Ukigombana na Mkeo, akaenda kwao; USIENDE wala Usimtafute

Ukigombana na Mkeo, akaenda kwao; USIENDE wala Usimtafute

Ukiona mwanaume anam chase mwanamke jua tu kuwa mwanamke ni potential sana kwa mustakabali wake.

Aidha ana akili za kimaisha sana na ana upepo wa pesa ama anamiliki mali nyingi zaidi ya mume ikiwemo nyumba mnayoishi![emoji23] Unakuta mafanikio mliyo nayo ame play part kubwa lazma kidume alegeze masharti.

Kwahio hili bandiko ni kwa wanaume wa shoka ambao wamehodhi mali kwa jasho lao! Akina Marioo huwa wanafukuzwaga na mabegi tu so lazima wajikombeleze
Huyo hatoshi kuitwa Mwanamume Bali ni mwanauume. Pili kaolewa na hastahili kuitwa Baba. Umesema anaitwa Mario sio Baba.
 
Mkuu samahani kwa heshima kabisa nikuambie kuwa uliyoandika ni fasihi andishi. Mtu anaitwa Mke ni habari nyingine tofauti kabisa.

Mwanaume atakayefuata wazo lako kuna mambo matatu yatampata:
1. Sonona
2. Aibu
3. Kudharaulika hata akifariki

Kweli kuishi na mke kunahitaji akili na busara, ila sio ubabe. Nitakuonesha jambo lakujifunza.
Playing dead is one of the technique that may earn you another day
Tuseme mfano Magu ni baba sisi ni watoto na Samia ndio alikuwa mama yetu. Kwa mambo yalivyo sasa hali ya familia na historia ya baba yetu ipoje?

Hii dhana yako ndio ile ile ya marehemu baba yetu Magu. Na ukweli mchungu hii dhana haifai kuongozea familia.

Utashangaa wale wanaowacheka na kuwaita wanaume wenzio dhaifu ndoa na familia zao zinateketea alafu wale wanaoitwa dhaifu ndoa na familia zao zinastawi.

Ni hayo tu Mkuu.
Playing dead is one of the technique that may earn you another day
 
MKIGOMBANA NA MKEO, AKAENDA KWAO, USIMFUATE WALA USIMTAFUTE

Anaandika Robert Heriel.

Kabla hujaoa jifunze kuwa Mwanaume. Niliwahi sema, mwanaume ni AKILI.
Kabla hujawa Baba jifunze kuwa Mtawala.
Na ili uwe Mtawala yakupasa uwe na hekima na busara. Pia uwe na maamuzi yasiyo yumba(uwe na msimamo).

Kitu kikubwa Kwa Baba ni Heshima, mwanaume Bora hulinda heshima yake kuliko kitu chochote. Yupo tayari kupoteza vyote lakini sio kupoteza heshima yake Kama Baba. Ndio maana Baba bora ni rahisi kufukuza mke na watoto pale anapoona heshima yake IPO hatarini.
Mwanaume anayepuuza heshima yake na kujali vitu vingine anapoteza sifa ya kuitwa Baba.

Mwanaume aliyeiva kamwe hawezi sumbuliwa na Mwanamke. Mwanaume ili asumbuliwe na mwanamke na hapa nazungumzia mke wake sharti aongozwe zaidi na Hisia pasipo Akili. Na siku zote mwanaume anayeongozwa na Hisia huyo sio mwanaume halisi.
Kama nilivyosema hapo juu. Mwanaume ni AKILI. Sio ajabu kwenye maandiko waliposema ishini na wake Kwa Akili.
Tafsiri yake ni kuwa pasipo akili heshima ya mwanaume ipo mashakani.

Baba ni jina kubwa. Baba hakosei. Na hapa namaanisha Baba aliyejifunza kuwa Mtawala.
Ikiwa Baba hakosei, tafsiri yake Baba haombi Msamaha.

Baba kuomba msamaha tafsiri yake hajielewi, hakujua alichokuwa anakifanya, Baba sharti awe na msimamo hata Kama wengine watamuona anakosea. Huyo ni Baba. Baba hapaswi kuwa kigeugeu.

Ikiwa mwanamke ambaye ataitwa/utamuita Mkeo mkakosana, iwe Kwa sababu yoyote Ile, iwe wewe ndiye chanzo cha ugomvi au yeye ndiye chanzo cha ugomvi. Akaondoka kukimbia kwenda kwao pasipo wewe kumfukuza,
Akaenda kwao wakamlaki Kwa sababu ni mtoto wao, wakijua walimuozesha kwako,lakini wakampokea,
Kamwe usijeenda kumchukua, wala USIMTAFUTE, wala usitake Suluhu naye.
Mwanamke kuondoka nyumbani pasipo iidhini ya Mumewe ni kosa tosha la kumfukuzisha kwenye nyumba yako, isipokuwa Kwa sababu zinazohatarisha usalama wake kama kupigwa na mumewe ikiwa ni Wale wanaume vichwa maji. Na hapa kupigwa namaanisha kupigwa haswa sio Yale makofi mawili matatu ya kuonywa.

Mwanamke anapokimbilia kwao na akapokelewa na wewe ukaenda kumchukua ni dalili kuwa utawala wako umepinduliwa na sasa wewe hauko utawalani.
Mwanamke kama itatokea akaona sababu ya kukimbia nyumbani kwako basi itampasa akimbilie kwenu, yaani Kwa Mama yako au Baba yako(akimbilie ukweni).
Hiyo ndio Heshima.

Na ndio maana ya wewe kuoa na kumuita huyo ni Mkeo. Lakini sio jitu umelioa likufanyie mapinduzi, ati uende ukalichukue kwao, hiyo kamwe haiwezi fanywa na Mwanaume aliyefunzwa akawa Mtawala Kama ilivyosilika ya mwanaume.

Mwanaume haweziitwa kikao ukweni akaenda, isipokuwa ukweni wanauwezo wa kuwasiliana na Familia ya Mkwe wao(mwanaume aliyeoa binti Yao), kisha wazazi wa mwanaume waitishe kikao, kisha upande wa kiukeni ualikwe Kama wageni na watoe malalamiko Yao.
Wanawake wengi ukienda kuwachukua kwao, hugeuka Mateso kwako hapo baadaye, huwa wajeuri, lazima wakupelekeshe kwani wanajua kabisa kuwa huwezi ishi pasipo wao.
Nimeshuhudia haya Kwa sehemu kubwa, nimejionea Kwa macho yangu na kuyafanyia tathmini hivyo maneno yangu yamepimwa yakathibitika.

Jifunze kukaza roho kabla ya kuitwa Baba. Jifunze kufanya maamuzi magumu kabla ya kuitwa Mume. Baba ni Cheo ambacho anastahili mtu mwenye maamuzi magumu. Ubaba Kwa sehemu hauhitaji kuwa na huruma hata kidogo.

Baba hasikilizi yeyote isipokuwa akili yake na namna ya kulinda heshima yake. Hakuna cha serikali, hakuna cha mchungaji sijui Sheikhe, hakuna cha wazazi. Linapokuja suala la heshima yako kama Mwanaume usimsikilize yeyote Yule.
Usihudhurie vikao ambavyo havina msingi wowote.
Mpaka wanakuozesha binti Yao waliridhishwa na kuwa wewe ndiye utakayemsimamia na kumhudumia mtoto wao.

Kama nitakupa binti yangu akaleta upuuzi wa kukimbia, Kwanza sitampokea, lakini kama atapata njia mbadala ya kwenda Kwa watu wengine. Fukuza na nitakupongeza na kukuona wewe ulistahili kumuoa mwanangu.

Lakini binti nimekupa alafu kakukimbia alafu unaleta pua yako kwangu, hakika nitakutoa nduki na panga mchana kweupe.

[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kama utatumia hisia ni kweli utakutwa na hayo uliyoyasema,

Mwanaume ni AKILI.
Kabla hujaoa jifunze kuwa Mwanaume, yaani kutumia zaidi kuliko hisia. Usiitumie moyo.

Pengine hujui maana ya Mtawala ndio maana unaleta mambo ya Sonoma, aibu na kudharaulika.

Linapokuja suala la heshima lazima lipaganiwe Kwa nguvu zote pasipo kujali matokeo
Mkuu Robert!Haya uliyoyaandika ni kama vile umepitia misingi yangu na wewe umecopy na kupest huku.Hakika nimekuwa nikiheshimika na familia nzima za ukweni kwangu kwa misimamo kama huu.Na mpaka sasa nina wake wawili na wala sina hofu yoyote.
 
Mkuu Robert!Haya uliyoyaandika ni kama vile umepitia misingi yangu na wewe umecopy na kupest huku.Hakika nimekuwa nikiheshimika na familia nzima za ukweni kwangu kwa misimamo kama huu.Na mpaka sasa nina wake wawili na wala sina hofu yoyote.

Hapo kwenye mke wa pili 🖖🖖🖖
 
Akienda mwache aende atakaa atachoka ipo siku atakupigia anauliza yaani umesindwa hata kuomba msamaha!!
 
Mi Nina principal Moja ngumu kidogo ni kama yako mkuu. Kabla cjaoa nilimwambia wife kabisa. Cku tumegombana kwa namna yoyote ukaenda kwenu hakutakuwepo kikao wala cntakuja kwenu. Kwasababu ninaamin mpaka umeenda kwenu ni kwamba umekimbia moto hapa so umeenda sehem tulivu kupumzika. Ni kama vile nikukute unakunywa sumu aisee ckunyang'anyi nakuacha unywe tukakuzike ukapumzike coz ndio ur wishes.
 
Mi Nina principal Moja ngumu kidogo ni kama yako mkuu. Kabla cjaoa nilimwambia wife kabisa. Cku tumegombana kwa namna yoyote ukaenda kwenu hakutakuwepo kikao wala cntakuja kwenu. Kwasababu ninaamin mpaka umeenda kwenu ni kwamba umekimbia moto hapa so umeenda sehem tulivu kupumzika. Ni kama vile nikukute unakunywa sumu aisee ckunyang'anyi nakuacha unywe tukakuzike ukapumzike coz ndio ur wishes.

😂😂😂
 
Ulichosema ni kweli,,mimi mwenyewe ni mwanamke lakini kwenye ukweli tukubali. Mara nyingi inachangiwa na wazazi,,sababu kama binti ameolewa anakuja nyumbani unampokeaje,,busara ni kumshauri binti malalamiko ayapeleke upande wa mume.

Nakumbuka kuna dada yangu mmoja miaka hiyo wakati ametoka tu kuolewa. Mume wake akawa mtu wa matukio na michepuko basi siku moja akaondoka akajidai karudi nyumbani kwako. Mama yake akamuuliza umekuja kufanya nini kusalimia na mume wako amekuruhusu? akajibu hapana. Akamjibu oooh mume wangu ana michepuko? Akamwambia wewe si ndo ulimtambulisha kwetu kuwa unampenda na uko tayari kuishi naye,,,kwa hiyo ukija nyumbani ndo ataacha michepuko. Rudi kwa mume wako mkayaongee wenyewe ukichoka nenda mahakamani kadai taraka. Basi akarudi kwa mumewe toka siku hiyo hajawahi kupeleka malalamiko,, wakikosana wanamalizana wenyewe.
Lakin pia tamaduni zetu upande wa mwanamke kushika simu kumpigia mkwe wako kwa sababu za ugomvi huwa wanaona kama matusi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marioo hawana Akili, hawana maamuzi, marioo hawezi kuwa na msimamo thabit usio yumba. Hizi ndio sifa zilizotajwa kwenye post.
 
Back
Top Bottom