Ukikua kiumri taste ya baadhi ya aina ya chakula inapotea ama nini?

Ukikua kiumri taste ya baadhi ya aina ya chakula inapotea ama nini?

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Nakumbuka nikiwa mdogo hadi miaka ya shuleni nilikua napenda sana wali maharake, pilau na vitu kama hivyo, ilikua wali na mimi, mimi na wali.

Cha kushangaza siku hizi ugali ndio umekua kama default food yangu, ugali nyama, samaki, dagaa ama mboga za majani, ndizi choma nyama, samaki. Maharage bado nakula bila shida ila wali umenishinda kabisa.

Nikafikiri ni mimi tu nakabiliana na hilo tatizo, jana nimekutana na classmate wangu akaniambia tatizo hilo hilo kwamba wali umemshinda kabisa sasa chakula chake kikuu ni ugali.

Wakuu kuna mtu anapitia changamoto kama hii ya kupoteza interest ya baadhi ya misosi aliyokua anaipenda?
 
Uko sahihi asilimia mia ...Binafsi hata nikienda kweny sherehe sijui vyakula vile naona kawaida sana labda matunda na ugali ila chips, wali ,pilau ,nyama ya kuku haswa haya ya kizungu sina mzuka kabisa.

Ila ugali uwe local na mboga za kawaida nitakula sana kama dagaa.
 
Ulipenda wali maharage kwasababu ulikuwa huna mbadala. Ulikuwa unalishwa na wazazi tokea utotoni, ila ulipopata mkwanja na kuanza kuishi mwenyewe ukawa na uwanja mbadala wa kuchagua vyakula vingine vyenye mapishi tofuati ya yale ya mama yako.
 
LAW OF DIMINISHING RETURN:
(The more you Consume, the more you loose an appettite)

Haipungui, ila kinachotokea ni kwamba umetumia kiasi cha kutosha hicho chakula kwahiyo umekikinai.
Kikawaida ukiwa mdogo access ya baadhi ya vitu au vyakula upatikanaji wake unakuwa limited, ila unapokuwa mkubwa una access ya kula kitu unachokitaka kwa kipimo unachohitaji hivyo nafsi inakuwa kama imeridhika hivi na hauna ulimbukeni na hicho kitu au chakula.
Mifano:
1.Rejea ile kasi unayotumia kunywa glass ya kwanza ya maji unapokuwa na kiu ukilinganisha na glass zilizofuata. Je, kasi na hamu ya yale maji itabaki ileile uliyokuwa nayo kwenye glass ya kwanza?

2.Pia rejea ile pisi iliyokuwa inakutoa udenda kabla hujaipata na hamu unayokuwa nayo baada ya kuila zaidi ya mara tatu. Je, uchu unafanana na hapo awali?
 
Ukitaka radha ile ile rudi katika umri ule ule na mazingira yale yale,Nyie ndio mlio sababisha walimu wagundue fimbo kwenye kueleweshana[emoji144]
 
Wali maharage haujawai kuniangusha hata siku moja,tena ukipikwa siku hiyo lazima niwahi kurudi nyumbani mapema kabisa saa moja tu usiku nimeshatia timu na wife anavyonijualia lazima ataniwekea ukoko na matandu kwa mbaliiii...
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] wali naziii na maharagwe...

Naupenda pia...

Nisipike mimi apike mwingine...
 
Angalia namna ya uandaaji wa hivyo vyakula pia.

Miaka ya zamani nilikuwa nakula Wali ulioungwa Mafuta.

Nilipohamia Mikoa ya Pwani, nilipikiwa Wali wa Nazi.

Kutokea hapo nikajua kumbe mapishi ndiyo huchangia radha ya chakula.
 
Binafsi Mimi ugali nimetokea kutouelewa kabisa nkila Sioni kama mtamu Yani kitu ugali mdomoni kwasasa siinjoy wakati Zamani nlikua nakula Dona hili hili now napenda Zaidi walii nakula mchana usiku....kingine nyama za michuzi nimetokea kuzikinai napenda Zaidi either zikaangwe au zichemshwe kama kuku napendelea zaid ichemshwe ninywe supu Naenjoy zaid nkila supu Ya kuku Na wali Kuliko kuki Ya kuungwa
 
Tatizo lako umezaliwa kwenye ugali afu unataka kulazimisha kula wali.
Nikwambie tu kitu ndugu kuna maeneo tanzania hii hawaamini kama ugani ni chakula. Nakupa mfano. Tembelea mkoa wa morogoro wilaya ya malinyi kuanzia itete,sofi,usengule,kiswago,tanga, malinyi mjini kwenyewe ngoheranga mpaka kilosampepo hautokuja kukuta kuna mgahawa wanapika ugali.
Na ukihitaji ugali ni lazima utoe pesa ya unga kwanza ndo utapikiwa huo ugali. Sasa njoo kwa wenyeji sasa wanaamini wakila ugali wanakojoa sana.
Hivyo nadhan haya mambo yanatokana na mazingira uliokulia mzee n.b msukuma chakula chake ugali
 
Nakumbuka nikiwa mdogo hadi miaka ya shuleni nilikua napenda sana wali maharake, pilau na vitu kama hivyo, ilikua wali na mimi, mimi na wali.

Cha kushangaza siku hizi ugali ndio umekua kama default food yangu, ugali nyama, samaki, dagaa ama mboga za majani, ndizi choma nyama, samaki. Maharage bado nakula bila shida ila wali umenishinda kabisa.

Nikafikiri ni mimi tu nakabiliana na hilo tatizo, jana nimekutana na classmate wangu akaniambia tatizo hilo hilo kwamba wali umemshinda kabisa sasa chakula chake kikuu ni ugali.

Wakuu kuna mtu anapitia changamoto kama hii ya kupoteza interest ya baadhi ya misosi aliyokua anaipenda?
hata homone za vichocheo mbalimbali vinapungua kabsaa ulafi wa unapotea kabisa na huangaiki navyo tena
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] wali naziii na maharagwe...

Naupenda pia...

Nisipike mimi apike mwingine...
Mimi wali na maharage niukute kwenye mkusanyiko wa watu/shughuli...halafu kuwe na chachandu pembeni🤣🤣🤣

Nikipika mwenyewe sioni utamu wake
 
Yaani mkuu kama ulikuwepo,mm skuizi kiti moto hakina ladha kabisa Hadi nimekikataa,wali nakula kushiba tumbo ila nainjoi nikienda bush kwa bib nakula wali unaopikwa kwenye chungu,yaani ladha yake siwezi sahau milele.Pia nimegundua Kuna ladha tofauti kwenye jiko la kuni,mkaa,au gesi,tafiti utaona.
 
Back
Top Bottom