Ukimaliza chuo ukakaa mtaani miaka mitano bila ajira, mifumo ya ajira serikalini inakutema

Ukimaliza chuo ukakaa mtaani miaka mitano bila ajira, mifumo ya ajira serikalini inakutema

Chukulia mfano umemaliza chuo mwaka 2015, 2016, 2017, 2018 na 2019 kishuka chini alafu jaribu kuomba ajira serikalini.

Pitia vigezo vyote kabla ya maombi 😀 kivyovyote vile lazima kuna kigezo kimoja utakuwa haukidhi hasa hasa umri. Mfano Tangazo la ajira za polisi la juzi.

Watu wamesoma engineering miaka minne, wengine medicine miaka mitano, wengine veterinary medicine miaka mitano, wengine education mitatu kisha wakakosa ajira wakakaa kitaa miaka mitano bila bila.

Wakijaribu kuomba lazima kuna kitu kina kosekana.

Graduates mmejipangaje?

Wajukuu zangu zangu naomba mnisikilize ......

Mimi ni babu ambaye nilimaliza chuo kikuu zamani sana Nina uzoefu wa mifumo ya ajira kwa muda mrefu sana naombeni mnisikilize kuhusu hizo ajira zenu .......

1.kuwa na vigezo au kutokuwa na vigezo sio issue muhimu ni kuwa na connections

2.ajira zenyewe sasa kwa kipindi chenu ambacho kila mwaka Graduates zaidi ya milioni moja wanamaliza vyuo vikuu alafu mnapigania nafasi moja na bado una mawazo ya kuajiriwa .

3.mwisho kabisa nawakumbusha wapiga nia ajira sikumbuki ilikuwa sijui ni mwaka Gani wazee wenu tulifanya interview uwanja wa taifa majibu kutoka kumbe watu walishaweka ndugu zao sasa sijui kilitokea kuna mwamba akasanua Habari zilivyofika kwa wakubwa zikafutwa wenye kumbu mtanisaidia .


Nina mengi ya kuwaeleza wajukuu wangu ila kwa sasa babu yenu nimejiajiri na maisha yanaenda sio lazima uajiriwe
 
miaka yote mitano hujafungua hata genge la kuuza nyanya unasubiria ajira za siisiiemu, kutakuwa kuna hitilafu mahali, maana hata hao wenye hizo ajira wanahangaika kuuza vitumbua ili watoke, kimsingi elimu yetu imekaa kiubwenyenye sana yaani watu hawana kabisa fikra za kujiajiri.SHAME.

Hapo ndani ya miaka mitano unakuta tiyali ameshafanya interview kibao kila anapokwenda akimaliza interview wanamwambia tutakuita na bado a asubili kuitwa na miaka 5 imeshapita tiyali .
 
Back
Top Bottom