Eti jameni mume wangu amejenga kijumba haijaisha bado. Tunakula dagaa na nyama mara moja moja, je anatesaje wanae?
Kwa kuwa ni kweli ujenzi hauishi siku moja, sawa ujinga unakujaje hapo
Huu uzi ukiuangalia haraka haraka utaudharau.
Lakini kiko kitu cha kujifunza hapa:
1.Kwanza kabisa tukubaliane kwamba kuna aina mbili za watu hapa-Watumishi/Waajiriwa na Wajasiriamali(Wafanya biashara).
-Watumishi/Wafanyakazi wana option mbili katika kujenga nyumba ya kuishi-Au kujengewa nyumba kwa mkopo na kisha kukatwa marejesho kwa muda mrefu au adunduluze kidogokidogo.
Ukikopa nyumba ni kwamba kwanza utakuwa na uhakika wa nyumba yenyewe na hivo utatumikia Ndoto yako iliyotimia .
Ukidunduliza ni vizuri lakini kuna mateso makubwa sana ndani ya familia na pia inawezekana nyumba ya ndoto yako isitimie.
2.Wafanyabiashara:
Hawa nyumba za kuishi siyo option ya kwanza.
Hawa wanafungua fursa kila uchao ili kupanua wigo wa kujiongezea faida.
Nyumba ya kulala kwa watu wa namna hii inaweza kuwa au ya kupanga na au ndogo na ya kawaida sana.
Mfanyabiashara anayejitambua atajenga nyumba ya kuishi isiyoathiri kabisa mitaji yake na au akijenga nyumba ya ndoto yake basi inaweza kutokea akiwa na umri mkubwa-Say 50 and above au baada ya kuwa na mitaji mikubwa na himilivu.
Actually ujenzi wa nyumba za makuzi si kazi ya mtu mmoja mmoja(Kaya)-Hii ni kazi ya Serikali kujengea wananchi wake nyumba na kisha kuwapangishia.
Huko mbeleni nategemea hili nikitokea.