Ukikua kiumri taste ya baadhi ya aina ya chakula inapotea ama nini?

Ukikua kiumri taste ya baadhi ya aina ya chakula inapotea ama nini?

Sio kweli mzee.wali maharage ni chakula pendwa kwa watoto umri mdogo.

Chunguza hata vijana wanaobahatika kupata kazi ktk umri mdogo hiendelez mapenzi na wali,chipsi,nyama nk mpaka umri flani upite.
Wali maharage na Ugali ndiyo Staple Foods in Tanzania. Mbali na hapo ni watu wachache mno nchini Tanzania wenye uwezo wa kula mboga saba at whim.
 
Mm breakfast yangu ni viazi mviringo vya kukaanga na udambuudambu wenye kapilipili.aisee viazi vya uswazi kwa mama asha mchafu vya Mia Mia ni vitamu balaa.mm na bite jamii ya ngano ni Kama maji na mafuta
 
LAW OF DIMINISHING RETURN:
(The more you Consume, the more you loose an appettite)

Haipungui, ila kinachotokea ni kwamba umetumia kiasi cha kutosha hicho chakula kwahiyo umekikinai.
Kikawaida ukiwa mdogo access ya baadhi ya vitu au vyakula upatikanaji wake unakuwa limited, ila unapokuwa mkubwa una access ya kula kitu unachokitaka kwa kipimo unachohitaji hivyo nafsi inakuwa kama imeridhika hivi na hauna ulimbukeni na hicho kitu au chakula.
Mifano:
1.Rejea ile kasi unayotumia kunywa glass ya kwanza ya maji unapokuwa na kiu ukilinganisha na glass zilizofuata. Je, kasi na hamu ya yale maji itabaki ileile uliyokuwa nayo kwenye glass ya kwanza?

2.Pia rejea ile pisi iliyokuwa inakutoa udenda kabla hujaipata na hamu unayokuwa nayo baada ya kuila zaidi ya mara tatu. Je, uchu unafanana na hapo awali?
kwenye Siasa za Afrika hii law of diminishing haifanyi kazi kabisa
 
Mnataka kujua sayansi nyuma ya hii dhana kwamba watu wamepoteza ladha ya wali kwa sababu ya umri? La hasha sio kwasababu ya umri. Sababu ya kisayansi ni hii:

Zile mbegu tamu za asili zenye ladha harufu nzuri zimepotea siku hizi kwani tumeletewa mbegu za kisasa kutoka Malaysia, India, etc zenye mazao mengi lakini bila ladha nzuri!
Inawezekana kiasi fulani, ila naona umri nao umetembea sana maana kuna madogo hapa wanafurahi sana kula wali kila siku ila mimi hapana.

Kingine mimi binafsi vile vyakula vya kweny masherehe ya ukumbini wanavyochanganya yaani kuna siku nilitapika labda nichukue matunda ,mboga haswa za majani ,nyama kavu ila za mchuzi ila harufu inanikera.

Kitu nakula sana ni biryani naweza kula mchana na usiku ila wali na pilau hapana kabisa...Ugali hata nile wiki mzima fresh bado nautamani.
 
Mnataka kujua sayansi nyuma ya hii dhana kwamba watu wamepoteza ladha ya wali kwa sababu ya umri? La hasha sio kwasababu ya umri. Sababu ya kisayansi ni hii:

Zile mbegu tamu za asili zenye ladha harufu nzuri zimepotea siku hizi kwani tumeletewa mbegu za kisasa kutoka Malaysia, India, etc zenye mazao mengi lakini bila ladha nzuri!
Nilikuwa sijui hili
 
Mimi naona sio kwamba hamu ya baadhi ya chakula inaondoka bali sababu ni kwamba sasa hivi una mkwanja ,vyakula ambavyo baadhi mlikuwa mnakula siku moja moja sababu ya gharama kuwa kubwa, kwenye familia za wazazi wenu mlipokulia ,kwa sasa unakipato ambacho kina kufanya uwamue Leo ule nini ,saa ngapi ,sehemu gani ndio maana utaona kama hamu imepotea ya baadhi ya vyakula lakini sio.
 
Huko ndo kuiaga dunia siyo kama tulovyozoeshwa, eti mtu akitokwa na uhai ndo tunasema ameaga dunia.
Kuaga dunia ni gradual process, anaaza kupunguza baadhi vionjo ama kwa hiari ama kwa kulazimishwa. Utaacha mwenyewe au utambiwa acha hiki acha kile hasa vile ambavyo dunia inavipenda. Ukiona uko hiyo stage basi jua safari ya kuiaga dunia imeanza.
Unachovuta acha mkuu
 
Nakumbuka nikiwa mdogo hadi miaka ya shuleni nilikua napenda sana wali maharake, pilau na vitu kama hivyo, ilikua wali na mimi, mimi na wali.

Cha kushangaza siku hizi ugali ndio umekua kama default food yangu, ugali nyama, samaki, dagaa ama mboga za majani, ndizi choma nyama, samaki. Maharage bado nakula bila shida ila wali umenishinda kabisa.

Nikafikiri ni mimi tu nakabiliana na hilo tatizo, jana nimekutana na classmate wangu akaniambia tatizo hilo hilo kwamba wali umemshinda kabisa sasa chakula chake kikuu ni ugali.

Wakuu kuna mtu anapitia changamoto kama hii ya kupoteza interest ya baadhi ya misosi aliyokua anaipenda?
Nilikuwqga nasema siwezi enda mgahawani nikaagiza sembe ila siku hizi ndio nakula
 
Nakumbuka nikiwa mdogo hadi miaka ya shuleni nilikua napenda sana wali maharake, pilau na vitu kama hivyo, ilikua wali na mimi, mimi na wali.

Cha kushangaza siku hizi ugali ndio umekua kama default food yangu, ugali nyama, samaki, dagaa ama mboga za majani, ndizi choma nyama, samaki. Maharage bado nakula bila shida ila wali umenishinda kabisa.

Nikafikiri ni mimi tu nakabiliana na hilo tatizo, jana nimekutana na classmate wangu akaniambia tatizo hilo hilo kwamba wali umemshinda kabisa sasa chakula chake kikuu ni ugali.

Wakuu kuna mtu anapitia changamoto kama hii ya kupoteza interest ya baadhi ya misosi aliyokua anaipenda?
Kiufupi umri unavyokwenda hamu ya kula chochote inapungua ,Kwa Sasa siwezi kukaa nikawaza sijala Biriyani siku nyingi hayo niliyawaza nikiwa naanza ajira na miaka 23
 
Wali za zamani ulikuwa huko poa, ukipikwa unanukia na una ladha wa sasa yamekuwa makapi hayanukii wala nini.
 
Back
Top Bottom