Nilikuwa najuaga mwanamke kunywa pombe ni aibu kubwa, kumbe ni kawaida bana. Nilipoenda chuo nikakutana na mdada wa kishua tukawa marafiki.
Alikuwa akitumia pombe za gharama sana hata kwao wote wanatumia pombe. Alijitahidi kunifundisha pombe ila ilishindikana kabisa.
Aliwahi niambia hivi " my wii mimi nakupenda sana kwa sababu hutumii pombe nikipata shida wewe ni mtu wa kwanza kunifata popote"
Na kweli mimi nilikuwa siendagi club, ila akienda mara nyingi alikuwa akinitumia sms ' wii niko sehemu fulani niko na watu fulani, kesho mapema nipigie sim uone kama nimerudi"
Nilichokuwa nampendea akilewa sio kwa kiingereza kile [emoji23][emoji23] siku moja tulienda kula baadae akaagiza wine alikuwa akichanganya na pombe nyingine. Sasa kuna kaka mmoja akapita kwenye meza yetu akamkanyaga bahati mbaya aiseee aliongea kiingereza sikuwa kumuona hata class akichangia vile nilicheka sana. Kesho yake nikamkumbusha alikana kila kitu.
Mimi naenjoy kumtizama mlevi. Mlevi anachekaga sana, some times anaimba mlevi hanaga stress