Ukikua kiumri taste ya baadhi ya aina ya chakula inapotea ama nini?


Kila jema.
 
Zamani nilikuwa namshangaa sana baba yangu kwanini alikuwa hapendi kula wali, kila siku tunapopikiwa wali na maharage, mama atasonga ugali au ndizi za baba, kipindi hicho wali na maharage napenda kweli, nilipofika umri wa miaka 24 adi sasa na 28 sijawahi kutaman wali wala pilau nakula basi tu sioni ladha yake na sijui kwanini, nimekuwa napenda sna ugali hata nikiwa hotelin lazima niagize ugali na mboga za aina mbalimbali.
 
Tambi ndio sijazielewa maana nikila nasikia njaa muda si mrefu na siwezi kula usiku eti nilale hapo lazima ntaamka kula usiku chakula kingine kwangu Tambi nimeweka kwenye kundi la chakula ambacho unatakiwa kula kama jioni hivi sio usiku au mchana ni kundi la chips tuu...
 
Ulipenda wali maharage kwasababu ulikuwa huna mbadala. Ulikuwa unalishwa na wazazi tokea utotoni, ila ulipopata mkwanja na kuanza kuishi mwenyewe ukawa na uwanja mbadala wa kuchagua vyakula vingine vyenye mapishi tofuati ya yale ya mama yako.
More deeply psychologically Ila najua Kuna mtu atakuja kupinga. Ila pia nikupinge Nina mtt yeye anapenda wali harage ama wali nyama. Chakula kingine hana mzuka nacho.. akikutana na sangara amechemshwa Hana mzuka smt Hana furaha Kama vyakula ivyo
 

Kula tambi na viazi mviringo pamoja na maharage, ukiweza ongezeka na chai. Uje kunishukuru
 
Kwa umri wako sijui..
Ila Wazee tastebuds cell zinakufa,
Ukiona mzee anang'angania nyama ujue ni uroho tuu ila hama ladha anaipata..
 
Ndivyo, ladha ya chakula hupungua, ndiyo maana wenye umri mkubwa wakikarangaziwa spices basi hapo hutekwa mazima. Hata take in ya maji nayo hupungua.
 
Kama mimi udogoni nilisema hata wakati wa kukata roho kitandani niletewe chips yai basi nitajitahidi nile nishushie na Pepsi baridiii ndio nife lakini mambo yamekuwa tofauti kabisa najionea sawa tu vyakula vyote
 
Nikikumbuka jinsi nilivyokuwa napenda mkate, siku hizi hata hamu sina.
Mikate ya zamani ilikuwa na ladha nzuri. Chumvi kidogo tena kwa mbali na sukari kwa mbali. Sasa hivi hakuna waokaji. Mikate haina ladha kabisa.
 
Hii ni kweli kabisa.
 
Ulipenda wali maharage kwasababu ulikuwa huna mbadala. Ulikuwa unalishwa na wazazi tokea utotoni, ila ulipopata mkwanja na kuanza kuishi mwenyewe ukawa na uwanja mbadala wa kuchagua vyakula vingine vyenye mapishi tofuati ya yale ya mama yako.
Sio kweli mzee.wali maharage ni chakula pendwa kwa watoto umri mdogo.

Chunguza hata vijana wanaobahatika kupata kazi ktk umri mdogo hiendelez mapenzi na wali,chipsi,nyama nk mpaka umri flani upite.
 
Ni kweli kabisa.

Lakini hilo swala linasababishwa moja kwa moja mifumo ya kimetabolic,ni sawa na lile swali kwanini mtoto 0-15 akilala usiku ni kama amekufa??lakini ni tofauti kwa mtu mzima hasa 25 kuendelea,ambaye hata usingizi huwa ni mtihani wakati mwingine sababu ni kwamba kama mfumo wa maisha umebadilika kwa maana huchoki sana mwili,ni vigumu kupata usingizi sawa sawa,kupata hamu ya kula(njaa) sawa sawa.

Watoto umri huo,wana mambo mengi kuanzia michezo na kazi mbali mbali,wanaunguza vyema nishati zao mwilini kiasi cha kuhitaji chakula zaidi kila wakati.

Wakati wewe mwili ndio utaamua nini kinahitajika kwa wakati upi tu.
 
Nikikumbuka jinsi nilivyokuwa napenda mkate, siku hizi hata hamu sina.
[emoji16][emoji16]imagine ukawa unajisemea ukipata kazi yako unanunua boaloaf na blueband mpaka mingine ulalie[emoji23][emoji23],

Lakini kwa sasa unawezapitiliza asubuhi hata chai hujanywa na hujui kama hujanywa[emoji23]
 
Huko ndo kuiaga dunia siyo kama tulovyozoeshwa, eti mtu akitokwa na uhai ndo tunasema ameaga dunia.
Kuaga dunia ni gradual process, anaaza kupunguza baadhi vionjo ama kwa hiari ama kwa kulazimishwa. Utaacha mwenyewe au utambiwa acha hiki acha kile hasa vile ambavyo dunia inavipenda. Ukiona uko hiyo stage basi jua safari ya kuiaga dunia imeanza.
 
Mimi imebak na ndizi,nyama choma na my wangu.Nyama mchuzi ndo nakula Kwa kulazimisha tu
 
Kweli kila mtu na pango lake...
Sijawahi penda Mikate, skonzi yaani kwa ufupi haya ma pof pof sijawahi yaelewa.
Pia vitumbua sivielewagi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…