Ukikaribia miaka 40 utagundua vingi; mojawapo ni kuwa tunaishi na hofu ambazo si halisi

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
1,414
Reaction score
2,181
Nipo nje ya ofisi kidogo Napata muda wakutafakari. Lakini niko nje ya nchi kabisa, kilomita elf 4 toka Dar es salaam, hata simu nazopata ni chache, zile zilizopitia whatsapp tu. Hivyo akili inazidi kuwa tulivu. Na ukiongeza miji yenyewe nilotembelea si ya makelele na miziki mabarabarani wala maspika ya kuita wateja kama nilozoea kariakoo, nazidi kupata utulivu nilipofikia Samaya Hotel kando ya National Bank of Dubai (NBD) na Dubai Chamber of Commerce

Hapo nimekumbuka matukio kadhaa yalotokana na hofu isiyo halisi

Pedeshee anayeishi uhamishoni kwa wizi wa magari
Nimemsahau pedeshee nani, ila katika kipindi watu wenye pesa mjini ilikua hukutana ukumbi wa bendi hasa FM Academia nao huanza kutunza pesa kama karatasi tu. Hapa wanamuziki hawa wenye asili ya Kongo wakawaita pedeshee (PDG)(kifaransa 😛resident Director General).

Hofu: Baadhi kwa kuhofia hadhi yao inashuka wakajiingiza biashara haramu, namkumbuka huyu mmoja kwa kusakwa kwa wizi wa magari ,akiwa na zaidi ya miaka 50 kalazimika kutanga tanga mafichoni nchi za watu ,muda ambao wenzie wanakula pensheni hata kwa kile kidogo.

2. Mfululizo wa wanawake wanaojiua kwa kuzidiwa madeni Vicoba
Ukifuatilia michezo ya upatu maarufu kama vicoba mitaani, kuna vicoba vichache watu huinuana tena bila riba, huzungusha biashara na mtaji unakua, wanakopeshana. Pia vicoba vingi utapata mambo ya kuumiza, kuanzia vyanzo vya kuvunja ndoa, kuongeza wagonjwa wakili na stress na kubwa ni hii walofikia kujinyonga.

Hofu: Baadhi ya wanachama hasa wanawake wana hofu ya kuonekana wako nyuma kwa fasheni ya maisha (Life style) kuanzia nguo, jezi na viingilio mipirani, simu n.k .Hivyo hujiingiza vicoba vingi au vichache vyenye dau kubwa kuliko kipato chake. Mwisho fedheha ya kudaiwa inamuelemea. Kama alishindwa kuvumilia kuonekana yuko nyuma kfasheni, atawezaje kuvumilia fedhehe ya kudaiwa kwa kuismangwa?

3. Mfululizo wa wanandoa wanaouana
Kama kuna habari zinajirudia kwa mwaka 2021 na 2022 basi ni habari za wanandoa kuuwana, vifo vya kikatili. Kuna mmoja Kigoma aliuwa familia ya watu 7!! Ikanikumbusha kisa kimoja kilotokea Misri miaka ya nyuma, bwana mmoja alimkuta mwanaume kitandani kwake na mkewe. Alichofanya ni kumchinja mwanaume Yule na kunywa damu yake.

Hofu: Mwanandoa anasaliti ndoa yake baada ya kuhisi athaminiwi ipasavyo ndani ya ndoa. Kiuhalisia hakuna njia ya kuondoa matatizo mengi duniani kama maongezi. Ndiyo maana hata uwanja wa vita kuna ofisi za mazungumzo kwanza, mazungumzo kati kati na mazungumzo mwishoni kujadili kifuatacho baada ya vita kuisha. Ongea na mwanandoa mwenzio, mwambie mwenendo wake usivyoridhisha, ukiwa na ushahidi. Epuka ninasikia, ninahisi, wanasema.

Mwisho muulize kama mkataba wenu wa ndoa anaona uendelee kwa yeye kujirekebisha au umekuwa unabana kila upande, mjivue kuwa huru.

Zingatia, jitathmini na wewe uko tayari kubadilika kuelekea mlikokubaliana kabla.wanasema watu wengi hupenda mabadiliko,Ila hawako tayari kubadilika.!! Uko kundi lipi?

4. Wanaojichubua, kubadili shepu ujanani au kufake maisha na kujutia uzeeni
Kwa uzoefu, Ili mwanamke ampende mwanaume anaangalia urefu wa mfuko wake(pesa). Na ili mwanaume ampende mwanamke anatazama sura na umbo (pisi kali).

Hofu: Wataalamu wa saikolojia wanaamini aina mbaya zaidi ya ulemavu ni hali ya kukosa kujikubali. Kuamini bila kuendana na brand ya nguo, simu n.k hautakuwa kwenye daraja hilo limewakumba hadi viongozi wa nchi za kimaskini hujikuta na matumizi makubwa ya brand za magari kuliko uwezo wa makusanyo huku viongozi wa nchi zinazozalisha magari haya makali huendesha magari ya kawaida,bali wapo wanaoenda kazini kwa baiskeli!!

Kuepuka hofu hizi siri ni moja tu
Kwanza kumuomba mwenyezi mungu akupe misimamo ya kujielewa na kutofuata mkumbo (mob psychology). Kisha hebu tazama uhalisia wa kile tunachohitaji:

1. Unaposikia njaa, tunahitaji Sahani moja tu, sisi siyo kama tembo anayehitaji kilo 150 kwa siku mpaka kilo 300.

2. Unalala padogo mno, kwenye nyumba unaingia chumba kimoja, hulali chumba chot bali kitanda ulichoweka kwenye kona ya chumba, na kitandani huenei nusu ya godoro!

3. Ukifika miaka 40 utagundua watu walikuwa wanashughulishwa (busy) na shida zao zaidi kuliko kukuona,hivyo muda mwingi ulikuwa unajiona au kujishtukia. Hapa ndiyo unaanza kuhangaika kurudi kuishi uhalisia wako

-Mwisho nikakumbuka mwenye hekima alosema sentensi mbili:

Ya kwanza:

Kondoo hutumia umri wake wote akihofia mbwa mwitu wakati wa kuchungwa, Kumbe humalizwa na kisu cha mchungaji wake. 🙂D😀)

Ya pili (ilonimaliza): Ushawahi kuona mtotoo ametoka kwao mikono tupu, na akiitwa na mzazi au mlezi wake hatakiwi kurudi na chochote.Lakini akifika uwanjani kuna vitu vya kuchezea kama midoli,mpira,vifuu vya kupika kupika n,k , Sasa mtoto anayechekesha zaidi ni Yule ambaye kwa muda mchache tu kashapiga watoto wenzie woote,kawapora vitu vyote kakusanya kwake, halafu anaitwa ,anaviacha anaondoka huku anatazama wenzie wakiendelea navyo.

Huyo ndo mwanadamu, kazaliwa bila nguo, ataondoka bila chochote, ila hapa kati kati kafanya kila awezalo kudhuru wengine ili ajikusanyie mali ambazo ataziacha tena akiitwa kwa Muumba 🙂D😀)

WhatsApp Image 2022-09-30 at 17.00.57.jpeg

Dk.Mussa Zaganza
 
Kama hii ni kweli inakuwaje mlezi wangu ambae kwa sasa ana umri wa 55 huwa ana panic kutokana na changamoto za maisha anazozipitia...haonyeshi ukomavu wa kifikra, kuna muda ana ropoka bila kufikilia kile anachokitoa mdomoni kitamuumiza vipi mwingine..........naomba tutafakari hili andiko.
 
View attachment 2372753
Dk.Mussa Zaganza
sawa sawa mkuu
 
Back
Top Bottom