Ukiitegemea biashara yako mpya ikulishe, ikulipie kodi ya nyumba na kadhalika, jiandae kuanguka

Ukiitegemea biashara yako mpya ikulishe, ikulipie kodi ya nyumba na kadhalika, jiandae kuanguka

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Habari wakuu,

Ukosefu wa ajira serikalini, taasisi mbali mbali, viwandani n.k imekuwa ndio chanzo cha vijana wengi mpaka wazee kukimbilia kwenye biashara,

Wengi tunapoanza biashara huwa hatuna uelewa wa kutosha, maarifa tunayoyapata kwa kuulizia ulizia kwa watu, mtandaoni au kwa ndugu na marafiki huwa hayajitoshelezi, hili jambo ni hatari sana.

Unakuta mtu ameanzisha biashara yake mpya hapo hapo anaitegemea imlipie kodi ya fremu, umeme, TRA, taka, ulinzi, kodi ya anakoishi, maji, chakula, vocha, usafiri n.k,

Ukiona upo kwenye hali kama hiyo jua moja kwa moja ushaanguka, siku si nyingi utafilisika au kuanza kuhisi unachawiwa kumbe tatizo niwewe mwenyewe,

ukitaka kuanzisha biashara hakikisha una kazi (ajira), kipato kingine cha ziada cha kukulisha, kukuvisha, kukulipia kodi ya nyumba, vocha n.k hapo utatoboa mapema tu ndani ya miezi hata 9 au 10,

ila ukianzisha biashara wakati unanjaa, au umepigika ndugu wamekuchangia mtaji wa milioni 3 au umekusanya pesa ukaacha kazi, au umefungua biashara kwa pesa za pensheni baada ya kustaafu tegemea anguko, kufirisika kuhama mtaa au kurudi nyumbani kwenu. Ndio maana waswahili wanasema mwenye nacho huongezewa


Hii ndio sababu inayopelekea biashara nyingi mpya kufa haraka hata bila kumaliza miezi 8 au mwaka,

NB: USIANZISHE BIASHARA WAKATI UKIWA NA NJAA. Akili ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO

Nawasilisha
 
Nimefungua fremu ya viatu vya watoto na wanawake siku 8 sijauza hata pair 1,frame laki 2x 6 months!! Naona nyotanyota!
Nilikuwa nafanya biashara kama yako mkoani Morogoro, sikuwa na frame nilikuwa nauzia minadani, minada ya pale Moro town tu, ila bado ilinikata.

Tatizo kubwa lilikuwa kama alivyoeleza Dube hapo juu, yani pesa hiyo hiyo nile,nilipe kodi, maji, umeme, bia, n.k.

Nikafunga vilago kwenda mkoa mwingine kuzisaka.
 
Nashukuru kwa kulileta hili hapa jukwaani maana imenigusa haswa. Niliwahi kuanguka kwa kutegemea biashara moja kwa moja!

Moja ya somo ambalo nililipata ndio hili ambalo umepost hapa. You can never succeed in business kama huna namna ya kui support (probation period) mpaka itakapoanza kujiendesha yenyewe kwa uhakika. Wengi tunaanzisha biashara with expectations kwamba zitufanyie kila kitu which is not realistic kwa biashara mpya!

Ndio maana watu ambao wana extra sources of income wana succeed kirahisi sana na ku realize ukuaji wa biashara sababu anaitazama kwa kando biashara yake inavyokwenda na mahesabu yake! Haigusi kabisa mpaka itakapoanza kuzalisha faida kubwa. Ila wengine mtu anaanzisha genge na kuanza kulitafuna pre-maturely lazma ukaange mtaji!
 
Nilikua nafanya biashara kama yako mkoani Morogoro,sikua na frame nilikua nauzia minadani,minada ya pale Moro town tu, ila bado ilinikata.

Tatizo kubwa lilikua kama alivyoeleza Dube hapo juu,yani pesa hiyo hiyo nile,nilipe kodi,maji,umeme,bia,n.k.
Nikafunga vilago kwenda mkoa mwingine kuzisaka.
Morogoro 😀😀 ni mkoa ambao karibia raia wote ni wafanyabiashara sijui mnunuzi atakuwa nani?

Hakuna biashara utaikosa Moro.
 
Huo ndiyo Ukweli Mkuu!

Nilianza biashara ya M-Pesa kwa miaka 6 iliyopita. Niliweka pesa kama Million 2 tu, baada ya kulipia frame, leseni na kila kitu. Lakini, sikuwa na wazo lolote la kuniletea faida kwa wakati huo.

Mwezi wa kwanza katika biashara nilipata 36,000 tu. Imagine kama ndiyo nilikuwa naitegemea initoe.

Biashara hiyo ilinipigisha kwata miezi nane bila return ya maana. Hata mdada aliyekuwa akinisaidia nammegea sehemu ya Mshahara wangu.

Baadae hali ikachachamaa, mambo yakaanza kuwa mazuri. Angalau sasa malipo ya binti yakaanza kulipwa na Commission. Sipati kitu. Lakini it worth fighting.

Miaka sita sasa, nina mtaji wa zaidi ya Million 40 na sijawahi kutia mia yangu nyingine tangu niweke ile 2M. Imejizalisha mpaka kufika hapo.

Sema nilikuwa sichukui faida. Ikipatikana, narudisha humo humo. 2019 mwishoni ndiyo nikaanza kuchukua Commission inayopatikana huku kiasi kingine nakiacha.

Sasa imagine kama ndiyo nilikuwa naitegemea. Ndani ya miezi mitatu tu hiyo hela ingeshaisha. Kuwa na kipato kingine tofauti kitakachokuwezesha kuishi wewe kama wewe na backup ya biashara yako kama beginner.
 
Nashukuru kwa kulileta hili hapa jukwaani maana imenigusa haswa. Niliwahi kuanguka kwa kutegemea biashara moja kwa moja!

Moja ya somo ambalo nililipata ndio hili ambalo umepost hapa. You can never succeed in business kama huna namna ya kui support (probation period) mpaka itakapoanza kujiendesha yenyewe kwa uhakika. Wengi tunaanzisha biashara with expectations kwamba zitufanyie kila kitu which is not realistic kwa biashara mpya!

Ndio maana watu ambao wana extra sources of income wana succeed kirahisi sana na ku realize ukuaji wa biashara sababu anaitazama kwa kando biashara yake inavyokwenda na mahesabu yake! Haigusi kabisa mpaka itakapoanza kuzalisha faida kubwa. Ila wengine mtu anaanzisha genge na kuanza kulitafuna pre-maturely lazma ukaange mtaji!
Ni kweli, mimi nina duka yani siku ukisema uchukue laki tano urushe kwenye ada lazima upasue kichwa jinsi ya kuilipa la sivyo mambo ya goma kabisa dukani unafunga, ikawa nafanya hivi mfano budget ya chakula cha family ni laki 2 mfano kwa mwezi kwa hiyo tarehe 1 naweka vitu vya laki 2 kwa hiyo sasa hii pesa ya mboga ndio inakua inatoka dukani . na nikichukua pesa kwa shughuli isiyokua ya duka lazima nirudishe. Lkn kumbuka hapa hii 200,000 inatoka kwenye salary au mishe zingine
 
Ni kweli, mimi nina duka yani siku ukisema uchukue laki tano urushe kwenye ada lazima upasue kichwa jinsi ya kuilipa la sivyo mambo ya goma kabisa dukani unafunga, ikawa nafanya hivi mfano budget ya chakula cha family ni laki 2 mfano kwa mwezi kwa hyo tar 1 naeka vitu vya laki 2 kwa hyo sasa hii pesa ya mboga ndo inakua inatoka dukani . na nikichukua pesa kwa shughuli isyokua ya duka lazima nirudishe. Lkn kumbuka hapa hii 200000 inatoka kwenye salary au mishe zingine
Kwahio unaidumbukiza tu inazungukaga mle siku ukiitoa hamna impact
 
Umenena, ni fundisho zuri, biashara inataka uelewa wa hali ya juu. Ila muombe Mungu wako kuhusu"chuma ulete" kama ni uswahilini, hawataki ufanikuwe. Ulimwengu wa roho unaangusha sana watu pasipo kujua.
Hapo kwenye ulimwengu wa roho nimebaki najiuliza, upande unaotizamana na biashara yangu kuna frame kubwa tu na nzuri sasa kila anaepanga pale nadhani kodi ikiisha haendelei kukaa pale na wengine mwanzo tu wa biashara wanakua wazito kuendelea na biashara eneo hilo.

Sasa story zilizopo ni kuwa before kulikuwa na mpangaji akawa ametofautiana na mwenye nyumba akaamua kuhama pale na kumwambia mwenye nyumba hutokaa ufanye biashara hapa, huwa ukiona mpangaji amepalipia anaanza kuidesign anavyotaka iwe unaona huruma tu maana miezi mitatu haiishi ni either aone uvivu kuendelea na ile biashara au ahame
 
Back
Top Bottom