- Source #1
- View Source #1
Wakuu nimekutana na hii concern ya mdau nikaona si mbaya nikiieleta hapa kupata ufafanuzi zaidi.
- Tunachokijua
- Mdau amehitaji kujua je ni sahihi mtu kumeza dawa tena iwapo ametumia dawa na kuitapika baada ya dakika 10 ama muda mfupi baada ya kunywa.
Tovuti ya vinmec inaeleza kuwa mambo kadhaa yanapaswa kuzingatiwa unapoamua ikiwa utameza tena dawa baada ya kutapika. Mambo hayo ni;
- Ugonjwa unaotibiwa,
- Sifa za kifamasia za dawa hiyo mwilini (pharmacokinetics),
- Uwezo wa dawa kufanya kazi bila kuleta madhara (therapeutic window), na
- Madhara yanayoweza kutokea (side effects).
JamiiCheck imewasiliana na Afisa tabibu kutoka mkoa wa Dodoma, Isack Chelleah ambaye ameeleza kuwa ikitokea mgonjwa ametapika dawa anapaswa kuachwa apumzike kwa dakika 10 au 15 kisha apewe dawa nyingine kwa kuwa kitaalam inamaanisha atakuwa ametapiga hiyo dawa na itakuwa bado haijaingia katika mzunguko wake kama ilivyotarajiwa.
Anaendelea kueleza kuwa;
Hivyo, baada ya muda huo kupita akiwa ameshapumzika, apewe dawa nyingine anywe ili kuangalia kama anaweza kumeza, na akimeza aangaliwe kama atatapika tena.
Ikitokea ametapika tena mara ya pili, inamaanisha kuwa bado anaweza kuendelea kutapika, hivyo anaweza kubadilishiwa njia ya kupewa dawa.
Itabidi itumike sindano kumchoma kuzuia kutapika, kisha baada hapo dawa aliyokuwa anapewa kwa vidonge apewe kwa njia ya sindano kwa kuwa inawezekana.
Saa chache baadaye inaweza kuwa after 10 hours atakapotakiwa kuendelea kupewa dawa basi apewe kwa njia ya vidonge ili kuona kama atakuwa amekaa sawa.