ERoni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 48,052
- 104,677
Ndugu zangu,
Maisha hayajawahi kuwa fair hata kidogo, coz dunia nayo haipo fair kwetu. Wapo wenzetu kwa tofauti hii ya usawa, wamezaliwa na kukuta mambo yapo vizuri kuanzia kuvaa, kula, kulala na hata mengine ambayo kwa sisi wengine tungesema ni anasa tu lakini wao wanayo na wakikuona wewe huna wanaweza kushangaa. Hawa ni aina ya watu ukimwambia "sina hata buku mfukoni hakuamini".
Sasa basi, kwenye kutafuta kuna siku lazima utatoka "kwenu" na kwenda huko kujitafutia/kujitegemea. Tuseme umeshaua college sasa inabidi kijana uchomoke kwa bimkubwa na mzee uanze kuhaso. Hapa ndipo mambo yanapobadilika, wale dunia iliyoamua kuwa fair kwao wataingia mji tofauti na kwao, watachukua self-contained room yenye sebule na jiko(wenyewe wanasema maji na umeme unajitegemea), around 250,000p/m, si wazazi wame-provide bwana, no worries hata. Huenda hata mchongo hana ila kodi ikiisha daddy atatuma nyingine tu...dunia iko fair kweli?
Kuna wale wanajiamini, wanatoka huko wanakuja town hawamjui yoyote, hawana ndugu, wapo na kianzio cha 500k maximum, hats off to them kwa kweli. Hawana connection wala mchongo, ila Mungu sio Eroni after 5yrs uliza yuko wapi and you'll be shocked. Hawa watu ni majasiri sana, imagine unaingia Dar humjui yoyote, unakutana na stand kubwa pale Louis kwa Magu...then from there unaanzia wapi.. hats off once more!!
Kuna sie waoga, tunafikia kwa kaka/dada, uncle/auntie etc. Aisee hatuna mishe ndio tunatembeza khaki zetu na kutwa tupo ajira portal. Dunia ikivyokosa adabu, unfairness ya hii dunia dhalimu, no equality wala equity, unakuta tupo kwa auntie/uncle for yrs...mambo hayaendi, hatuwezi kurudisha mpira hata kwa beki, lakini gozi limekuwa gumu halichezeki tena.
Tunaoangukia hapa tufanyeje ili tusichokwe na wenyeji wetu?(kumbuka binadamu ana tabia ya kuchoka, so tusiwalaumu sana wenyeji wetu)
1.....
2.....
3....
4....
Jadili kidogo hapo, kipindi hiki cha mpito chaweza kuwa kigumu kuliko hata hizo course works na UE.