Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Miaka michache iliyopita nilikuwa kwenye pita pita ya mitaa za Nairobi. kutahamani mbele yangu kushoto kuna mama mmoja akaniita. sijakaa vizuri mwingine pembeni kulia nae akaniita tena kwa nguvu 'kuja huku!'. kwanza nikapigwa na butwaa. Kulikoni? kutazama mbele pia kukawa na mama mwingine wa kisomali nae ananiita niende kwake. huku nyuma nako nikasikia naitwa na mama mwingine! Nikajua hapa nimepita kwenye mitaa nisiyoitarajia. ilibidi nitafute junction haraka na kutokomea huku nikitweta utadhani nimetoka kukimbia marathon. Mdau hususan Mwanamme mwenzangu wewe ungetii wito? kama ndio ungewatembelea wote wakukaribishao?