Ukimiliki laini zaidi ya moja ya mtandao mmoja utalipa faini Tsh 5M au kufungwa gerezani kwa miezi 12 au vyote kwa pamoja kuanzia 1 Julai, 2020

Nchi hii ina upumbavu mwingi sana, hata nikiwa na laini 5 za voda tatizo lao nini? Mimi si ndo najua matumizi yake?
Mpaka sasa nina line hizi

Voda-3
Airtel - 2
Tigo-2
Ttcl-1
Halotel-2
Kabisa nkamu

Unashindwa kuelewa tatizo ni nini? Ingekuwa magari tungesema tatizo foleni, sasa mimi laini zangu 10 nimesajili kwa NIDA tatizo lao nini?
 
Mimi nataka nijaribu sumu kwa kuionja. Nina laini zaidi ya moja kwa tigo na airtel na nimeshindwa kuiacha moja bila shuruti.
Mkiona sionekani jukwaani mjue tayari.
 
Kabisa nkamu
Unashindwa kuelewa tatizo ni nini? Ingekuwa magari tungesema tatizo foleni, sasa mimi laini zangu 10 nimesajili kwa NIDA tatizo lao nini?
Acha ubishi Mkuu, km Lugha inakupiga chenga uliza wenzako. HAIRUHUSIWI kuwa na Line zaidi ya moja kwa mtandao mmoja, kwa kitambulisho cha NIDA kuanzia July Mosi 2020 km unayo katoe taarifa nenda post #43
 
Wakuu heshima kwenu, kuna wakati nlisikia kuna sheria TCRA inatulazimu kuwa na ulazima wa kumiliki line moja kwa kila mtandao na mwisho ni tareh 30 Juni, 2020, hii imekaaje? Tutafungiwa laini leo?

Harafu waambie wangeandika kwa Kiswahili mimi nipo tarime sijui kusoma hiyo.
 
Mambo za majina sijui namba TANO ni ya zamani sana, siku hizi hivi viwakala uchwara tu njiani vinafufua.... buku mbili tu bwashee.
Taratibu Bwashee, ni akili ya aina gani unadaiwa 1,700,000/ Line za mitandao miwili iliyofungiwa eti unaenda kwenye viwakala vya mwamvuli unalipa Buku 2 ufufue Deni la 2M na riba zake wewe sijui kabila gani Mangi, unamfuata mdaiwa wako unawajua kwanza hao waliojiunga na mitandao kutukopesha? unajua walishafikishwa Mahakamani? Uliza
 
Nimetoka kuongea na wahudumu wa voda na tigo, wote wanasema kumiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja sio kosa ila tu ziwe na usajili halali na matumizi halali.

Kwa mujibu wao unatakiwa kwenda kwenye mtandao wako ukaainishe unazitumiaje! Mfano labda una laini ya kupokelea pesa kwa ajili ya biashara yako na kuwasiliana na wateja, pia una laini binafsi ya kuwasiliana na ndugu familia nk.
Nimeridhishwa angalau na majibu haya.
 
Kwani kuna ulazima gani wa kumiliki laini nyingi za mtandao mmoja?
Hapo nawapongeza TCRA.
Ndio kupunguza gharama za kupiga. Waweza kuwa nazo laini hata nne za mtandao mmoja kupunguza gharama za kuwasiliana ya kwanza ya ofisi ya pili ya nyumbani ya tatu yako mwenyewe ya nne ya mwanao ambaye hajafikia umri wa kuwa na kitambulisho cha taifa ili asajiliwe anayesoma tuition mbali.
 

Bwashee kabila langu linaingiaje hapo!

Ulisema line zako zilikuwa na ‘mikopo’ na ukaenda ofisini ili kuzifufua, ulichokwama ni majina matano tu ila lengo lako ilikuwa kuzifufua!

Hoja yangu sio kutetea mikopo yako, na kwanza wala sikujua kama ni unadaiwa ama unadai, nilijikita kwenye uwezekano wa kuzifufua kwa njia nyingine.

Nkong’wanzoka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…