Ukiitegemea biashara yako mpya ikulishe, ikulipie kodi ya nyumba na kadhalika, jiandae kuanguka

Kuna jirani yangu yeye alifungua mini-supermarket daily anatupa vitu vilivyooza/haribika hajawahi kuuza hata mkate 1pc. Kweli biashara hizi tuwaachie Wapemba/wahindi/waarabu sisi waswahili tuendelee kupiga domo Kama Msemaji (aliyetimuliwa)
Hizi biashara za kuuza bidhaa zinataka moyo sana..
Mimi kuna miaka nilikuwa na biashara ya hardware, nikabebwa na ule ujinga wa vitu vya hardware haviozi, ndio haviozi ila je mzunguko upo?
Kuna items niliweka toka nafungua duka mpka limekuja kunishinda hazijauzika kabisa na hapo ni kama miaka mitatu.
Hizi physical business zimenipa uoga sana, hata kama nitarudi kwenye biashara basi nitafanya services na sio kuuza bidhaa.

Ila cha ajabu watu humo humo wanatoboa na wanafanya mambo makubwa kabisa [emoji3][emoji3] ukiwa na imani ndogo utasema wanaroga .
 
[emoji3516]
YAANI MILIONI 4 UNUNUE DAWA YA AINA MOJA PEKEE??!!

HUKO NI KUTAKA DAWA ZIJE KU_EXPIRE WAKATI MZIGO UPO MWINGI-
UPATE HASARA.

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
Supernatural power...can you add something to this statement?
 
very nice observation..noted something..stay blessed!
 
Hili ndo la kushangaza aise, biashara iyo iyo kuna waja wanafanikiwa na biashara igo iyo kuna waja wanafeli kbs yani...ndo hapa msemo wa kupata ni majaaliwa unapochukua nafasi yake.
 
Hii ni kwa experience yako Au general!?
Kwangu imefanya kazi
It goes well so far.
Frame paid in advance

kama lengo lako limesimama
Na unajua unachotaka
Izo ulizotaja ni simple challenges.

(mtazamo wangu)
Huwezi lipa frame in advance kka kwa bongo hii Cha msingii kma upo na business ambyo ndio inaianza na waotegemea in running ur life cha msingii tafta biashara ndgo ambyo waifanya kila siku inakuwa Kama part ya biashara means unaweza ukaianza hiyo mfno fungua genge la matunda au kijiwe chchote kaanga samaki kuku broiler au chchote kisichohitaji investment kubwa Wala Mambo y Kody Anza na hichoo Cha msingii iwe biashara ambayo inagusa direct maisha ya watu kwa kila siku ukianza kupta hta 5000 -10000 kwa sikuu Anza biashara yako Sasa
Badae njoo nishukuru
 
Ntakushukuru vipi na hujajua biashara pia!
Bytheway frame ishalipiwa!

kwa ulichosema sijui Kama kinaeleweka.
Yani ili niwe na biashara mpya inabidi niwe na biashara ndogo kwanza!?

kuna biashara isiyogusa maisha!?
Hapo ndio kwenye makosa.
What is that!!?😂

(naheshim wazo lako)

na kwanini kila anaeanza biashara anaita biashara ndogo ndogo!?
Kwanini uanze na fikra ndogo!?

na kama kwako haijafanyakazi haimaanishi wote haijawezekana.

kama uliweka mkakati wako sawa
Ukajua unachotaka hiwezi ita biashara yako ndogo.

kwanza mtaji si pesa Pekee(ingawa ni mhimili mkubwa)
WAZO lako kwanza ni mtaji.
The rest is to get your butt up and work hard

PERIOD.
 
Wazee vipi biashara ya dagaa wakavu toka ziwa victoria hasa mikoa ya Kanda ya kusini,wenye uzoefu na hii watoe ushuhuda hapa
 
Nimefungua fremu ya viatu vya watoto na wanawake siku 8 sijauza hata pair 1, frame laki 2x 6 months!! Naona nyotanyota! Mzigo (gharama)1.5m, leseni+bills (bado sijapigia hesabu). Halafu utashangaa TRA sijui manispaa na ving'ora.

Biashara sasa hivi waru wengi wananunua mtandaoni i mean inst gram anaona kitu anaagiza kupitia inst ukikaa usubiri wateja wa kupita mamaweeh itakula kwako na kama hiyi fremu yako ipo sehemu haiko busy ishakula kwako[emoji28][emoji23]
 
Biashara sasa hivi waru wengi wananunua mtandaoni i mean inst gram anaona kitu anaagiza kupitia inst ukikaa usubiri wateja wa kupita mamaweeh itakula kwako na kama hiyi fremu yako ipo sehemu haiko busy ishakula kwako[emoji28][emoji23]
Poa Mama. Ila uswazi hiyo mitandao wanatumia kuchambana SI kununua bidhaa
 
Mkuu, unaizungumziaje Morogoro mjini kwa kijana anaetaka kwenda kuanza kutafuta maisha kwa upande wa biashara?
 
Morogoro [emoji3][emoji3] ni mkoa ambao karibia raia wote ni wafanyabiashara sijui mnunuzi atakuwa nani?

Hakuna biashara utaikosa Moro.
Mkuu, unaizungumziaje Morogoro mjini kwa kijana anaetaka kwenda kuanza kutafuta maisha kwa upande wa biashara?
 
Vipi ujio wa tozo za mama haijaathiri hii biashara ya mitandao? Na kama ndio ni kwa kiasi gani?
 
Huyu msaidizi wako, Mungu amjalie kwa moyo wake wa kupambana.
 
Risks zs bodaboda ni zipi mkuu?
Njooni tupige bodaboda, mimi nikitoka zangu kazini mida ya jioni naingia kijiweni kupose na boda yangu. Kufikia saa tatu usiku sikosi 10 kama faida ingawa hii kazi ni risk saana.
 
Kaza mkuu utatoboa kuwa mvumilivu
 
BIASHARA NA NJAA NI VITU VIWILI VISIVYOENDANA KABISA

HAKUNA BIASHARA PENYE NJAA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…