Ukikua utajua wale uliokuwa unawategemea wakusaidie kumbe nao wanahitaji Msaada. Jifunze kujitegemea

Ukikua utajua wale uliokuwa unawategemea wakusaidie kumbe nao wanahitaji Msaada. Jifunze kujitegemea

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
UKIKUA UTAJUA WALE ULIOKUWA UNAWATEGEMEA WAKUSAIDIE KUMBE NAO WANAHITAJI MSAADA. JIFUNZE KUJITEGEMEA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Sisi Watibeli tunajifunza kujitegemea mapema tuu baada ya kujua uchi ni nini. Baada ya kusikia haya na aibu kutembea bila nguo.

2. Ndio maana maisha yetu ni Yetu. Future yetu ni Yetu.

3. Hatuhitaji kumtegemea MTU ili tukue na tufanikiwe. Tunategemea nguvu na akili zetu tukisaidiwa na Mungu aliyetuleta duniani.

4. Hatuhitaji kumnyenyekea yeyote, kumuabudu yeyote ili maisha yetu yaende.

5. Kwa sababu tulijua mapema kuwa Wale ambao tungewategemea wanamatatizo mengi kuliko Sisi.

6. Sisemi hivi kujipa moyo. Au kujifurahisha nazungumzia ule ukweli. Kwamba Wale unaohitaji msaada kutoka kwao wanamatatizo kuliko wewe.

7. Kamwe usidanganywe na Pesa au utajiri, au mwonekano. Au mavazi au chochote kinachoonekana ndio kikakupa sababu ya kumtegemea MTU yeyote. Ikafikia kumuabudu.

8. Mambo yote hayo ni yakawaida. Na hayaondoi matatizo na shida za Watu.

9. Wakati unajiliza kwa mtu. Ukiomba Msaada kama vile unamuomba Mungu. Kumbuka wale wanaokutegemea wewe na kukuomba wewe wakidhani wewe unaweza kuwasaidia na unauwezo kumbe hawajui uhalisia wako.
Vile unavyowaona ndivyo unaowategemea wanavyokuona na kukushangaa.

10. Siku zote kwenye maisha yako. Usikubali Msaada wa Bure. Usikope! Hiyo ni kanuni za Watibeli.

11. Ni Bora ufe. Kama huna kitu cha kubadilishana na huo msaada usipokee huo msaada.

12. Kupokea msaada burebure ni kujilaani. Kujidharau. Kumuabudu Mtu. Kumfanya kuwa Mungu wako. Nawe unajigeuza mtumwa wa MTU huyo.

13. Watu wote unaowaona. Wanamatatizo yao. Wote! Wanashida zao.

14. Usikae kwa mtu bure. Zungumza naye tokea mwanzo. Kuwa Mimi siwezi kupokea msaada burebure ni Bora usinisaidie nife na shida zangu.

15. If God does not come to my rescue, then no one else ever will.
Watibeli tunaishi humu. Kwamba kama Mungu hatakuja kutuokoa. Basi hakuna mwingine wakufanya hivyo.

16. Kama Mungu aliyekuumba hataki kukusaidia bure. Anahitaji ufanye Jambo Fulani ili msaada wake ufike kwako. Kwa nini utegemee mtu burebure?

17. Watibeli tunasema, kama Mungu hatataka kutusaidia. Na hatataka kuwa upande wetu. Sisi watibeli hatuhitaji msaada kutoka mahali popote.
Tutabaki hivihivi. Yaani ni Bora tufe.

18. Watu wengi wanawasema wenye mafanikio au utajiri kwamba hawawasaidii. Wengine wanafikia kuwatetemekea. Lakini nataka nikuambie hawakusaidii kwa sababu hawana uwezo wa kukusaidia. Wanamatatizo mengi na wenyewe wanahitaji Msaada.

19. Kuna wakati nilishika kiasi Fulani cha pesa Ambazo kabla sijazishika niliziona ni pesa nyingi Sana. Pesa ambayo nilifikiri Mungu akinipa ningekuwa nimefanikiwa.

20. Nilifikiri nikizipata basi matatizo na shida zangu zingeisha.

21. My friend siongei kukuhamasisha katika uongo. Kwani Sisi watibeli hatunaga desturi ya kuongea uongo hasa usio na sababu ya msingi.

22. Nilipopata zile pesa. Ndio matatizo yaliongezeka zaidi. Nilihisi nahitaji msaada zaidi. Nahitaji pesa zaidi. Nahitaji kusaidiwa.

23. Watu wakaribu wanaziona nyingi kama nilivyokuwa naziona. Mimi naziona chache.

24. Sisemi kwamba usiombe Msaada ukihisi kutaka Msaada. Bali nasema, kamwe usitegemee msaada au kusaidiwa au kumtegemea mtu akusaidie.

25. Pili kamwe Usisaidiwe Bure. Itakutesa Sana.

26. Tatu, hakuna mwenye wajibu wa kukusaidia bure. Hata Mungu wako hatakusaidia bure. Kuna mambo atahitaji uyafanye. Lakini kwa Mungu angalau hatakunyanyasa, hatakudharau, hatakuonea wivu.

27. Zaidi atataka ukue na ufanikiwe zaidi na zaidi.

28. Mtu anayekusaidia Leo atakunyanyasa Kesho. Atakuonea wivu Kesho kutwa ukifanikiwa zaidi yake. Mara nyingi atakukwamisha.

29. Kuelezea matatizo yako. Ni kujivua nguo. Kujidhalilisha kwa Watu.

30. Kamwe usijieleze kwa watu shida zako. Hakuna wakukuonea huruma zaidi ya kujichoresha.

31. Shida haziui. Matatizo hayaui. Pambana na hali yako.
Tenda kwa juhudi, bidii na akili. Ukimwomba Mungu.

32. Saidia watu lakini sio Bure. Wape mia chukua 10 ili wasijisikie vibaya waone nao walikupa.

33. Mwambie MTU nitakusaidia kitu unachohitaji. Lakini hata mimi pia ninashida. Kila MTU anashida.

34. Njoo nyumbani, wewe nimeona ni mwalimu. Nifundishie kijana wangu Yule angalau wiki hii anashida ya hesabu au mada au somo Fulani ambalo wewe ni bingwa. Alafu Mimi nitakupa pesa uliyoiomba.

35. Mpe kazi mtu inayoendana na ujuzi wake, au uwezo wake. Ili asije kukunukuu vibaya. Ingawaje kama ana bad attitude anaweza kufikiri vibaya.

36. Ni kosa kumsaidia mtu burebure.
Kama ilivyo kosa kusaidiwa burebure.

37. Wanawake watibeli nao hawapendi burebure. Kulipiwa lipiwa. Kusaidiwa saidiwa. Kupewa pewa. Uanamke sio Kilema.

38. Ndio maana binti za Tibeli kamwe hawawezi kudharauliwa na kudharaulika.

39. MTU yeyote anayependa kusaidiwa saidiwa, burebure, kupewa pewa. Iwe mwanamke au mwanaume lazima adharaulike. Na tutamdharau dunia ingalipo.

40. Wahenga walisema amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu.

41. Usioe mwanamke aliyelaaniwa, anayependa burebure, kupewa pewa. Utaleta kizazi cha burebure Chenye laana.

42. Usiolewe na kijana/mwanaume anayependa kusaidiwa saidiwa, burebure, kupewa pewa, anayetegemea sijui babaake, sijui ndugu zake. Hamna kitu hapo. Ni mwanaume asiye na maamuzi, aliyelaaniwa, ambaye unastahili kumdharau.

43. Kwa kifupi,usikubali kudharauliwa na kujidharau. Wewe ni Mtu. Linda Utu wako.

Sina la ziada.

TaikonMaster
Kwa sasa Makumbusho, Dar es salaam
 
Africa hii wengi wanaamini lazima afanikiwe baba au kaka ndipo nao wafanikiwe
 
Back
Top Bottom