Hivi ukiamua kuoa au kuishi unataka uishije, kwa kudanganya danganya au kwa kutenda wema? Kanuni ya maisha ni kuwa mtu mwema na sitaki kuiga tabia za watu wengine, ikiwemo ya mke wangu (kama ni mbaya) inibadilishe na mimi nianze kuwa mtu mbaya. Wanandoa - mume na mke - kila mmoja ana udhaifu wake. Baadhi ya wanandoa hukubaliana kubadilika na kuzifanyia kazi tofauti zao na huwa mfano kwa wengine. Wanandoa wengine kila mmoja anabaki kama alivyo (kumwona mwenzake tu ndiye mbaya na yeye ni mwema). Hawa hawana muda wa kukaa pamoja na kujadiliana wafanye, isipokuwa matatizo ya ndoa yao huyapeleka kwa watu wengine ambao hata hawawezi kuwasaidia. Mwisho wa siku wanandoa kama hawa hujikuta wameshaweka ufa mkubwa katika mahusiano yao (kati yao) kiasi kwamba hawana njia ya kuuondoa huo ufa, isipokuwa kuishi kijanja janja tu. Wanandoa wakishafikia hatua hii kila ushauri wataona haufanyi kazi. Binafsi nataka to do my best. The rest, namwachia Mungu na ikitokea tukafarakana sikati tamaa na wala silalamiki, maana nilichokifanya ndicho hicho nilichoweza au nilichotakiwa kufanya. Lakini sasa kama unaishi na mtu kwa kutenda mambo nusu nusu au kijanja janja, je mkifarakana utaona uliyoyofanya ndiyo uliyotakiwa kufanya?