Vya mtumba au special??
Nina biashara ndogo tofauti tofauti kote kuna changamoto lakini angalau biashara ya viatu inalipa, mimi nachanganya mtumba na special ila mtumba ndio unaenda sana, nazungumizia mtumba grade 1, weekend hii liyopita nimechukua mzigo dar nikachanganya na pull meck maana ni maeneo yenye baridi hasa, mzigo ukafunguliwa pale dukani jumanne, ndani ya siku tatu(mpk alhamis) namuuliza muuzaji kaachia pea 70, na pull neck zikawa tayari zimeisha mpk nikajuta kuchukua chache..
Najua moja ya sababu za kuuza kwa haraka ni kua kuna watu wengi walishaweka oda hivyo walikua wanasubiri tuu, ila si kwamba kila siku mambo yanaenda hivyo, inaweza pita hata siku mbili sijauza chochote au uuze pea moja kwa siku, kwa ufupi ni mauzo ambayo kipindi kingine inanichukua mwezi na zaidi kuyafikia, kwahio kushuka au kupanda kwa mauzo ni ka upepo tuu, kikubwa jipe mda pale kabla hujaanza kuhukumu biashara, nakushauri usiwaze kufunga hio biashara mapema, hata mimi nilipitia hapo, na bado kuna siku haziendi vizuri ila najipa mda.
Hili la kutegemea hio biashara ndio ikupe kila kitu ndio kulinifanya nirudishe mpira kwa kipa kwanza, nikamwambia mfanyakazi afunge kwanza sitaweza kumlipa, Kwa kweli kitu ambacho sikuamini Mwenyewe kwa Hiari yake Akasema hapana atauza bila malipo maana anaona kweli ndani hamna kitu ila tukifunga kabisa ndio tutapoteza wateja na pia fursa itaenda na mwingine, aliuza 2 months bila mshahara, mimi ndio nikawa najiongeza kwa uungwana alioonesha, mpk nikaleta mzigo.