SI KWELI Ukihisi harufu ya wali au mchele uwapo porini ni ishara kuwa Chatu yupo karibu

SI KWELI Ukihisi harufu ya wali au mchele uwapo porini ni ishara kuwa Chatu yupo karibu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Habari,

Kumekuwa na hoja mtaani inadai kwamba ikitokea upo porini na ukahisi harufu ya wali au mchele unapaswa kuchukua tahadhari kwani ni ishara kuwa chatu yupo karibu na anatoa harufu hiyo kukuvuta.

Je, kuna ukweli kuhusu hoja hii? Tunaomba ufafanuzi.

1713444598154.png
 
Tunachokijua
Chatu ni aina mojawapo ya nyoka ambayo ni wakubwa kiumbo. Tofauti na aina nyingine za nyoka, chatu hawatoi sumu (ni nyoka wasio na sumu). Chatu wanaishi katika maeneo ya kitropiki ya Afrika na Asia. Wanaweza kupatikana katika misitu ya mvua, savanna na jangwa.

Kama alivyouliza mleta mada hii, kumekuwa na hoja ya kijamii inayodai kwamba Chatu chatu ana harufu ambayo anaitumia kuvutia mawindo yake. Baadhi ya simulizi zinadai na kutahadharisha kwamba uwapo porini na kusikia harufu ya wali au chakula basi unapaswa kukaa mbali kwani ni ishara kwamba Chatu yupo karibu. Hoja inayofanana na hii pia imewahi kuletwa ndani ya JamiiForums (Soma Hapa) ambapo Mwanachama Mshana Jr alikuwa akieleza namna ngozi ya Chatu ilivyo na nguvu ya kumpumbaza na kuvuta Mbwa kujipeleka mwenyewe.

Je kuna ukweli wowote kuhusu madai haya?

JamiiCheck imefuatilia madai haya kwa kufanya mawasiliano na Afisa Habari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA), Beatus Maganja na
Mhifadhi na Mkufunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Tito Lanoy ambao wote wanakubali kuwa nyoka anapojikoboa (kujivua) ngozi huwa kuwa na harufu fulani kama marashi lakini haifanani na wali.

akifafanua zaidi hoja hii, Beatus Maganga anaeleza kuwa hii inatokana na dhana za kijamii tu ambazo zimekuwa zikiaminika hivyo na kurithishwa katika vizazi na vizazi. Anasema:

Madai kuwa ukipita sehemu ukasikia harufu ya wali na kujua kwamba eneo hilo linahusiana na uwepo wa chatu au nyoka wakubwa si kweli.
Inawezekana wakati nyoka anajivua magamba huwa kuna harufu fulani labda watu watakuwa wanahusisha harufu hiyo na harufu ya wali lakini sidhani kama inatoa harufu ya moja kwa moja ya wali.
Kwa uzoefu wangu hiyo ni dhana tu na sio jambo la Kisayansi, ni stori tu zilizopita tangu enzi na enzi.
Kwa upande wake Tito Lanoy Mhifadhi na Mkufunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka anaeleza kuwa nyoka anapojikoboa ngozi yake hutoa harufu fulani isiyovutia 'Odor Smell' ambayo hutokana na majimaji anayotatoa wakati wa kujivua ngozi yake. Harufu hiyo hutofautiana kati ya nyoka mmoja na mwingine na huisha baada ya ngozi na majimaji hayo kukauka. Akifafanua zaidi hoja hii Tito Lanoy anasema:

Ni hivi inapofikia muda wa nyoka kujikoboa magamba yake kwa ajili ya kukua kuna majimaji ambayo yanakuwa kwenye magamba yake, yale majimaji huwa yanatoa harufu fulani ambayo hupotea baada ya kukauka. Na kuna mimea ambayo huwa na harufu hivyo mtu akisikia harufu ya mimea na akiona nyoka maeneo hayo anahisi ni harufu ya nyoka jambo ambalo sio kweli.
Harufu hiyo huwa ni mbaya na haifanani na wali kama inavyodaiwa. Maji hayo huitwa Lymphatic fluid ambayo nyoka hutoa na inamsaidia kutenganisha mwili wake na ngozi (Damis na Epidamis ya ngozi ya nyoka)ndiyo huwa na 'Odor smell' ambayo huisha kwa kadri ngozi hiyo inavyokauka lakini sio kwamba ukihisi harufu ya wali basi ni ishara kuwa nyoka yupo hapo.
1714210610851-png.2975198

Dhana hii inaweza kuwa imetokana na mtu aliyeona nyoka mahali labda akasikia harufu fulani na kudhani ni ya nyoka, hii dhana si ya kweli.

Mbwa na kumfuata Chatu mwenyewe
Tito Lanoy anaeleza kuwa suala Mbwa kudaiwa kumfuata chatu mwenyewe kuhusushwa na harufu sio sahihi. Mbwa humfuata chatu sababu chatu huweka mtego kwa kuchezesha mkia wake ambao humzubaisha na kumfanya Mbwa asogee mwenyewe.

1714210261593-png.2975190
Akisogeza karibu na mkia ndipo humvamia na kummeza. Kitendo hiki cha kutikisa mkia chatu hukitumia kama mbinu na uwezo wake wa kuwinda.

Hivyo, kutokaka na ufafanuzi huu kutoka kwa Mtaalamu wa Masuala ya Wanyama JamiiCheck inaona hoja inayodai kuwa ukisikia harufu ya wali uwapo porini basi ni dalili kuwa Chatu yupo karibu haina ukweli.
Wakuu habari za asubuhi!
Je uliwahi kunusa harufu ya wali/ubwabwa porini ambako hakuna hata dalili ya watu kuwahi kuishi?
Hii harufu huwa inatokana na nini hasa ?


USSR
 
Nyoka akijivua magamba yake, ile harufu hata ni mixer ya michele yote, wa mbeya, moro na kanda ya ziwa.
 
Mmeona mshana JR ,haonekani hapa na nyuzi zake mmeamua mmtafute kivingine
 
Back in de dayz secondary school.mimi na wanangu ilikuwa weekend tukasema tukatembee milimani.
Shule ilikuwa inje sana ya mji.tulipo anza kupanda milima (msituni).tukafka katikati,tukakuta mawe tukashauriana tupumzke kidogo kwani kigongo kimesimama balaa.

Pembeni ya yale mawe kulikuwa kama kuna shimo(kipango).
Baada ya dakika kadhaa tuna endelea kufurahia mandhari na story mbili tatu.ghafla kijiharufu kama cha wali kikaanza kuvuma tena kwa wingi.

Kumbe kila mtu ameanza kukipatapata ila tunavunga.kwani wengine wanaimani kuwa hapo kuna majini.

Kunamwanangu mmoja akafyatuka ghafla kama risasi.wote tungaunga kushuka kwenye ule mlima.tulitelemka kama tuko tambalale.kila mmoja anataka kuwa wa kwanza kumbuka huo mloma umezungukwa na msitu mzito kwaiyo unavyo achwa nyuma unajihisi ww ndio sadaka.

Baada ya mbio ndefu tulafka kwenye uwanda wa nyasi ndipo tukafunga break.tukaanza kumuhoji alichomoka yule wa kwanza"vip unakimbia nn.akasema kwani nyie hamjui.
Akasema hamkusikia harufu ya wali basi 😃 😀 😄 kila mtu akaanza kufunguka aah niliskia ila nikawana naogopa kusema.
 
Mimi nitatembea na maharage nazi ili nipate wali maharage ya nazi. Gharama za maisha itapungua
 
Mimi kwa ufahamu wangu mdogo najua kuna mnyama flan hiv yuko kama paka(paka pori) ndio ukojoa mkojo wenye harufu hiyo kama wali hvii
 
Back
Top Bottom