Ukiishi kwa ndugu, rafiki, jirani zingatia haya

Ukiishi kwa ndugu, rafiki, jirani zingatia haya

La kuzingatia ni moja tu FANYA KILICHOKUPELEKA 100%....,,,na mambo mengine yasiyo na mpango yatajichuja yenyewe....

Zingatia Ratiba za wenyeji,,,Epuka kurudi mida mibovu wenyeji wawe daily wanakufungulia mlango(WATAKUCHOKA),,,,hakikisha ukifika kwa watu usiharibu utaratibu wao hata mmoja,,,,Yaani kuongezeka kwako wewe wakuone kwenye ratio ya msosi tu,, Vingine viache viende kama ulivyovikuta.....hujashirikishwa Jambo basi KAUSHA,,acha kiherehere...

Jitahidi usiwe mzigo,,,hela ya kujikimu nenda nayo,,,usianze kuomba kwa wenyeji(hapa ndio VITA ilipo)

Mwisho,,,Hakikisha umeenda na Chakula chako,,,Mahindi, Viazi, Mchele,,Maharage.....Kila kimoja walau Debe 1,,,KAMWE USIENDE MIKONO MITUPU,,ikiwa hujui utaondoka lini...

Note: kuna watu asili yao tu ni hawapendi tu wageni,,so ukikutana na hao,,hayo yote nilosema hayatasaidia,,ONDOKA UPESI.
 
Jikaze
Screenshot_20220427-213714_WhatsApp.jpg
 
Kuishi kwa ndugu, mambo ya kufanya
1. Siku zote amka mapema na ufanye shughuli za kimsaada kwenye mji huo, kwa mfano kufagia, kusafisha mabanda ya kuku n.k. wjatever it is, lakini asubuh na mapema ikukute nje.
2. Jitahidi kutoka nje na kuzunguka kitaa ukitafta mishe ndogo ndogo za kukupa vijisenti ili usipauke kisoro
3. Usiwe na mazoea yaliyopitiliza hasahasa Kwa shemeji au wifi yako. Kaa kwa step wacha kiherehere
4. Ukipata chochote huko duniani, kamwe usirudi mikono mitupu, hata ndizi za buku zinaeza sindikiza wali maharagwe hapo ndani. Always provide some input kuwapunguzia mzigo.
5. Kuwa msafi, kuwa msafi kuwa msafi!
6. Fuata sheria zao, kwa mfano kuwahi kurudi, kusali n.k. kama una sheria zako kazipeleke kwenu, hapo ni kwa watu, wacha kisebengo cha kupanga masharti.
7. Hakikisha wale watoto kina "junia" hawakuzoei, wale wana mambo ya kiwaki unaweza mkata kelebu akatema meno. Jiepushe nao
8. Beki 3 ana mbolea iliopitiliza, ukipanda mbegu nakuapia lazma izae matunda. Mkwepe!
9. Kuwa mstaarabu
7&8
 
Yaaani kukaa kwa ndugu ukiwa na hizi tabia wee basi hawato kuchoka
1. Kuwa bize na mambo yako
2. Acha dharau tambua bila huyo mtu aliyekuweka hapo wewe ungekua wapi
3. Epuka kukaa nyumbani mda mwingi kuna kazi zingine ni xa hovyo utaambiwa ufanye zitakazo shusha heshima yako
4. Kama umechakalika na kupata kazi sehemu fanya juu chini usiwahi kurudi hapo nyumbani fanya kitu hadi wawe wana miss uwepo wako
5. Kama mkaka achana na mabinti wa mtaa wa hapo karibu the same kwa mdada hivyo hivyo.
6. Usikae kinyonge watakuzoea fanya kazi tafuta geto
 
Imagine mwenyeji wako anakuambia, " wewe pumzika tu, nitafanya kazi zangu"!

Atakuwa na maana gani hapo?
Dah, Jana tu jioni nimezungumza na ndugu yangu wa kike kaniambia amemwambia shemeji yake asifanye chochote yeye pale Ni mgeni atamuhudumia yeye,kuanzia kutenga chakula,maji ya kunywa amuombe atamletea,na asitoe vyombo Wala kusafisha!nikajiuliza Lengo lako haswa Nini?akanijibu SITAKI MAZOEA ndani kwangu...akizoea ataanza kuparamia vitu kwenye friji na ujuaji mwingi hataki!kijana wa watu kapigwa na butwaa maana ndio kafika kutoka Ikonda.
 
Dah,Jana tu jioni nimezungumza na ndugu yangu wa kike kaniambia amemwambia shemeji yake asifanye chochote yeye pale Ni mgeni atamuhudumia yeye,kuanzia kutenga chakula,maji ya kunywa amuombe atamletea,na asitoe vyombo Wala kusafisha!nikajiuliza Lengo lako haswa Nini?akanijibu SITAKI MAZOEA ndani kwangu...akizoea ataanza kuparamia vitu kwenye friji na ujuaji mwingi hataki!kijana wa watu kapigwa na butwaa maana ndio kafika kutoka Ikonda.
Hapo ukweli ni kuwa huyo ndugu yako hamtaki shemeji yake hapo ndani. Ni njia watu wanaitumia kuwafukuza wageni ndani kwao..

So sad Joannah lakini huyo shemeji yenu atafute pa kwenda, ndugu yako hamtaki. Anamzuiaje mtu kufanya shughuli ndogo ndogo za ndani eti "hataki mazoea"!
 
Ni kweli hamtaki, ni tabia na roho mbaya tu, nilimkumbusha tu bwana achana nae mgeni Ni Kama mawingu ya mvua hata yatande vipi yataondoka tu hayatabaki milele,akasema we dada Joa hujui tu ndugu zake huyu Bwana wanavyopenda kutawala hii nyumba.
 
Ni kweli hamtaki,Ni tabia na roho mbaya tu, nilimkumbusha tu bwana achana nae mgeni Ni Kama mawingu ya mvua hata yatande vipi yataondoka tu hayatabaki milele,akasema we dada Joa hujui tu ndugu zake huyu Bwana wanavyopenda kutawala hii nyumba.
Duh! Hapo pole yake. Lakini mimi nadhani hii kasumba ya "ndugu zake mwanaume kupenda kutawala the house", kosa sio la huyo mdada. Kosa ni la mwanaume.

Wanaume tunatakiwa tutambue kuwa, hata kama unalipa kodi au umejenga nyumba, mji ni wa mwanamke. Na watu wote inabidi wafuate maelekezo yake maaana yeye ndo waziri wa mambo ya ndani.

Sasa mwanaume ukiwa mzembe ndo hizi biashara za ndugu kuja na kuanza kumsumbua wife kwa maelekezo yasio na kichwa wala miguu.

Mi nkikufumq unasumbua mke wangu, ni uppercut chembe kidevu lazma ukae. Na kesho ake unashika nauli unachora kwenu!
 
Hapo ukweli ni kuwa huyo ndugu yako hamtaki shemeji yake hapo ndani. Ni njia watu wanaitumia kuwafukuza wageni ndani kwao..

So sad Joannah lakini huyo shemeji yenu atafute pa kwenda, ndugu yako hamtaki. Anamzuiaje mtu kufanya shughuli ndogo ndogo za ndani eti "hataki mazoea"!
Yaani tuseme siku ndio nimeoa nitambue labda mwanamke wangu anamfanyia visa mdogo angu au ndugu yangu aisee atanijua mimi ni nani hata kama huyo ndugu ni wa mbali au aliwahi kunifanyia visa

Mi nashangaa hawa wanaume wanaoshtakiwa na ndugu zao au wanaojua mke anawaonea ndugu zao kwao na wao wapo kimya aisee pengine labda wana akili ndio hao wanastahili kuwa na mke ndani maana sisi hizo akili hatuna Au labda tumeumbwa tofauti
 
Ni kweli hamtaki,Ni tabia na roho mbaya tu, nilimkumbusha tu bwana achana nae mgeni Ni Kama mawingu ya mvua hata yatande vipi yataondoka tu hayatabaki milele,akasema we dada Joa hujui tu ndugu zake huyu Bwana wanavyopenda kutawala hii nyumba.
Aisee kweli tumeumbwa tofauti yaani mdogo angu anashtakie shemeji kafanya hivi au uchunguzi wangu wa kitelijensia nimegundua unafanya visa humtaki dogo

Pengine watu wanatofautiana kwenye kukua wengine tukisema damu ni nzito kuliko maji tunamaanisha ni nzito kweli
 
Kumbuka mke ndio mwenye nyumba, day to day activities za nyumba zipo chini yake. Uombe Mungu sana awe na moyo mwema, otherwise mbona hata wewe baba utaumia sana tu.
 
Duh! Hapo pole yake.
Lakini mimi nadhani hii kasumba ya "ndugu zake mwanaume kupenda kutawala the house", kosa sio la huyo mdada. Kosa ni la mwanaume..
Wanaume tunatakiwa tutambue kuwa, hata kama unalipa kodi au umejenga nyumba, mji ni wa mwanamke. Na watu wote inabidi wafuate maelekezo yake maaana yeye ndo waziri wa mambo ya ndani.
Sasa mwanaume ukiwa mzembe ndo hizi biashara za ndugu kuja na kuanza kumsumbua wife kwa maelekezo yasio na kichwa wala miguu.
Mi nkikufumq unasumbua mke wangu, ni uppercut chembe kidevu lazma ukae. Na kesho ake unashika nauli unachora kwenu!
Ni maoni yako lakini haupo serious wewe. Mji wa mwanamke? Wewe ndio aina ya watu baada ya kuoa kwenu inarudi maiti na ndugu zako(kaka,baba,mama) wanakanyaga kwako wakiwa wagonjwa.

Kivyovyote vile ukiona unachukia mgeni, hukosi hizi tabia uchoyo,umaskini au majivuno.

Wengine tumekulia familia ambazo karibu kila mwaka tuna mgeni ambaye unaishi naye kwa miezi hadi miaka. Hii kitu imenifanya sioni kipya kuhusu mgeni zaidi ya kumuona kama ni mwanafamilia mwenzetu na nafurahia pia hiyo hali.
 
Aisee kweli tumeumbwa tofauti yaani mdogo angu anashtakie shemeji kafanya hivi au uchunguzi wangu wa kitelijensia nimegundua unafanya visa humtaki dogo

Pengine watu wanatofautiana kwenye kukua wengine tukisema damu ni nzito kuliko maji tunamaanisha ni nzito kweli
Nakubaliana nawewe mkuu, mke ni mtu wa karibu ila baba ni baba, mama ni mama hivyo hivyo kwa kaka au dada. Unaweza kupata mke mwingine ila si Baba mama kaka au dada. Cha ajabu mtu wa aina hiyo ataona ni sahihi pia ndugu wa mwanamke kutembelea home ila si wa mwanaume.

Mimi kwenye suala linalohusisha ndugu I see tutagombana kama Kiba na mke wake.
 
Toka niko Advance niliapa sitokuja kuishi kwa jamaa/ndugu mara zote nikiwa safarini ninafikia hotel hata kama nipo mkoa wenye ndugu ninaenda kuwasalimu tu na kuondoka.

Maana familia nyingi za kibongo hazina utaratibu mzuri mgeni na heshima zako watakulalisha na watoto vikojozi, utasimangwa kwenye chakula n.k
 
Back
Top Bottom