Ukikuta Mwanao wa kike Darasa la 6 anaangalia Ngono, unapaswa kufanyaje kumsaidia?

Ukikuta Mwanao wa kike Darasa la 6 anaangalia Ngono, unapaswa kufanyaje kumsaidia?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
Mwili wa mtoto Vaileth Soka (13) aliyefariki dunia kwa kudaiwa kujinyonga umeagwa katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Kibosho Umbwe wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro kwa maziko.

Baba mzazi wa mtoto huyo, Innocent Soka, akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Julai 23, 2026 amesema tukio hilo limempa pigo kubwa, lakini anamwachia Mungu. Amesema alikuwa akiishi na watoto wake wawili wa kike baada ya kutengana na mama yao, lakini sasa amebaki na mmoja.

"Binti yangu alikuwa mcheshi na asiyependa kuweka vitu moyoni, ila nimesikitishwa na sikutegemea kuchukua uamuzi mgumu kama huu," amesema Soka.

Amesema tukio hilo lilitokea Jumamosi Julai 18, 2026, siku ambayo hakukuwa na masomo kwa kuwa Vaileth alikuwa akisoma darasa la sita katika Shule ya mchepuo wa Kiingereza Mirerani.

CHANZO:-
Soka amesema chanzo cha tukio hilo kilikuwa kumkuta mtoto huyo akiangalia maudhui yasiyofaa kwenye luninga kupitia flashi ambayo hakujua ilipotoka"

Mtoto alikuwa anaangalia pono huku akijisugua, ni darasa la sita na pono zilikuwa kwenye flash, Je wewe kama mzazi ukimkuta mwanao anaangalia, utampiga, utamkaripia, utavunja Tv ama utakaa kimya?

Ushauri Dr Adam Francis DR HAYA LAND Doctor Mama Amon Mshana Jr Advocate_Silayo raraa reree miss Jane Miss Eagle dorothcharlz GwajiBoy TANESCO

1.jpeg
 
Moose Bull inasikitisha sana hii.
Alipomkuta anafanya hivyo angemkalisha chini na kuanza kumweka sawa.

Siku zote ukimkuta mtu anafanya jambo baya au la aibu halafu ukamwacha bila kuongea huwa anajiuliza maswali mengi sana na magumu, na hatimaye kujidhuru au kumdhuru huyo aliyemwona akiwa anatenda jambo hilo.
 
Kuna mshenzi mmoja hapo juu eti anasema "baba angemtafutia kijana wa kumwondoa hamu " huyo mtoto, mimi nasema hiyo si suluhu,.

hili la kumkalisha chini ni wasomi wa saikolojia ndio wanajua na ndio maana nimeita madaktari watusaidie, sisi ni makofi na mbata za hatari zingeshuka.
 
Aisee, ukiwa mzazi jitahidi kujua saikolojia ya binadamu. Kuna jamaa alimfumania mkewe anashiriki ngono na Basha mmoja hivi, halafu akawaacha kama walivyo bila kuongea.

Mke alipoona jamaa haongei nadhani kimoyomoyo akajisemea, "huyu mtu anataka kunifanyia kitu kibaya". Dah! Time mwanamke akamvizia mumuwe akiwa amelala na kumuua 😭.

Ukimya (wa aliyeshudia/aliyetendewa jambo) siku zote huchanganya mtu(aliyetenda jambo) kiasi cha kufanya uamuzi usiosahihi!
 
Hapo inabidi ukae naye chini umueleze madhara ya hilo jambo, bila kuficha chochote.

Kwa dunia ya leo huwezi kabisa kuzuia mtoto asione ponografia. Kuwa na urafiki na mtoto kunazidi kuwa jambo la muhimu sana.

Wengi tulipigwa na kukaripiwa kwenye haya masuala tukawa waoga, tukafanya kwa vificho, wala hatukusaidika.
 
Mimi kama Millenial huyo mtoto angekuwa binti yangu ningemuita ..namuagiza soda mbili tunakaa nje kwenye bustani ya nyumbani kisha namwambia ulichofanya ni hali ya kibinadamu na lazima kila binadamu aipitie ,hata mimi na mama ako tumefanya ndio mana ukazaliwa wewe ila wewe bado utakiwa usome umalize shule utaleta mwanaume wako tutawapa baraka zenu ili nanyi mkafanye hivyo sawa mwanangu? ...pia usitazame hizo video zitakuletea mazoea hutafurahi ukiwa na mwenza wako muda ukifika unanielewa binti yangu kipenzi? Aya maliza soda yako kanunue viazi na nyama leo nina hamu tule chips mwanangu.FULL STOP

Kuna kitu nawaambia ambao tumezaliwa na wazazi wa 1950s- 1960 hiki ni kizazi cha kipuuzi sana ndio mana hata nchi yetu kuna baadhi ya mambo hayaendi kwa ujinga wao najua mama yangu yupo hili kundi na baba pia ukoloni wa kipuuzi kila muda na ndio mana mimi siwezi omba ushauri kwa mzee bora kijana mwenzangu.
 
Hapo inabidi ukae naye chini umueleze madhara ya hilo jambo, bila kuficha chochote.

Kwa dunia ya leo huwezi kabisa kuzuia mtoto asione ponografia. Kuwa na urafiki na mtoto kunazidi kuwa jambo la muhimu sana.

Wengi tulipigwa na kukaripiwa kwenye haya masuala tukawa waoga, tukafanya kwa vificho, wala hatukusaidika.
Umeshauri vizuri sana. Haya Hebe eleza vizuri hapo uliposema, "...tulifanya kwa vificho, wala hatukusaidika".
 
Back
Top Bottom