Ukikutana naye........UTAMUULIZA?

Ukikutana naye........UTAMUULIZA?

tukitaabika ndo tunamkumbuka ....lol!!

akitupa raha tunasahau hata kama yupo, hadi tena atukumbusheee...

ni sehemu ya maisha bana, shida kidogo raha kidogo, wengine shida kwa kwenda mbele basi alimradi vururuvururu...

wee biggy hebu mwache Mungu bana! humuwezi

"with fire we test gold, with gold we test our servants"....(usiniulize nimemkoti nani...ni maneno ya Mungu hayo)

Hilo nalo nalo......barikiwa.
 
  • Thanks
Reactions: bht
Mi ningemwuliza Mungu kwa nini 2nazeeka na kuwa wa bibi na wababu? C ange2acha2 na ujana wetu 2endelee kufaidi dunia na bila kufa?
 
Hahahahah.........Dah...hayo maneno ya Mungu mi hoi.....Lakini Mamushka, tukiwa na raha tukamsahau, bado sia ana uwezo wa kutukumbusha bila kutuumiza?...........Yeye si ana nguvu zote? Hivi wewe mwanao akikusahau ucamchapa au unamuuliza kwa upole kwanini kakusahau?
 
Angekunasa kibao kwa kumsingizia uongo kwakuwa mimi ni baba yake baba yako.....Mi ni wa upande wa kiumeni

Hujambo Bombu mpenzi? Mwache Mungu aitwe Mungu, na aendelee kukaa hukohuko aliko.

Sijambo babu, ila hiyo mpenzi iondoe kwanza ili nikupe shikamoo. Bado naandika maswali ya kuuliza coz ninayo mengi sana
 
Sijambo babu, ila hiyo mpenzi iondoe kwanza ili nikupe shikamoo. Bado naandika maswali ya kuuliza coz ninayo mengi sana
Hivi kumbe hujui mjukuu ni mpenzi wa babu? Siliondoi mpenzi mjukuu wangu.

Haya fanya upesi na maswali yako, Mungu yuko busy, ataondoka muda si mrefu kurudi kwenye makazi yake......
 
Mi ningemwuliza Mungu kwa nini 2nazeeka na kuwa wa bibi na wababu? C ange2acha2 na ujana wetu 2endelee kufaidi dunia na bila kufa?
Hahahahaha hasa wewe uliyezaliwa mwaka 1986......... ndo kipindi chako cha kula raha.... hutaki kufa kabisaaaaa, sembuse kuzeeka LOL
 
Hahahahah.........Dah...hayo maneno ya Mungu mi hoi.....Lakini Mamushka, tukiwa na raha tukamsahau, bado sia ana uwezo wa kutukumbusha bila kutuumiza?...........Yeye si ana nguvu zote? Hivi wewe mwanao akikusahau ucamchapa au unamuuliza kwa upole kwanini kakusahau?

Rafiki, inategemea mwanao amekusahau kwa namna ipi.....maana kama ndo ameamua kuhamia kwa jirani kabisa na wala hakumbuki hata kama kuna baba....hivi hapo utamuuliza kwa upole kweli????!! Lazima utakuwa mkali kidogo....najaribu kuwaza tu....mhhhh!!!
 
God's tests are the healing medicine of those who are nigh unto Him, His sword is the ardent desire of all them that love Him, His dart is the dearest wish of those heartsthat yearn after Him, His decree is the sloe hope of them that ave recognized His truth.....

kama vipi kafanye marudio ya katekisimu biggy....
 
Asprin unatafuta makwenzi kutoka kwa huyo unayemtaja taja
 
Mamushka haya maneno ya Busara ya Mungu huwezi yaandika kwa kikwetu nikupate zaidi...lol
Nakusalimu tu Mshiki!!
 
  • Thanks
Reactions: bht
Wapendwa marafiki salamu,

Jana nlimpigia simu rafiki yangu. Alipokea akiwa na simanzi kubwa. Kumbe ndio alikuwa kapokea habari ya msiba wa kaka yake. Alikuwa analia na kuongea kwa shida. Nilihuzunika kwa niaba yake..........kama si nguvu ya Tusker Malt labda nami ningemwaga chozi. Mnywaji mwenzangu akashangaa kwanini nimepata simanzi ya ghafla, nikamsimulia.

Huyu mtu akaniambia neno ambalo limenifanya nitafakari kwa kina usiku kucha......... Namnukuu: "Ndugu yangu, Mwache Mungu aitwe Mungu na aendelee kukaa hukohuko aliko maana ningepata nafasi ya kukutana naye sasa hivi ningemuuliza KWANINI ULIMCHUKUA BABA YANGU nikiwa bado mdogo nikataabika namna ile?"........ Nilichoka na mpaka sasa nimechoka.....Jamaa alivyonisimulia maisha yake, jinsi mama yake alivyohangaika.......Kweli kila mtu ana swali lake.....Dah!

Nami najiuliza.... Hivi ningepata nafasi ya kukutana na Mungu akanipa nafasi ya kumuuliza au kumwambia chochote ningemwambia na kumuuliza nini?.....

Kwanza ningeanza na shukrani:
Ahsante kwa kuniumba Mwanaume..... manake angeniumba mwanamke ningemuuliza kwanini ameniumba mwanamke.
Ahsante kwa kunipa mke mzuri (japo kwa ubinadamu wangu huwa natelezaga) na mabinti wawili wazuri.
Ahsante kwa kunipa wazazi wanaonipenda na kunijali sana
Ahsante kwa kunipa ndugu, marafiki, majirani tunaoheshimiana na kupendana sana.

Then lazima ningemuuliza;

Kwanini tatizo hili limetokea kwenye familia yetu?..... Kwanini kwetu?......... Ningemuuliza mbona kila siku tunakuomba kwenye maombi/sala utuondolee hili tatizo lakini huliondoi?........Lazima ningemuuliza...Niape?

Kuna mtu mwingine huku angekuwa na Swali kama angekutana na Mungu na kupewa nafasi ya kumuuliza?

Kama alivyonambia ndugu yangu, mwacheni Mungu aitwe Mungu......... Na aendelee kukaa huko aliko.
AMINA.

Leo ODM yuko kimajonzi zaidi.
Harudi kitandani wala nini. Anajiuliza tu.
Hommie kuna ile amri ya "Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako" hivi kulitaja bure ndo inakuaje?
 
God's tests are the healing medicine of those who are nigh unto Him, His sword is the ardent desire of all them that love Him, His dart is the dearest wish of those heartsthat yearn after Him, His decree is the sloe hope of them that ave recognized His truth.....

kama vipi kafanye marudio ya katekisimu biggy....
Katekisimu mamushka haina majibu kutoka kwa Mungu.........Katekisimu si kaandika binadamu? Mi nataka Mungu anijibu direct... kama alivyoongea na Musa na Nuhu anipe na mimi nafasi kidogo ya kumuuliza japo kaswali kamoja. Au nimwombe kitu kimoja......

Rafiki, inategemea mwanao amekusahau kwa namna ipi.....maana kama ndo ameamua kuhamia kwa jirani kabisa na wala hakumbuki hata kama kuna baba....hivi hapo utamuuliza kwa upole kweli????!! Lazima utakuwa mkali kidogo....najaribu kuwaza tu....mhhhh!!!
Sasa rafiki ukimuuliza kwa ukali si ndio atakuogopa na kutokomea moja kwa moja?........Kama unampenda mwanao utamwachaje atokomee moja kwa moja? Labda kama humpendi. Mi naamini Mungu anatupenda, kwanini anamwacha shetani atufanyie visa? Kwanini asimuue atuache tujinafasi?
 
Asprin unatafuta makwenzi kutoka kwa huyo unayemtaja taja
Hawezi kunipiga kwa kuwa ananipenda na ameniambia: Tafuteni nanyi mtapata..... Namtafuta, nataka nimpate anijubu maswali yangu......

Hommie kuna ile amri ya "Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako" hivi kulitaja bure ndo inakuaje?
Ewaaaa, siku ukifanikiwa kukutana naye jaribu kumuuliza. Au na wewe utaogopa kama mamushka?
 
mh...! hilo ndo litakuwa swali la kwanza kwa nini babu anamwita mjukuu wake mpenzi? Halafu mlolongo na mvua ya maswali itamwandama
 
mh...! hilo ndo litakuwa swali la kwanza kwa nini babu anamwita mjukuu wake mpenzi? Halafu mlolongo na mvua ya maswali itamwandama
Bombu mpenzi kuwa na amani.... sitakuita tena hivyo.....Samahani kama nimekukwaza.
 
Ila amesema usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako si unaikumbuka hii amri na amesisitiza kabisa
Huoni hapa unamtajja taja bure
 
Ila amesema usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako si unaikumbuka hii amri na amesisitiza kabisa
Huoni hapa unamtajja taja bure
Siamini kama nimelitaja bure. Nataka nimjue zaidi. Nimuulize maswali. Anisaidie.......

Kutaja bure ni kama hivi: Unamwona binti mrembo anapita kafungasha masaburi ya haja, guu kama chupa ya bia, sura kama Cleopatra......afu badala ya kuendelea na biashara yako we unapiga shingo feni afu unaibuka na "Mungu wangu, ningempata huyu demu, sitatumia kondom wallah) .......Sasa huku ndio kulitaja bure jina la Mungu..............Sawa eh?
 
Bombu mpenzi kuwa na amani.... sitakuita tena hivyo.....Samahani kama nimekukwaza.

Asante babu, na ubarikiwe na ukifanikiwa kumuuliza kheri, hope atakujibu yote kwa ufasaha na upendo mwingi.
 
Back
Top Bottom