SI KWELI Ukihisi harufu ya wali au mchele uwapo porini ni ishara kuwa Chatu yupo karibu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Yaaah hiii kitu inatokeaga sana Maporini, hata mimi nisha experience hii kitu, sio chatu, tunavyoaminigi ni hawa Nyoka wadogo (cobra) anakuwa anatoa Miayo.

Kwa upande wa chatu ni moja ya viumbe adimu sana kuonekanaa. Ukikutana naye kwenye anga zake umekwisha.

Nimechunga sana ng'onbe wa Digii Mapori ya Mavota - Biharamulo Kagera, na Kigosi (Ushirombo) - Geita
 
Yeye siyo kwamba anatoa harufu hiyo akiona upo karibu. Inasemekana ni hatua ya uwindaji wake.
Hiii imani ipo sehemu nyingi. Hata mimi mara kadhaa nimeshapita maeneo nikasikia hiyo harufu ya wali. Kwangu mimi nadhani kuna mimea/miti ambayo huwa inatoa hiyo harufu. Nakumbuka kuna mmea mmoja huwa unatoa harufu ya maziwa ya mgando.
 
ikitokea upo porini na ukahisi harufu ya wali au mchele unapaswa kuchukua tahadhari kwani ni ishara kuwa chatu yupo karibu na anatoa harufu hiyo kukuvuta.

hii story nimewai isikia katambo sana.

Hiyo harufu huwa si ya chatu ila nyoka flani wakuitwa Kifutu.

Niliskiaga Enzi hizo majini wanapika

Miaka ya hivi karibuni ndio nikaskia ni chatu huwa anapumu hiyo harufu ya wali.

Yeye siyo kwamba anatoa harufu hiyo akiona upo karibu. Inasemekana ni hatua ya uwindaji wake.

kipind nipo shule ya msingi tuliambiwa kuwa tukisikia harufu ya pilau chooni mida ya saa saba mchana, tusiseme kuwa eti pilau inanukia, eti huyo ni jini, tukisema tu tutapigwa makofi.

nahisi hizo ni nadharia tu.

Huwa inakuwa ni nyoka anajivua magamba


Sio chatu. Bali nyoka yoyote anapojitoa kwenye magamba ndio hiyo harufu ya wali kama unapikwa inasikika. Vile vile kama wali
Hiyo ni mitazamo ya kwenye jamii , maoni ya watu

~Lakini sayansi yenyewe je..?

Viumbe vidogo na vikubwa kwenye udongo (kama vile bakteria, minyoo); madini katika udongo (kama vile chuma, magnesiamu, phosphates); unyevu, maji na vitu vinavyooza kama vile majani, magome, wanyama waliokufa husababisha harufu tofauti za msitu

Moja ambayo inaweza kuwa ya mchele uliopikwa lakini kwa watu wengine wakapata harufu tofauti.

Aina ya harufu inayotolewa inategemea mambo kadhaa kama vile aina ya udongo, kitu kilichoozea ndani ya udongo
 
Si harufu ya chatu bali ni harufu ya nyoka aliyejivua gamba.
Ukifuatilia eneo hilo utakuta gamba lililovuliwa na nyoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…