MKIGOMBANA NA MKEO, AKAENDA KWAO, USIMFUATE WALA USIMTAFUTE
Anaandika Robert Heriel.
Kabla hujaoa jifunze kuwa Mwanaume. Niliwahi sema, mwanaume ni AKILI.
Kabla hujawa Baba jifunze kuwa Mtawala.
Na ili uwe Mtawala yakupasa uwe na hekima na busara. Pia uwe na maamuzi yasiyo yumba(uwe na msimamo).
Kitu kikubwa Kwa Baba ni Heshima, mwanaume Bora hulinda heshima yake kuliko kitu chochote. Yupo tayari kupoteza vyote lakini sio kupoteza heshima yake Kama Baba. Ndio maana Baba bora ni rahisi kufukuza mke na watoto pale anapoona heshima yake IPO hatarini.
Mwanaume anayepuuza heshima yake na kujali vitu vingine anapoteza sifa ya kuitwa Baba.
Mwanaume aliyeiva kamwe hawezi sumbuliwa na Mwanamke. Mwanaume ili asumbuliwe na mwanamke na hapa nazungumzia mke wake sharti aongozwe zaidi na Hisia pasipo Akili. Na siku zote mwanaume anayeongozwa na Hisia huyo sio mwanaume halisi.
Kama nilivyosema hapo juu. Mwanaume ni AKILI. Sio ajabu kwenye maandiko waliposema ishini na wake Kwa Akili.
Tafsiri yake ni kuwa pasipo akili heshima ya mwanaume ipo mashakani.
Baba ni jina kubwa. Baba hakosei. Na hapa namaanisha Baba aliyejifunza kuwa Mtawala.
Ikiwa Baba hakosei, tafsiri yake Baba haombi Msamaha.
Baba kuomba msamaha tafsiri yake hajielewi, hakujua alichokuwa anakifanya, Baba sharti awe na msimamo hata Kama wengine watamuona anakosea. Huyo ni Baba. Baba hapaswi kuwa kigeugeu.
Ikiwa mwanamke ambaye ataitwa/utamuita Mkeo mkakosana, iwe Kwa sababu yoyote Ile, iwe wewe ndiye chanzo cha ugomvi au yeye ndiye chanzo cha ugomvi. Akaondoka kukimbia kwenda kwao pasipo wewe kumfukuza,
Akaenda kwao wakamlaki Kwa sababu ni mtoto wao, wakijua walimuozesha kwako,lakini wakampokea,
Kamwe usijeenda kumchukua, wala USIMTAFUTE, wala usitake Suluhu naye.
Mwanamke kuondoka nyumbani pasipo iidhini ya Mumewe ni kosa tosha la kumfukuzisha kwenye nyumba yako, isipokuwa Kwa sababu zinazohatarisha usalama wake kama kupigwa na mumewe ikiwa ni Wale wanaume vichwa maji. Na hapa kupigwa namaanisha kupigwa haswa sio Yale makofi mawili matatu ya kuonywa.
Mwanamke anapokimbilia kwao na akapokelewa na wewe ukaenda kumchukua ni dalili kuwa utawala wako umepinduliwa na sasa wewe hauko utawalani.
Mwanamke kama itatokea akaona sababu ya kukimbia nyumbani kwako basi itampasa akimbilie kwenu, yaani Kwa Mama yako au Baba yako(akimbilie ukweni).
Hiyo ndio Heshima.
Na ndio maana ya wewe kuoa na kumuita huyo ni Mkeo. Lakini sio jitu umelioa likufanyie mapinduzi, ati uende ukalichukue kwao, hiyo kamwe haiwezi fanywa na Mwanaume aliyefunzwa akawa Mtawala Kama ilivyosilika ya mwanaume.
Mwanaume haweziitwa kikao ukweni akaenda, isipokuwa ukweni wanauwezo wa kuwasiliana na Familia ya Mkwe wao(mwanaume aliyeoa binti Yao), kisha wazazi wa mwanaume waitishe kikao, kisha upande wa kiukeni ualikwe Kama wageni na watoe malalamiko Yao.
Wanawake wengi ukienda kuwachukua kwao, hugeuka Mateso kwako hapo baadaye, huwa wajeuri, lazima wakupelekeshe kwani wanajua kabisa kuwa huwezi ishi pasipo wao.
Nimeshuhudia haya Kwa sehemu kubwa, nimejionea Kwa macho yangu na kuyafanyia tathmini hivyo maneno yangu yamepimwa yakathibitika.
Jifunze kukaza roho kabla ya kuitwa Baba. Jifunze kufanya maamuzi magumu kabla ya kuitwa Mume. Baba ni Cheo ambacho anastahili mtu mwenye maamuzi magumu. Ubaba Kwa sehemu hauhitaji kuwa na huruma hata kidogo.
Baba hasikilizi yeyote isipokuwa akili yake na namna ya kulinda heshima yake. Hakuna cha serikali, hakuna cha mchungaji sijui Sheikhe, hakuna cha wazazi. Linapokuja suala la heshima yako kama Mwanaume usimsikilize yeyote Yule.
Usihudhurie vikao ambavyo havina msingi wowote.
Mpaka wanakuozesha binti Yao waliridhishwa na kuwa wewe ndiye utakayemsimamia na kumhudumia mtoto wao.
Kama nitakupa binti yangu akaleta upuuzi wa kukimbia, Kwanza sitampokea, lakini kama atapata njia mbadala ya kwenda Kwa watu wengine. Fukuza na nitakupongeza na kukuona wewe ulistahili kumuoa mwanangu.
Lakini binti nimekupa alafu kakukimbia alafu unaleta pua yako kwangu, hakika nitakutoa nduki na panga mchana kweupe.
[emoji122][emoji122][emoji122]