Kibenje KK
JF-Expert Member
- May 28, 2016
- 270
- 391
Ninatambua kwamba watu wengi wanafuta ajira usiku na mchana bila mafanikio.
Ukifikiri kwa makini utagundua kwamba, njia iliyokuwa bora ya kujihakikishia ajira sio kutafuta ajira. Bali ni kutafuta tatizo au matatizo unayoweza kuyatatua.
Jaribu zoezi hili; mwezi huu tembelea Ofisi kadhaa popote pale Tanzania halafu ukipata nafasi ya kuongea na mmiliki wa kampuni, Mkurugenzi au meneja baada ya salamu uliza, 'samahani, hivi hapa kuna tatizo au uhitaji gani kwa sasa ambao mnatafuta suluhisho?
Walio wengi watashtushwa na swali hili. Kisha fafanua kwa kusema 'Niko hapa ningependa kujitolea kutatua baadhi ya changamoto mlizo nazo kama nina uwezo nazo'.
Hii haimaanishi kwamba utafanikiwa kila mara. Lakini kuna uwezekano kukawa na uhitaji wa
1. Mtu wa Mauzo
2. Mtu wa masoko
3. Mtu wa Masoko mtandaoni (internet marketing)
4. Mtu wa Mauzo Kupitia mitandao ya kijamii (social media)
5. Mhasibu au mtunza kumbukumbu za biashara
6. Mtu wa kusaidia manunuzi
7. Mtu wa kuandika proposal
8. Mtengeneza ripoti
9. Muuzaji kwa njia ya simu (tele-seller)
10. Mtu wa IT
11. Mtu wa usafi
12. Mtu wa kusimamia usafirishaji na usambazaji
13. Mpaka rangi na repair ndogo ndogo ofisini
14. Messenger n.k.
Japo baadhi ya kazi hizi zinaweza kuonekana ni za chini lakini ndio mwanzo wa safari ya kwenda juu.
Lakini kwanini watu wengi wanasema hawana ajira wakati kazi zimejaa kila mahali?
Upofu, kuzoea maisha rahisi ya bila kuhangaika n.k.
Mimi hufikiri FURSA nyingi kuliko zote na za wazi kabisa za ajira sio ualimu wala unesi. Ni Mauzo (sales).
Kwenye ma-godown nchi nzima kuna watu wana bidhaa hawana wauzaji.
Kuna watu wana viwanja hawana wateja na kuna watu wanatafuta viwanja hawajui pa kuvipata
Kuna huduma nzuri sana kila siku zinaanzishwa wenyewe hawajui kuuza.
Sasa; tunajua watu wengi hawajui kuuza hata kama wangeoneshwa kitu kizuri cha kuuza.
Ndio maana naweka nguvu kubwa kufundisha vijana namba ya kujiuza, namna ya kuuza ujuzi, taaluma au kipaji ulicho nacho.
Kama unahitaji mtu wa mauzo au unahitaji masomo na masoko juu ya mauzo tafadhali wasiliana na mimi.
Pia kama una biashara au huduma na unahitaji mtu wa mauzo au unashindwa namna ya kuuza, Tuwasiliane
WhatsApp only 👉+255762815104
Social media 👉 #kelvinkibenje