOPENDA kuishi Kwa kumtega mwanaume kuona atafanyaje, na sio kosa kwani ni kawaida Yao kumpima mwanaume anaakili kiasi gani, au hekima kiasi gani ya kuamua Jambo.

Wanawake anaweza kufanya Jambo Fulani akijua ni Baya ili tuu akuone utamkaripia au kutumia ubabe kumkataza, usipomkaripia na kumletea ubabe atakuona humpendi πŸ˜€πŸ˜€.
Ukimletea ubabe atanuna Kwa muda huku akijua yeye ndiye kakosea mwishowe atataka umbembeleze😊😊.

Ukimbembeleza, utakuwa umefaulu mtihani wake.

Kuleta ubabe wakati mwingine Kwa mwanamke ni ishara ya kumjali na kumpenda.

Ubabe ambao Wanawake hawaupendi ni ule yeye yupo sahihi alafu mwanaume kakosea lakini mwanaume anakomalia msimamo wake licha ya kuwa amekosea. Hapo ndipo wanaume wengi wanapopishana na wake zao.

Ndio maana niliandika, mwanaume ni AKILI. Nikasema kabla hujaoa jifunze kuwa na Akili, na kabla hujawa Baba jifunze kuwa Mtawala
 
Neno samahani au nisamehe ni dawa na tiba kwenye mahusiano yote hapa duniani..Muungwana akikosea uomba samahani..kama unapeleka zawadi mbadala wa msamaha hiyo ni rushwa tu kumpumbaza mtu huyo asione kosa lako..
Asante kwa mtizamo wako mkuu

Ndio maana ya mitizamo yenyeweπŸ™
 
Usije washauri wenzako hivi ww hitendi kwa kweli usipo tenda ulaaniwe
 
Hamna mahali ambapo nimesema sijaolewa.
Ubabe Ubabe ndo sipendagi,
Heshima utapata lakini Ubabe wako tupa kule
Lakini ukweli ni kwamba hujaolewa madam[emoji2957][emoji2957]
 
Tema madini wakuelewe hawa
 
Uko sahihi kabisa Robert Hariel
 
Mwanaume aliyelishwa madawa ndio anaweza kwenda kinyume na maelekezo yako mkuu
 
Mkuu nakubaliana nawe kwenye hili
 
Mbona kama unatumia Njia ngumu ku-solve matatizo madogo.

Unatumia kila Njia kulinda heshima Yako bila kujali hisia za wengine huo ni ubinafsi
Unarudi kule kule. Tofauti ya kufanya maamuzi kwa kutumia hisia na kutumia akili.

Tumefika hapa kwasababu tuliruhusu kutumia hisia badala ya akili.
 
Na mwanamke akishapata kijihela

Kazi nzuri mshahara nzuri,uchumi kwake mzuri

Mwanaume hesabu maumivu

Na ukishamuwezesha mwanamke imekula kwako

Ova
Maumivu yatakuja kama utaruhusu atumie mamlaka yako kufanya maamuzi magumu. Unatakiwa kama mwanaume unayejitambua mwanamke kuwa na kipato isiwe ajenda muhimu kwako maana hata wenyewe ndani ya nafsi zao wanajua hawapotayari kutumia pesa zao kama vile sisi wanaume tunavyotumia zetu.

Bali wanachotakiwa kujua ni kwamba mwanaume anabakia kuwa mwanaume na mwanamke anabakia kuwa mwanamke period. Hizo discussion zingine za usawa ni irrelevant na hazina mashiko hata kidogo.
 
Nakazia.
Kama umeongelea kabisa kisa cha jamaa angu mmoja,
Yy alikuw anamfata mkewe kwa mamamdogo wake alipokuw anakimbilia,
Akifika huko anajiliza kibwebwege mke anarudi,
Sasa hivi ni kama mke kamuacha kbs.
Kati ya makosa tunayofanyaga wanaume ndo hayo....mwanamke ukimfata ndo anakufanyia desturi na unadharaulika,akitishia kuondoka mpe na nauli kabisa na unakaa kimya....badae utanishukuru..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…