Ukijiona tu una hasira kali na yanayoendelea Tanzania ni kwako sikiliza nyimbo hizi za lucky dube ufarijike

Ukijiona tu una hasira kali na yanayoendelea Tanzania ni kwako sikiliza nyimbo hizi za lucky dube ufarijike

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
1. Children in the Street
2. Don't Cry
3. Feel Alright
4. House of Exile
5. Love Me the way I am
6. Mama Africa
7. Peace Perfect Peace
8. Prison
9. Puppet Master
10. Reap what you Sow
11. Reggae everywhere
12. Soul Taker
13. The way it is
14. I have got you Baby

Ukizisikiliza hizi Nyimbo zangu pendwa na tajwa hapa za Marehemu Luck Dube halafu ukawa bado una Usununu ( Uchungu ) wa Maisha Magumu uliyonayo na unayoyapitia basi jua kuwa Wewe hata Mbinguni hutoenda.

Jitahidi uwe Unazisikiliza mara kwa mara utaona Maisha yako ni ya kawaida, utayazoea na kuwa ni mwenye Amani, Furaha na Afya Njema hata kama huna hata Buku Moja mfukoni kama Masikini aliyetukuka GENTAMYCINE.

Mtakaosikiliza hii ( hiyo ) Playlist yangu ya Mwamba ( Mngwena ) Lucky Dube nitaomba mnipe Mirejesho yenu tafadhali kwani Ukizisikiliza hutokumbuka kama kuna Mgawo wa Maji na Hujooga, kuna Mgawo wa Umeme na hujaangalia Habari ITV au Azam Tv Leo, hutokumbuka Ajali ya Ndege ya hivi majuzi huko Bukoba iliyovutwa na Kamba ya Katani na wala hutokwazika na Tozo za Miamala ya Simu pamoja na Ukame ulioko nchini wakati kwa Vyanzo vyote vya Mvua ( Maji ) tumeviharibu kwa Upan'gang'a ( Upumbavu ) Wetu.
 
Nani asikilize hizo choir? Sijawahi kumkubali dube hata mara 1
. Raggae ipo jamaica.
 
Pini za dube ni zaidi ya kuwa na afutatu
Hizi ( hizo ) Pini tajwa hapo juu ni lazima kila Asubuhi nikiamka Kumshukuru Mwenyezi Mungu nizisikilize na nikimaliza Kumshukuru tena Mwenyezi Mungu Usiku kabla ya Kulala pia ni lazima nizisikilize.

Rest In Peace Mwamba Lucky Dube!!!
 
Hizi ( hizo ) Pini tajwa hapo juu ni lazima kila Asubuhi nikiamka Kumshukuru Mwenyezi Mungu nizisikilize na nikimaliza Kumshukuru tena Mwenyezi Mungu Usiku kabla ya Kulala pia ni lazima nizisikilize.

Rest In Peace Mwamba Lucky Dube!!!
Nikiwa safarini naweka playlist za mwamba nakula 👂 phone yaani huyu binadamu alishaimba Almost yote duniani
 
Mkuu huyu jamaa alikua gifted sana. Ngoma zake hakuna mbovu hata moja. Kuna hii inaitwa sin of flesh sio pouwa.
 
Stand alone
Big boys don't cry
Man in the city
The way it is
Dracula
Back to my roots
 
Back
Top Bottom