Ukikipenda kitu utapambana ukipate na kibaki katika mikono yako

Ukikipenda kitu utapambana ukipate na kibaki katika mikono yako

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,237
Reaction score
1,744
Yn 14:23 SUV
[23] Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.

Kila mmoja mpaka kufika umri alionao sasa, amewahi kupenda kitu katika maisha yake, hata kama kwa wengine kinaonekana ni kitu cha kawaida.

Baada ya kukipenda hicho kitu mtu huyu atahakikisha anachukua hatua kuhakikisha anakipata hicho kitu.

Kama mtu alikuwa na kitu alihakikisha kinaendelea kubaki kwenye mikono yake.

Ukiona mtu anakuambia ameshindwa kupata kitu fulani, huenda sababu ikawa hajakipenda vizuri hicho kitu.

Upendo una nguvu zaidi vile tunaweza kuufafanua hapa, mtu akipenda kitu huwezi kumzuia zaidi utamchelewesha kukiendea na kukikapata hicho kitu, mazuio ambayo yanaweza yasiwe na matunda yeyote.

Mtu akimpenda Yesu na akamwelewa vizuri juu ya utendaji wake katika maisha yake, anaweza kufanya chochote kwa ajili ya Yesu.

Ukiona mtu unamtoa kirahisi kwa Yesu ujue huyo Upendo wake ulikuwa nusu nusu, yeyote aliyekaa sawasawa na Yesu hawezi kuondolewa kiurahisi moyoni mwake.

Yn 14:24 SUV
[24] Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.

Huwezi kusema sina muda wa kusoma biblia, ujue huna Upendo ndani yako, mwenye upendo na Mungu wake atakuwa naye karibu kwa njia ya kusoma biblia na kutafakari.

Huwezi kusema mimi nimekuwa mtu mzima sasa siwezi kuendelea na mambo ya Yesu, huko ni kupotea na kukosa mambo aliyonayo Yesu katika maisha yako.

Upendo wetu uwe juu zaidi mbele za Mungu, hatutokuwa na visingizio vingi tulivyonavyo leo vya kutuzuia kulitimiza lile kusudi la Mungu.

Ukiona unakuwa na visingizio vingi juu ya jambo fulani ujue hujakipenda, mtu akipenda kitu atapambana mpaka akipate hicho kitu.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
 
Back
Top Bottom